Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe sidhani kama yamechochewa kisiasa. Natamani kukutana na Wapinzani

Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe sidhani kama yamechochewa kisiasa. Natamani kukutana na Wapinzani

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,015
Reaction score
2,680
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.

Wafuasi wa Bwana Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa.

Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.

BBC
---

UHURU WA KUJIELEZA

Kikeke:
Tanzania unayoingoza sasa hivi ina Uhuru wa Kujieleza na Demokrasia ya kutosha?

Rais Samia: Ahaaha! Wewe ni mwandishi wa habari toka umefika umesikia vyombo vya habari vimelalamika? Hakuna chombo kimelalamika kuna uhuru wa kutosha wanajieleza, na wanajieleza mpaka wanavuka mipaka saa nyingine. Lakini kwasababu viongozi inabidi mvae ngozi ngumu muangalie.

Lakini wakati mwingine kusema kwao bora umpe nafasi mtu a-offload alichonacho atoe umsikie kama kiongozi useme kumbe kinalalamikiwa hiki, basi unakifanyia kazi kuliko ukiwabana hawasemi, hujui wanafukuta na nini ndani, ile! Sasa Tanzania kuna uhuru wa kutosha, vyombo vyote vya habari viko huru, anayefuata sheria, anayefuata maadili ya kazi yao wako wanafanya kazi yao.


DEMOKRASIA

Kikeke:
Demokrasia ya Kisiasa?

Rais Samia: Demokrasia ya Kisiasa, Yes ipo. Na hapa naomba nitofautishe baina ya Demokrasia ya Kisiasa na fujo za kisiasa.
Demokrasia ya Kisiasa ni nini? - Demokrasia ya Kisiasa tuna vyama vya Siasa, wana vyombo vyao, wanajadili mambo yao kwa mfano baraza la vyama vya siasa. Huko wanajichagua wao, wanajadili mambo yao ya kisiasa wanaelewana. Kuna kamati ya vyama vyenye wabunge Bungeni na wenyewe wana ya kwao, wakakaa wanazungumza wanajadiliana huko. Lakini kuna vyama vyenyewe vya siasa ambavyo vimeundwa na Katiba zao, na kwenda kwao au kufanya kwao kazi kunategemea katiba zao.

Kwa mfano chama changu cha Mapinduzi, Katiba yangu inaniambia labda katika mwaka nitakuwa na vikao viwili vya Halmashauri Kuu ya Chama, Labda Vikao 6 vya Kamati Kuu na vikao vingine katika ngazi za chini Mikoa na Wilaya. Na hivyo vikao vimeelezea wajumbe ni wakina nani na kila kitu. hivyo Vikao vinaendeshwa bila bugudha bila kuomba ruhusa polisi kwasababu Katiba imeshaelezwa na imeshapita kote na inajulikana. Na vivyo hivyo vyama vingine vyote vina katiba zao, zina system zao za Mikutano, wajumbe wao ni kina nani, hivyo wako free kufanya wakati wowote.

Kitu ambacho hakipendezi ni ile kutaka uhuru wa kufanya fujo za kisiasa, labda tumemaliza uchaguzi, Serikali imeundwa. kinachotakiwa kuendelea ni kujenga nchi uwe na chama gani wote mnakuja pamoja mnajenga nchi yenu, ndicho kinachotakiwa kuwa.

Lakini kinapotokea chama, wao wanataka tu kuitisha maandamano kila siku, maandamano yasiyo mwisho, sijui maandamano nini, labda leo mkutano huko, kesho mkutano huko fujo vurugu, aaah ile

Kikeke: Ndio Uhuru wa Demokrasia

Rais Samia: Hapana, kama uhuru wa Demokrasia mbona Marekani hawa-observe, mbona Ulaya hawa-observe? Wakimaliza chaguzi ni kimya, wanaendelea shughuli zao za maendeleo, nchi inapewa nafasi inafanya kazi zake wanajijengea nchi zao. Hatujasikia vurugu za kila siku za huko Marekani na Ulaya, kama kutatokea maandamano ni Constituency ndogo wamekosa umeme jana na juzi umeme umekuja low Voltage wanaandamana mtaa huo wanakwenda kwa huyo mwenye umeme huko, wanasema ya kwao wanarudi peacefully. Sasa haya ya kwetu ya vurugu, piga magari, choma.. ah aha

KESI DHIDI YA FREEMAN MBOWE
Kikeke:
Nazungumzia suala hilo la kisiasa kwa sababu kiongozi wa upinzania Freeman Mbowe amefikishwa Mahakamani, amefunguliwa mashataka ya Ugaidi, wananchi wake wanasema mashtaka haya yamechochewa kisiasa

Rais Samia: Mimi sidhani kama yamechochewa kisiasa kwasababu navyojua Mbowe alifunguliwa Kesi mwezi wa Tisa mwaka jana (2020), kwa hiyo yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashtaka ni ugaidi na kuhujumu uchumi. Nadhani wenziwe kesi zao zimesikilizwa na wengine wameshapewa sentence zao wanatumikia. Yeye (Mbowe) upelelezi ulikuwa haujeisha, uchunguzi ulikuwa unaendelea so amekwenda amefanya tumeingia kwenye uchaguzi, amemaliza uchaguzi nadhani sasa Polisi wamekamilisha uchunguzi wao, wamemuhitaji waendelee na kazi yao, Lakini kwa sababu na kama utakumbuka Mbowe hakuwepo nchini alikuwa Nairobi, sasa kwanini kakimbia sijui. Lakini alivyoingia tu nchini Kaitisha maandamano ya Katiba na madai ya katiba. Nadhani ni Calculation akijua kwamba ana kesi ya aina hiyo na hii vurugu ambayo ana-instigate akikamatwa aseme mmhh! kwasababu ya Katiba, kwasababu tumeitisha Katiba... nadhani sina hakika.

Lakini kwa sababu jambo liko mahakamani, sina uhuru wa kulizungumzia kwa sana. Nadhani tuache Mahakama zioneshe ulimwengu kwamba hizo shutuma walizomshutumu zilikuwa za kweli au siyo za kweli Mahakama itaamua.

KUKUTANA NA WAPINZANI
Kikeke: Na Katika Suala hilo hilo la Siasa za upinzani, ulivyoingia madarakani ulisema uko tayari kuzungumza nao na hata Mbowe alikuwa anauliza ni lini utakutana naye, lini utakutana na viongozi wa upinzani?

Rais Samia: Nimesema nitakutana nao lakini sikutana kukutana nao wakiwa wamechambuka chambuka, kama nilivyokueleza hawa watu wana vyama vyao vidogo vidogo, wana mabaraza yao. Nilitaka kwanza wajiunge kwenye mabaraza yao. Na Baraza la Demokrasia nadhani la Vyama vya siasa wamefanya uchaguzi wiki mbili zilizopita au wiki iliyopita ndio wamejiunda vizuri. Kwa hiyo kama wamejiunga vizuri, na hizi kamati zao ndogo ndogo zimejiunda vizuri, basi tutatafuta tu siku tuitane tukae tuzungumze kwasababu hata mimi nataka kuzungumza nao niwaambie mwelekeo wangu kwamba sasa tumemaliza uchaguzi twendeni tukajenge nchi.

Na kwenye kujenga nchi mimi sichagui, nikimuona mpinzani amekaa vizuri ana mwelekeo namuweka kwenye serikali yangu twende tukajenge nchi kwasababu hakuna pahala pamesema baada ya uchaguzi chama kilichoshinda peke yake ndicho kitajenga nchi, hapana.

Tumesema watanzania tutajenga nchi. So Mtanzania yeyote mwenye ideology yoyote ya kisiasa kama ni mzuri anaweza ku-deliver na kuleta yale ambayo wananchi wanataka mimi namtumia tu, namuingiza kwenye system zangu tu twende namtumia

Kwa hiyo nataka waje tukae tuone tunakwendaje na hili, kwa hiyo wakati ukifika nitawatafuta, nitawaambia karibuni njooni tukae.

 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.

Wafuasi wa Bwana Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa.

Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.

BBC
Maza katili kabisa kuwahi kutokea
 
Screenshot_20210805-122956_1.jpg
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.

Wafuasi wa Bwana Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa.

Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.

BBC
Hana hamu alikuwa anatetema na kurembua magololi kama pia! An incompetent nincompoop
 
Mahojiano ya Leo nimepata mstuko kuona inaelekea Mh. Rais kesi hii nzito ya shutuma za ugaidi na uhaini anayoshutumiwa Freeman Mbowe na wenzake 4 haifahamu vizuri. Maana Mh. Rais Samia Suluhu anasema wenzake na Mbowe tayari kesi yao ilishahukumiwa. Pia Mh.Rais kusema hizi vurugu za kuchoma magari na maandamano ya barabarani Tanzania hawazitaki, sijui ni Tanzania gani katika miaka 5 iliyopita tumeona magari, mali yakichomwa na wapinzani au hata maandamano barabarani. Ni kama hizi 'vurugu' azionazo Mh. Rais labda ni za nchi zingine lakini hazijawahi kutokea ktk utawala wa awamu ya 5 wala hii ya awamu ya 6.

Mbinyo unazidi, CCM baada ya miaka 5 na miezi miwili hatimaye Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Mh. rais wa awamu ya 6 imebidi aachane na yale ya awamu ya 5 kukwepa mahojiano na vyombo vikubwa vya habari kama BBC na kulazimishwa kuitetea serikali yake na ilani ya CCM.

Baada ya BBC nahakika watafuata MEDIA zingine za kimataifa kutaka kuongea na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan na maswali yatazidi kuwa magumu na ndiyo maana mwendazake (revered) hayati rais John Pombe Joseph Magufuli hakutaka kufanya mahojiano na chombo chochote cha media / habari cha kimataifa, kikanda au kiTanzania.

Kwetu sisi tunasibiri muendelezo mpya wa Mh. Rais kukubali kufanya mahojiano na media mbalimbali maana kina Jaji Mkuu, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dr. Bashiru Ally Kakurwa aliyekuwa katibu mkuu CCM, Dr. Abbas, Msigwa wa MAELEZO , Humphrey Polepole, Shaka wa CCM, IGP Simon Sirro, DPP, Regional Commissioners, maDC n.k wote hawa press conference zao au mahojiano hayakukidhi kiu watanzania kuelewe kiongozi wao wa juu kabisa wa nchi ana maono, ideolojia, itikadi na fikara gani kuhusu yanayotokea ktk utawala wa awamu ya 5 na awamu ya 6.

Rais Samia Ahojiwa Kuhusu Mashtaka ya Mbowe​

August 9, 2021 by Global Publishers

samia-4.jpg


RAIS wa Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

salim_kikeke.jpg


Kwa mujibu wa BBC, katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC, Salim Kikeke, Rais Samia amesema Mashtaka dhidi ya Mbowe hayajachochewa kisiasa, ana imani sheria itachukua mkondo wake.



Wafuasi wa Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa. Aidha, katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha. Mahojiano hayo yatarushwa leo Jumatatu, kupitia Dira ya Dunia ya BBC
 
Sawa sisi tupo tunaangalia mkondo kwa makini Maana umeanzia kwenye bumping uelekeo wake ndo haujulikani!
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.

Wafuasi wa Bwana Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa.

Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.

BBC
Akina Rugemalila wako sero sasa mwaka wa tano. Kusema kuwa sheria itachua mkondo wake haitoshi ...... Dhulma huwa haina tabia ya kujificha. Hata serikali za Makaburu na Wakoloni, sheria zilichukua mkondo wake ....!!
 
Back
Top Bottom