Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe sidhani kama yamechochewa kisiasa. Natamani kukutana na Wapinzani

Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe sidhani kama yamechochewa kisiasa. Natamani kukutana na Wapinzani

Kajifundishe Kiswahili, neno kudhani, katika kiswahili, lina maana nyingi,mojawapo unaposema nadhani ni kuwa na uhakika na unachosema. Ni kama mtu kuulizwa,"Utaendelea kusoma?"Na akajibu "Nadhani hapa ndio mwisho". Ikiamanisha kuwa ana UHAKIKA, haendelei tena kusoma.
Hahahaah ndio nasikia Leo! Anyway asante kuchangia
 
Hahahaah ndio nasikia Leo! Anyway asante kuchangia
Maneno mengi ya Kiswahili,hayana maana moja, yana maana pana.Kutokana na maneno mengi ya Kiswahili,yanatokana na maneno ya kiarabu.Neno dhana,hasa linakuja kwa upande mwingine, kuwa na uhakika wa jambo fulani.Ikiwa jambo huna uhakika nalo,ndio unatumia neno 'sidhani'(sina uhakika),ila ukisema nadhani(nina uhakika). Kajifundisheni kiswahili. Watu wengi,wasiokuwa wenyeji wa mija ya Pwani(kwenye chimbuko la Kiswahili)hupenda kujifanya wanajuwa Kiswahili.
 
Natamani kuona mkondo wa sheria
Maana watu wanasemaga kila mara sheria itachukua mkondo wake
Mara huoni mkondo wala nini kesi inayoyoma
Kinachoniboa ni pale wanapoona maji yanakaribia kuvuka shingo, utawasikia, DPP AMEAMUA KUFUTA KESI, AMEONA HANA SABABU YA KUENDELEA NAYO...!!
 
Hahahaah ndio nasikia Leo! Anyway asante kuchangia
Kuna Nadhani(nina uhakika),na Sidhani(sina uhakika).Kiswahili kina maneno mengi ya kiarabu,neno dhana(asili yake ni kiarabu),linatumika sana kwa watu wa Pwani.Tofaitisheni 'Nadhani'(nina uhakika) na 'Sidhani'(sina uhakika).

Hii lugha ya Kiswahili,kwa mtu aliyezaliwa mikoa ya bara ya Tanzania,kuweza kumuelewa mtanzania,aliyezaliwa mikoa ya Pwani,afanye kazi sana kumuelewa kimakini.
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi...
Amesema nini kuhusu viongozi wa CHADEMA kila sehemu kuwekwa mahabusu, au hilo nalo ni swala la "sheria itachukuwa mkondo wake", hata kama ni sheria yenyewe inavunjwa na wanaotakiwa kusimamia hizo sheria?

'Maza Mizinguo' anadhani watu hawana akili kujuwa yanayofanyika sasa hivi?
 
Kinachoniboa ni pale wanapoona maji yanakaribia kuvuka shingo, utawasikia, DPP AMEAMUA KUFUTA KESI, AMEONA HANA SABABU YA KUENDELEA NAYO...!!

Kufuta kesi zilizothibitishwa kukidhi kigezo cha kufutwa nayo ni kazi ya dpp
 
Urais ni taasisi ndugu yangu mambo mengine yanafanyika hata yeye "NADHANI" huwa hajui. Rais hasilaumiwe sanaa
Taasisi kwenye ugaidi hauwezi kutangazwa bila Amiri jeshi mkuu kujua mazingira yote.
 
Rais SSH amehojiwa na Salim Kikeke wa BBC Swahili, kwa mtazamo wangu, yeye kama Rais hakutakiwa kutawaliwa na matumizi ya neno "nadhan"! Yaani majibu na maelezo yake yote yeye ni kudhani tu.

Kuna umuhimu wa kufundishwa namna nzuri ya kujibu maswali kama kiongozi wa nchi. Huku kudhani, unadhani means huna uhakika.

Hana uwezo huyo Mkuu.
 
Mnatoka nje ya Mada,baada ya kuona,hamuelewi Kiswahili.Neno dhana,lina 'nadhani'(nina uhakika),na 'Sidhani(sina uhakika).Jifundisheni Kiswahili kwa watu wa Pwani.Moja Kati ya mchango mkubwa,wa Watu wa Pwani,ni kiswahili,lugha ya Taifa,na iliyonea Afrika mashariki na Kati na Dunia nzima.
 
Mama kama anataka kukilinganisha Chadema na Chauma au LTP basi atakuwa anafanya makosa sana. Hivi vyama havina uzito sawa!! Kwa hiyo atakapowaita Ikulu inabidi aangalie hilo .... Shibuda hawezi kuaminiwa na CDM au ACT ingawa anaweza kuwa ndiye kiongozi wa Balaza.
 
Mada ni neno Nadhani(nina uhakika).Mwatoka nje ya mada.Baada ya kuona mleta uzi,hajui maana halisi ya neno Nadhani(nina uhakika),na kinyume na si dhani(sina uhakika).
 
Back
Top Bottom