Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe sidhani kama yamechochewa kisiasa. Natamani kukutana na Wapinzani

Majibu yake yamekaa vizuri sana. Amejibu kama Rais huku akichukua tahadhari zote kutokuingilia uhuru wa mahakama. Ulitaka aingie kwa undani ili uje useme ameingilia uhuru wa mahakama?. Viva Rais Samia
Umefafanua vizuri sana.Kama ni mwalimu,basi itakuwa wanafunzi wako,wanakuelewa vizuri,labda awe mwanafunzi kilaza.
 
Hata mimi kuniambia ukasema "nadhani" basi hapo sikuamini tena sababu huna uhakika

Na anapata taarifa za kiintelejensia na kipolisi kila siku kuhusu hali ya kisiasa, usalama na kijamii ya nchi halafu Rais anakuwa kama hana uhakika na taarifa za Idara ya Usalama wa Taifa anazowakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa na zile za kutoka Idara ya Polisi anazowakilisha waziri wa mambo ya ndani na IGP..

https://www.intelligence.gov › presi.
What is the PDB?

The President's Daily Brief (PDB) is a daily summary of high-level, all-source information and analysis on national security issues produced for the ..
 
Hivi kesi ya 'amiri' au 'amurat' jeshi mkuu iliishaje?
Hivi si ni mama huyu huyu aliyetutangazia kuwa kesi zaidi ya 100 zilikuwa za kubambika na aliwaelekeza waziondoe Mahakamani?
Hakuingilia mahakama?
Nakushauri jifunze zaidi uelewe maana ya kuingilia uhuru wa mahakama na nafasi ya DPP kisheria na kikatiba. Usichanganye mambo
 
Tufanye ivi, Yeye kasema kuwa uhuru wa vyombo vya habari upo wa kutosha ila ninyi mnapinga si kweli.

Basi tuambieni ni vyombo vipi vya habari vimeminywa Au wanahabari wepi wameminywa.

Kama hamna Basi nashauri izo smart phone muache kuzitumia maana zinapunguza uwezo wenu wa kufikiri kadri siku zinavyojongea.
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.

Wafuasi wa Bwana Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa.

Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.

BBC
---
Kikeke: Tanzania unayoingoza sasa hivi ina uhuru wa kujieleza na Demokrasia ya kutosha?

Rais Samia: Ahaaha! Wewe ni mwandishi wa habari toka umefika umesikia vyombo vya habari vimelalamika? Hakuna chombo kimelalamika kuna uhuru wa kutosha wanajieleza, na wanajieleza mpaka wanavuka mipaka saa nyingine. Lakini kwasababu viongozi inabidi mvae ngozi ngumu muangalie.

Lakini wakati mwingine kusema kwao bora umpe nafasi mtu a-offload alichonacho. atoe umsikie kama kiongozi useme kumbe kinalalamikiwa hiki, basi unakifanyia kazi kuliko ukiwabana hawasemi, hujui wanafukuta na nini ndani, ile! Sasa Tanzania kuna uhuru wa kutosha, vyombo vyote vya habari viko huru, anayefuata sheria, anayefuata maadili ya kazi yao wako wanafanya kazi yao.
Mbowe should retire..
 
Unapofuta maana yake wakati unaipeleka mahakamani hukufanya utafiti wa kutosha.. Hukuwa na sababu za msingi, bali kulikuwa na nguvu nyingine nje ya kosa la mshitakiwa
Hii ni maana yako wewe. Siyo ya kisheria kwa mujibu wa Katiba na mamlaka ya DPP. Jitahidi kusoma Katiba
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.

Wafuasi wa Bwana Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa.

Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.

BBC
---
Kikeke: Tanzania unayoingoza sasa hivi ina uhuru wa kujieleza na Demokrasia ya kutosha?

Rais Samia: Ahaaha! Wewe ni mwandishi wa habari toka umefika umesikia vyombo vya habari vimelalamika? Hakuna chombo kimelalamika kuna uhuru wa kutosha wanajieleza, na wanajieleza mpaka wanavuka mipaka saa nyingine. Lakini kwasababu viongozi inabidi mvae ngozi ngumu muangalie.

Lakini wakati mwingine kusema kwao bora umpe nafasi mtu a-offload alichonacho. atoe umsikie kama kiongozi useme kumbe kinalalamikiwa hiki, basi unakifanyia kazi kuliko ukiwabana hawasemi, hujui wanafukuta na nini ndani, ile! Sasa Tanzania kuna uhuru wa kutosha, vyombo vyote vya habari viko huru, anayefuata sheria, anayefuata maadili ya kazi yao wako wanafanya kazi yao.

Hivi tunavyosema uhuru wa kutosha tuna maana gani? Ni nani hasa anaweka kipimo cha kutosha na kutokutosha?
 
Rais Samia akubali au asikubali, atambue kuwa kesi ya mwenyekiti wa chadema Freiman Mbowe watanzania pamoja na ulimwengu mzima wanaiona imechochewa KISIASA.
 
Rais wangu kipenzi kasema vizuri sana hasa hapo kwenye democrasia
 
Hii ni maana yako wewe. Siyo ya kisheria kwa mujibu wa Katiba na mamlaka ya DPP. Jitahidi kusoma Katiba
Yaani unazidi kuonyesha ubovu wa katiba ya sasa...!!! Yaani DPP afute kesi na sababu anayotoa ni kutoona haja ya kuendelea na kesi..!! Hii ni hatari, maana anaweza kutumika kuvuta muda wa jambo fulani lipite..!!
 
Siamini macho yangu na masikio yangu Mama nae??? Tutakimbilia kwa Nani?? Msituni??? Visasi??? Tujifunze ugaidi!??
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.

Wafuasi wa Bwana Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa.

Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.

BBC
---
Kikeke: Tanzania unayoingoza sasa hivi ina uhuru wa kujieleza na Demokrasia ya kutosha?

Rais Samia: Ahaaha! Wewe ni mwandishi wa habari toka umefika umesikia vyombo vya habari vimelalamika? Hakuna chombo kimelalamika kuna uhuru wa kutosha wanajieleza, na wanajieleza mpaka wanavuka mipaka saa nyingine. Lakini kwasababu viongozi inabidi mvae ngozi ngumu muangalie.

Lakini wakati mwingine kusema kwao bora umpe nafasi mtu a-offload alichonacho. atoe umsikie kama kiongozi useme kumbe kinalalamikiwa hiki, basi unakifanyia kazi kuliko ukiwabana hawasemi, hujui wanafukuta na nini ndani, ile! Sasa Tanzania kuna uhuru wa kutosha, vyombo vyote vya habari viko huru, anayefuata sheria, anayefuata maadili ya kazi yao wako wanafanya kazi yao.

Kikeke: Demokrasia ya Kisiasa?

Rais Samia: Demokrasia ya Kisiasa, Yes Ipo. Na hapa naomba nitofautishe baina ya Demokrasia ya Kisiasa na fujo za kisiasa.
Demokrasia ya Kisiasa ni nini? - Demokrasia ya Kisiasa tuna vyama vya Siasa, wana vyombo vyao, wanajadili mambo yao kwa mfano baraza la vyama vya siasa. Huko wanajichagua wao, wanajadili mambo yao ya kisiasa wanaelewana. Kuna kamati ya vyama vyenye wabunge Bungeni na wenyewe wana ya kwao, wakakaa wanazungumza wanajadiliana huko. Lakini kuna vyama vyenyewe vya siasa ambavyo vimeundwa na Katiba zao, na kwenda kwao au kufanya kwao kazi kunategemea katiba zao. Kwa mfano chama changu cha Mapinduzi, Katiba yangu inaniambia labda katika mwaka nitakuwa na vikao viwili vya Halmashauri Kuu ya Chama, Labda Vikao 6 vya Kamati Kuu na vikao vingine katika ngazi za chini Mikoa na Wilaya. Na hivyo vikao vimeelezea wajumbe ni wakina nani na kila kitu. hivyo Vikao vinaendeshwa bila bugudha bila kuomba ruhusa polisi kwasababu Katiba imeshaelezwa na imeshapita kote na najulikana. Na vivyo hivyo vyama vingine vyote vina katiba zao, zina system zao za Mikutano, wajumbe wao ni kina nani, hivyo wako free kufanya wakati wowote.

Kitu ambacho hakipendezi ni ile kutaka uhuru wa kufanya fujo za kisiasa, labda tumemaliza uchaguzi, Serikali imeundwa.. kinachotakiwa kuendelea ni kujenga nchi uwe na chama gani wote mnakuja pamoja mnajenga nchi yenu, ndicho kinachotakiwa kuwa.

Lakini kinapotokea chama, wao wanataka tu kuitisha maandamano kila siku, maandamano yasiyo mwisho, sijui maandamano nini, labda leo mkutano huko, kesho mkutano huko fujo vurugu, aaah ile

Kikeke: Ndio Uhuru wa Demokrasia

Rais Samia: Hapana, kama uhuru wa Demokrasia mbona Marekani hawa-observe, mbona Ulaya hawa-observe? Wakimaliza chaguzi ni kimya, wanaendelea shughuli zao za maendeleo, nchi inapewa nafasi inafanya kazi zake wanajijengea nchi zao. Hatujasikia vurugu za kila siku za huko Marekani na Ulaya, kama kutatokea maandamano ni Constituency ndogo wamekosa umeme jana na juzi umeme umekuja low Voltage wanaandamana mtaa huo wanakwenda kwa huyo mwenye umeme huko, wanasema ya kwao wanarudi peacefully. Sasa haya ya kwetu ya vurugu, piga magari, choma.. ah aha

Kikeke: Nazungumzia suala hilo la kisiasa kwa sababu kiongozi wa upinzania Freeman Mbowe amefikishwa Mahakamani, amefunguliwa mashataka ya Ugaidi, wananchi wake wanasema mashtaka haya yamechochewa kisiasa

Rais Samia: Mimi sidhani kama yamechochewa kisiasa kwasababu navyojua Mbowe alifunguliwa Kesi mwezi wa Tisa mwaka jana (2020), kwa hiyo yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashtaka ni ugaidi na kuhujumu uchumi. Nadhani wenziwe kesi zao zimesikilizwa na wengine wameshapewa sentence zao wanatumikia. Yeye (Mbowe) upelelezi ulikuwa haujeisha, uchunguzi ulikuwa unaendelea so amekwenda amefanya tumeingia kwenye uchaguzi, amemaliza uchaguzi nadhani sasa Polisi wamekamilisha uchunguzi wao, wamemuhitaji waendelee na kazi yao, Lakini kwasababu na kama utakumbuka Mbowe hakuwepo nchini alikuwa Nairobi, sasa kwanini kakimbia sijui. Lakini alivyoingia tu nchini Kaitisha maandamano ya Katiba na madai ya katiba. Nadhani ni Calculation akijua kwamba ana kesi ya aiana hiyo na hii vurugu ambayo ana-instigate akikamatwa aseme mmhh! kwasababu ya Katiba, kwasababu tumeitisha Katiba... nadhani sina hakika.

Lakini kwasababu jambo liko mahakamani, sina uhuru wa kulizungumzia kwa sana. Nadhani tuache Mahakama zioneshe ulimwengu kwamba hizo shutuma walizomshutumu zilikuwa za kweli au siyo za kweli Mahakama itaamua.
She is an extreme headless chicken.

Analishwa maneno anameza bila kutafuna, Tanzania tuna laana gani?
 
Back
Top Bottom