MENGELENI KWETU
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 9,552
- 24,166
Rais wa ovyo kabisa huyu..Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani- Chadema- Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.
Katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Salim Kikeke, Rais Samia amesema ana imani sheria itachukua mkondo wake.
Wafuasi wa Bwana Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa.
Aidha katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha.
BBC
Unambambikia Mbowe kesi halafu anafikishwa Mahakamani ndio anasema wacha sheria ichukue mkondo wake?? Je Mbowe angekamatwa kama sio amri yako wewe??
Ngoja tuzidi kulia na MUNGU aturudishe kati tuanze upya.