Rais Samia, mfute kazi Waziri wa Maliasili na Utalii, mzungu naye akamatwe na kushtakiwa kwa uhujumu uchumi

Duh...!.
Naomba tusubirie taarifa ya MNT, kujua kama crocodiles ni endangered species ambao hawaruhusiwi kuvunwa, maana Tanzania tuna hunting blocks za uwindaji wa kitalii ila muwindaji, anaandamana na game rangers ambao ndio huwa wanaelekeza ni mnyama yupi wa kuwindwa kuepuka kuwinda mnyama mja mzito, au anayenyonyesha.
P
 
Labda aña vibali.....asikilizwe kabla kukurupukaa.....mamba wako wengi sana...ukiomba kibali na kulipia unaua tuu wapungue
Na ndiyo kilichofanyika. Namshangaa huyu mleta mada.!!

Bow and arrow ni kampuni kubwa ya uwindaji ya kimataifa imefuata taratibu zote
 
Mkuu hao wanyama wote wana bei zao,kalipa huyo.
Mamba si chini ya dola 25000.
tembo 40000 zamani hiyo.
Simba 45000Usd zamani hiyo.
Nyati 20000
Swala,ndege,fisi,nyoka,kanga hao ni nyongeza.
So hao wanawinda kihalali kabisa.
na hachukui huyo mnyama ataondoka na ngozi tu na meno.
Mtaachiwa nyama hapo mle kama mnakula mamba.
 
Wapo watu wana vibali vya kuwinda hasa wanyama ambao.hawako hatarini kutoweka na wanyama kama mamba kuna wakatinwanatakiwa kuwindwa ili kupunguzwa

Uelewa.wa baadhi ya watanzania ni mdogo sana .
Yaani hii nchi ni shida sana mtu ana uwezo wa kuingia JF na kufungua Uzi hajui kabisa kuna vibali vya kuwinda hao wanyama na utakuta hajui kabisa kuna vitalu vya mapori vinakodishwa watu wawinde wanyama wanavyotaka.
Mtu huyo utakuta ana akaunt JF,FB,IG,Twitter,Tiktok na Mara nyingi watu hao utakuta hana akaunti hata moja benki.
Watu hawa ndio wanaongoza Kwa kutoa mada za hovyo mitandaoni
 
Mngetusaidia tujue mnazungumzia Hifadhi ipi na tukio limetokea lini
 
Mamba wamezidi mno, ni wengi kweli kiasi ni hatari kwa maisha ya watu huko vijijini, isitoshe mzungu huyu anavibali hakuna tabu yoyote, Mamba wamezidi mno!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…