Rais Samia, mfute kazi Waziri wa Maliasili na Utalii, mzungu naye akamatwe na kushtakiwa kwa uhujumu uchumi

Rais Samia, mfute kazi Waziri wa Maliasili na Utalii, mzungu naye akamatwe na kushtakiwa kwa uhujumu uchumi

Mzungu huyu ameonekana akiwa na maafisa wa wanyama pori akifurahia kumuua mamba mkubwa mwenye urefu zaidi ya mita 4 ndani ya hifadhi moja wapo ya Taifa.

Huu ni uhujumu wa makusudi ambae umefadhiliwa na vyombo vya dola (maafisa wa hifadhi kwani kazi ya kumuwinda mamba mkubwa kama huyo na hatimae kumuua na kuanza kumburuta na kumfunga abebwe sio jambo la siri na clips zimeenea mitandaoni na dunia nzima.

Mzungu husika akamatwe kama ndugu zetu na jamaa wanavuokamatwa hata kwa kukutwa na vipande vya nyama tu ya kitoweo cha familia.

Waziri husika nae aachie ngazi, ikiwa watu wanafikia hadi kufanya ujangiri wa kuhujumu uchumi huku wanalindwa na vyombo vya dola na wakijitajgaza wazi wazi, je vungapi hatuoni ambavyo ni zaidi ya hivi?



===

Raia mmoja wa Kizungu anayejiita Bowmarbow hunting ameonekana mitandaoni akitrend kwa kujisifu kuua Mamba mkubwa zaidi kutoka Tanzania.

Kupitia Instagram yake ameandika kuwa ameingia kwenye rekodi ya kuua Mamba mkubwa zaidi.

Ameandika haya;

“PENDING NEW WORLD RECORD CROC with a bow. This monstrous crocodile measured in at an astounding 16’ 3”! Making him the largest croc in history to ever be harvest with a bow and arrow. The best part is, he’s a 100% wild & 100% free ranging croc in the wilds of Tanzania, which is not how most of the WRs are shot in Africa.

This hunt was beyond incredible to say the least, I can’t wait to share it with you all! The footage we captured was some of our best and this is by far the biggest animal ever shot with a beast_broadheads at 25 yards with an 84lb bow and only a 530 gr arrow it buried through his armor and went all the way up to the fletching.

Just a crazy testament to the lethality of the head.

PSA: As for the Broadheads, next week we’ll be opening them back up for you everyone again A thank you all for your patience with being sold out”

Je, ni sahihi kwa Wanyama kama hawa kuuawa kiholela kwa ajili ya kuweka Rekodi?

Bongo 5
Duh...!.
Naomba tusubirie taarifa ya MNT, kujua kama crocodiles ni endangered species ambao hawaruhusiwi kuvunwa, maana Tanzania tuna hunting blocks za uwindaji wa kitalii ila muwindaji, anaandamana na game rangers ambao ndio huwa wanaelekeza ni mnyama yupi wa kuwindwa kuepuka kuwinda mnyama mja mzito, au anayenyonyesha.
P
 
Labda aña vibali.....asikilizwe kabla kukurupukaa.....mamba wako wengi sana...ukiomba kibali na kulipia unaua tuu wapungue
Na ndiyo kilichofanyika. Namshangaa huyu mleta mada.!!

Bow and arrow ni kampuni kubwa ya uwindaji ya kimataifa imefuata taratibu zote
 
Mkuu hao wanyama wote wana bei zao,kalipa huyo.
Mamba si chini ya dola 25000.
tembo 40000 zamani hiyo.
Simba 45000Usd zamani hiyo.
Nyati 20000
Swala,ndege,fisi,nyoka,kanga hao ni nyongeza.
So hao wanawinda kihalali kabisa.
na hachukui huyo mnyama ataondoka na ngozi tu na meno.
Mtaachiwa nyama hapo mle kama mnakula mamba.
 
Wewe kumbafff jana siulikuwa unachoma mapaja ya mbuzi? Hukuua mbusiiii wewe? Hukudhulumu nafsi ya mbusi wewe mbusiii?

Mkaldayo wewe ni mbusiiiii.
IMG-20231226-WA0020.jpeg
 
Wapo watu wana vibali vya kuwinda hasa wanyama ambao.hawako hatarini kutoweka na wanyama kama mamba kuna wakatinwanatakiwa kuwindwa ili kupunguzwa

Uelewa.wa baadhi ya watanzania ni mdogo sana .
Yaani hii nchi ni shida sana mtu ana uwezo wa kuingia JF na kufungua Uzi hajui kabisa kuna vibali vya kuwinda hao wanyama na utakuta hajui kabisa kuna vitalu vya mapori vinakodishwa watu wawinde wanyama wanavyotaka.
Mtu huyo utakuta ana akaunt JF,FB,IG,Twitter,Tiktok na Mara nyingi watu hao utakuta hana akaunti hata moja benki.
Watu hawa ndio wanaongoza Kwa kutoa mada za hovyo mitandaoni
 
Mzungu huyu ameonekana akiwa na maafisa wa wanyama pori akifurahia kumuua mamba mkubwa mwenye urefu zaidi ya mita 4 ndani ya hifadhi moja wapo ya Taifa.

Trophy hunting ni biashara kubwa tu, na ina taratibu zake. Swali la muhimu kabla ya kuja na hamaki ni "utaratibu ulifuatwa"?
Wapo watu wana vibali vya kuwinda hasa wanyama ambao.hawako hatarini kutoweka na wanyama kama mamba kuna wakatinwanatakiwa kuwindwa ili kupunguzwa
Mngetusaidia tujue mnazungumzia Hifadhi ipi na tukio limetokea lini
 
Mamba wamezidi mno, ni wengi kweli kiasi ni hatari kwa maisha ya watu huko vijijini, isitoshe mzungu huyu anavibali hakuna tabu yoyote, Mamba wamezidi mno!
 
Back
Top Bottom