Rais Samia, mfute kazi Waziri wa Maliasili na Utalii, mzungu naye akamatwe na kushtakiwa kwa uhujumu uchumi


"Je, ni sahihi kwa Wanyama kama hawa kuuawa kiholela kwa ajili ya kuweka Rekodi?
Hajauawa kiholela - Vigezo na masharti vimezingatiwa.
Lakini kama huridhiki kwa mujibu wa kichwa cha Mada milango iko wazi ya kuchukua hatua dhidi ya huyo Mzungu wala hili halimhitaji Rais aingilie kati.
 
Ndio
Lile jina mods walinibadilishia bila ridhaa yangu
Kiukweli mimi binafsi nililipenda lile zaidi. Kuna watu wanajiita shetani na majina mengine ya ajabu kabisa sijui shida ilikuwa wapi kwenye hiyo user name?

Je ulijaribu kuwauliza ni kwanini? Au je walikwambia sababu ya kulibadili?

Maana nafahamu na hata founder wetu Maxence Melo , huwa anahakikisha hata ukifungiwa na sababu ya kufanya hivyo unajulishwa pia nafasi ya kujitetea.
 
... sema mama mjane maskini alambwa miaka 20 jela kwa kukutwa na ndoo yenye vipande vya mzoga wa swala huko Iringa.

Mzungu tajiri milionea apongezwa duniani kote kwa kuua mamba mkubwa zaidi duniani kutoka Tanzania. Umaskini kitu kibaya sana!
Hakika, inasikitisha sana.
 
Unajua madhara ya mamba mkubwa hivyo kuroam freely?

Bora nchi imepata mapato na mamba kauwawa, siku zake zilikua zinahesabika na angeuwawa bure kabisa. BTW hunting is legal in TZ.
Ana madhara gani mkuu, tuache mambo ya kufikilika.
 
Sijaelewa theme ya hii story, kwamba ni ruhusa kuwinda maonesho ya kuvunja rekodi mamba mkubwa au ni kwa ajili ya matumizi ya binadamu...??
Jamhuri imuonee huruma yule Mama Mjane aliyekutwa na vipande vya nyama Poli kwa ajili ya watoto wake.
 
Da
Dah, yule Dada aliefungwa miaka 20 kwa kukutwa na mapande tisa, ya nyama poli, ni bora wange mlipisha tu, kuliko kifungo cha miaka yote ile.
 
Umesahau!

Pia iwaachie wote walofungwa Jela kwa kukutwa na Nyama za Swala, sijui Nyati...

Bila kusahau wale walofungwa kwa kugonga Twiga n.k

Wote waachiwe Huru.
 
Maonesho ya hiyo nyara yanatupa picha gani kwa yule Mama aliyekutwa na tuvipande twa minofu ya nyama poli kwa ajili ya watoto wake.??
Tupe Elimu kidogo Mkuu.
 
Mkuu hao wanyama wote wana bei zao,kalipa huyo.
Mamba si chini ya dola 25000.
tembo 40000 zamani hiyo.
Simba 45000Usd zamani hiyo.
Nyati 20000
Swala,ndege,fisi,nyoka,kanga hao ni nyongeza.
So hao wanawinda kihalali kabisa.
na hachukui huyo mnyama ataondoka na ngozi tu na meno.
Mtaachiwa nyama hapo mle kama mnakula mamba
Da

Dah, yule Dada aliefungwa miaka 20 kwa kukutwa na mapande tisa, ya nyama poli, ni bora wange mlipisha tu, kuliko kifungo cha miaka yote ile.
Huyo hakuwa hata na haja ya kulipishwa chochote.
Hizo nyama inawezekana ni hizo za wanyama hawa hunter wanaacha porini,wanakijiji wanachukua wanapeleka kuuza.
Hunter huwa wanachukua ngozi tu au meno au mapembe.
Ila viswalaswala hivi,kanga sijui mnyama gani mnatafuna tu havina deal.
Sasa fikiria Nyati mzima ni kilo 700-1000 nani atamaliza?
Tembo sio wengi wanauliwa


bei yao kali.
 
Anzia kwa watunza ifadhi kabla ya kumlaumu muuaji.
 
Usikurupuke kuandika vitu usivyovijua, kuna hifadhi za taifa na mbuga za wanyama. Kati ya hizo mbili, moja wapo, watu wanapewa vibali na wanawinda wanyama kwa lengo la ku-balance idadi. Jiongeze wewe boya
Mpuuzi kweli vitu vingine ni Bora kufatilia ukweli kwanza ndo uje kuandika hapa kwenye mitandao, utaratibu uko wazi na umefatwa halafu anatoka boya mmoja anataka waziri ajiuzulu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…