Rais Samia, mfute kazi Waziri wa Maliasili na Utalii, mzungu naye akamatwe na kushtakiwa kwa uhujumu uchumi

Rais Samia, mfute kazi Waziri wa Maliasili na Utalii, mzungu naye akamatwe na kushtakiwa kwa uhujumu uchumi

Muache mihemuko, haya ndiyo mafanikio ya Royal Tour Tanzania.

Mnyama maji mamba wamezidi kuwa wengi hivyo ni vizuri kuvunwa kwa kupitia utalii wa uwindaji.

Kubwa ni kuibeba stori hii kwa mizania inayostahili badala ya kucheza ngoma ya mabeberu au washindani wetu katika utalii makini wa kuwinda kupunguza idadi kubwa ya mamba na kuhakikisha wananchi wanakuwa salama pia kuwepo kizazi endelevu cha mamba ili utalii huu pia uwe wa manufaa kwa nchi na dunia kwa ujumla.

Stori hii ibebwe kwa umakini wa kusapoti Royal tour Tanzania, na habari hii haina uhasi/ negativity kwa utalii bali dunia ieleweshwe na kupewa taarifa sahihi na kupromoti maliasili hii adimu.
We heard a lot about how a good story can have a disappointing ending, but can a bad story have a good written ending?
ShowTime” is down! This two year journey has came to a beautiful end

Explore Our Hunting Regions


BOTSWANA
MOZAMBIQUE
NAMIBIA
SOUTH AFRICA
UGANDA
ZIMBABWE

Africa is home to all the dangerous and big game species​

Big Game Hunting in Africa | Chapungu-Kambako Safaris


Watafutwe waandishi wa habari nguli na watu wa PR Public Relations wajibu hii story kwa lugha zote wa watalii wetu Kiingereza, Kijerumani, Kiarabu, KiHispania n.k ili iishie kuwa ni habari njema kwa utalii wa Tanzania kwa kuwapa elimu walimwengu kuwa mamba wamezidi kupita kiasi Tanzania hivyo kuvunwa kwa kupitia uwindaji ni jambo jema kwa Tanzania na wale watalii wawindaji.
 
Ila mamba wanaua Watanzania maskini wanaohemea maji na dagaa.
Hupigi kelele.
Mwaka 2022/2023 Lindi pekee imepoteza Watanzania wengi kwa kuuliwa na tembo na serikali imeishia kutoa pole ya milioni 1 tu kwa familia zao.
Wauawe tu angalau wapungue kwa usalama wa Watanzania.
 
Mzungu huyu ameonekana akiwa na maafisa wa wanyama pori akifurahia kumuua mamba mkubwa mwenye urefu zaidi ya mita 4 ndani ya hifadhi moja wapo ya Taifa.

Huu ni uhujumu wa makusudi ambae umefadhiliwa na vyombo vya dola (maafisa wa hifadhi kwani kazi ya kumuwinda mamba mkubwa kama huyo na hatimae kumuua na kuanza kumburuta na kumfunga abebwe sio jambo la siri na clips zimeenea mitandaoni na dunia nzima.

Mzungu husika akamatwe kama ndugu zetu na jamaa wanavuokamatwa hata kwa kukutwa na vipande vya nyama tu ya kitoweo cha familia.

Waziri husika nae aachie ngazi, ikiwa watu wanafikia hadi kufanya ujangiri wa kuhujumu uchumi huku wanalindwa na vyombo vya dola na wakijitajgaza wazi wazi, je vungapi hatuoni ambavyo ni zaidi ya hivi?



===

Raia mmoja wa Kizungu anayejiita Bowmarbow hunting ameonekana mitandaoni akitrend kwa kujisifu kuua Mamba mkubwa zaidi kutoka Tanzania.

Kupitia Instagram yake ameandika kuwa ameingia kwenye rekodi ya kuua Mamba mkubwa zaidi.

Ameandika haya;

“PENDING NEW WORLD RECORD CROC with a bow. This monstrous crocodile measured in at an astounding 16’ 3”! Making him the largest croc in history to ever be harvest with a bow and arrow. The best part is, he’s a 100% wild & 100% free ranging croc in the wilds of Tanzania, which is not how most of the WRs are shot in Africa.

This hunt was beyond incredible to say the least, I can’t wait to share it with you all! The footage we captured was some of our best and this is by far the biggest animal ever shot with a beast_broadheads at 25 yards with an 84lb bow and only a 530 gr arrow it buried through his armor and went all the way up to the fletching.

Just a crazy testament to the lethality of the head.

PSA: As for the Broadheads, next week we’ll be opening them back up for you everyone again A thank you all for your patience with being sold out”

Je, ni sahihi kwa Wanyama kama hawa kuuawa kiholela kwa ajili ya kuweka Rekodi?

Bongo 5
Cheki kwanza na mamlaka husika, yawezekana ana vibali halali vya kuwinda.

Kwani wataalamu wa wanyama pori wanasemaje kuhusu eco system?
 
Watakuambia kuwa huo ni uvunaji wa wanyamapori..... Hakuna kesi hapo.
 
Kwa akili yako ya kawaida,kumuua mamba kama huyo kwenye hifadhi ni sawa?!! Unaweza kukadiria imechukua miaka mingapi mpaka akawa na ukubwa huo?!!

Kama angebaki na akajengewa eneo maalumu kwa ajili ya watu kwenda kumuona ingekua ni hasara kwa Taifa ama faida zaidi?!! Baada ya huyo kuuliwa,kuna wengine wenye ukubwa huo?!! Kama wapo,nao hawatauliwa?!! Aliemuua anaenda mfanyia nini?!!!! Hicho anachoenda kukifanyia- Taifa linanufaikaje?!!

Tuache kutetea upuuzi na uharibifu wa Mali asili
Punguza mihemko.mnyama anayetolewa vibali vyakuwindwa ni aliyekomaa,sasa unashangaa nini mamba mkubwa kuwindwa,au ulitaka wawinde mtoto?..Kwasababu sio kwamba yuko huyo peke yake nchi nzoma,wako wengi ila yeye anazungumzia rekodi ya aliyewindwa.Jambo jingine ni kwamba kwenye hifadhi za taifa hakuwindwi.mambo mengine kabla yakuleta mihemko mitandaoni pata muda wakujielimisha kwanza.
 
Kuwinda mamba sio kosa lakini tungejiwekea mipaka kwamba wawindwe mamba wenye ukubwa fulani huyo asingetakiwa kuguswa wala kusogea eneo alipo au makazi yake yote sasa tunasifia royo tua wakati ndugu zetu waongoza watalii wanakiri kwamba hakuna kilichoongezeka tena data zinapikwa mbaya mno labda mafanikio ya royo tua ni kuonyesha mabeberu sehemu gani nzuri waje waimiliki.....
 
leo kuna mtu kakamatwa na 3tons za madawa kigamboni huko.

Goli liko wazi, Nchi imefunguka sasa.
Sasa kaama goli liko wazi ni vipi mtu huyo kakamatwa!? Ukiwa mkosoaji kosoa kwa usawa,hoja yako ingekuwa na nguvu ikiwa mtu huyo wa kilo 3K asingekamatwa
 
Uelewa.wa baadhi ya watanzania ni mdogo sana .
Yaani hii nchi ni shida sana mtu ana uwezo wa kuingia JF na kufungua Uzi hajui kabisa kuna vibali vya kuwinda hao wanyama na utakuta hajui kabisa kuna vitalu vya mapori vinakodishwa watu wawinde wanyama wanavyotaka.
Mtu huyo utakuta ana akaunt JF,FB,IG,Twitter,Tiktok na Mara nyingi watu hao utakuta hana akaunti hata moja benki.
Watu hawa ndio wanaongoza Kwa kutoa mada za hovyo mitandaoni
Ujuaji ni mwingi sana bongo.Tena ujuaji wakijinga.
 
Hili nalo mkalitazame

Angekua mTanzania angebinywa mbupu na praizi mpaka mayai ya mule ndani yapasuke ila kwa sababu ni mdhungu amekuja kuweka rekodi hatujui tumfanye nini
 
Tanzania tuna uwindaji wa kitalii na ndio inayoingiza pesa nyingi kwenye sekta ya utalii.Hapo hakuna kosa lolote liliotendeka kila kinachofanyika hufanyika kwa uwazi na kihalali,ndo maana mmeona game scout wapo.Za kuambiwa changanya na zako,trophy hunting inafanyika nchi nyingi barani Afrika.
 
Back
Top Bottom