Rais Samia: Miaka 30 ya Vyama Vingi - Changamoto na mustakabali kusonga mbele

Rais Samia: Miaka 30 ya Vyama Vingi - Changamoto na mustakabali kusonga mbele

MABADILIKO
Kuna usemi mmoja maarufu, kwamba kitu pekee cha uhakika kwa mwanadamu ni mabadiliko.

Nimedhamiria, kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi. Serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.
Cc Etwege, Idugunde, Corticopontine, muuza kangala, nyankurugu, countrywide, kipara kipya, stroke, USSR, Kt the irreplaceable.
 
Mawazo ni mazuri ila tatizo ni lile kokolo(CCM) na watu waliomzunguka wamejaa uhafidhina,ataweza.Hili hii nchi isonge mbele ni lazima adhibiti ufisadi serikalini na asifumbie macho wakwepa kodi,kauli za kusema waliokuwa wanadaiwa Kodi miaka ya nyuma wasilipe bali walipe mwaka mmoja nyuma,zife.Sheria iwekwe mbele ya ukada na kujuana.
✓Uteuzi uzingatie sifa stahiki na siyo ukada ambao umesababisha watu wenye Brain nzuri kuachwa na mfumo wakizagaa mtaani na kukumbatia vilaza kwenye taasisi za serikali.
✓Kingine aache kuteua wazee maana mbwa mzee awezi kujifunza mbinu mpya.Kama anawahitaji aunde Baraza la Rais la ushauri.
✓Akemee kauli za kibaguzi za kina Nape ambao wanaona CCM na nchi hii mali yao.Kauli za kusema wenye chama tumerudi,mara wana-CCM wengine kuitwa viroboto kwasababu ya kutofautiana mtazamo,hizi kauli za kibaguzi zife.
✓Ahakikishe wanasiasa wote waliofungwa kwa kesi za kisiasa wanaachiwa huru bila masharti.
✓Ahakikishe maoni ya Wananchi yaliyotolewa kwenye Rasmu ya katiba ya Warioba ndiyo yanaheshimiwa na mchakato uanzie kwenye Rasimu ya Warioba na siyo kwenye Rasimu iliyotokana na mgawanyiko wa wanasiasa katika Bunge la Katiba.
✓Bunge la Katiba liundwe upya na lisiwe na sura ya kisiasa kama la awali ambapo liligeuzwa Bunge la Muungano na kuongeza uwakilishi mwingine kwa uchache.Inatakiwa makundi yote ya kiraia yapate uwakilishi na si Kama awali.
✓Watu wote ambao wanahusishwa na tuhuma za ufisadi au wameshawahi kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi,iwe ni marufuku kujihusisha na utumishi wa umma ama kugombea nafasi za uongozi wa nchi.
✓Jeshi la Polisi nalo lifumuliwe na kusukwa upya maana taswira yake si nzuri machoni pa watanzania waliowengi,na Askari wote ambao uadilifu wao unatiliwa mashaka na jamii waondolewe kwenye jeshi.
Tukifanya haya machache na mengine wataongezea wengine,4R itakuwa na maana pana sana.
Kwa hatua hii tu ya kusema ukweli na kuuandika wazi tunampongeza. Ni mwanzo mzuri.
 
Rais SAMIA Atafanikiwa iwapo tu Atawaweka Pembeni WAHAFIDHINA waliopo CCM Kwani Wao Hawataki Mabadiliko na ndio hao Waliokwamisha Mchakacho wa KATIBA MPYA ndani ya BUNGE la KATIBA mwaka Ule
 
Take my words Rais Samia anaweza kuwa Best President Ever wa nchi hii,na angeukuta Uchumi haujaharibiwa angeweka Historia ya pekee Afrika na kuliliwa na kila mtu siku akiondoka hapa Duniani.
Aisee!! Hata mimi nilikuwa nafikiria kama wewe.
 
MIAKA 30 YA VYAMA VINGI: Changamoto na Mustakabali kusonga mbele

Na Samia Suluhu Hassan


LEO Tanzania inatimiza miaka 30 tangu turejee rasmi katika siasa za mfumo wa vyama vingi. Katika kipindi hicho, taifa letu limepitia katika kipindi cha furaha, majonzi, misukusuko na changamoto zote wakati taifa linapoanza njia mpya. Jambo hili si jepesi kwa sababu nyakati hizo hazikuwa rahisi duniani kote.

Miaka ambayo Tanzania ilirejea katika mfumo huo ilikuwa miaka migumu.

Miaka ya mwanzoni ya 1990, ndiyo ilishuhudia changamoto kama vile kuanguka kwa iliyokuwa Urusi, vita za wenyewe kwa wenyewe barani Afrika, mauaji ya kimbari na migogoro mingi ya kisiasa na kiuchumi katika nchi zinazoendelea kama yetu.

Lakini Watanzania walipita katika wakati wote huo wakiwa wamoja na tumeendeleza utamaduni huo miaka 30 baadaye.

Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza wote na ni matumaini yangu makubwa kwamba viongozi watakaokuja miaka 50 hadi 100 baadaye, wataendelea kuongoza nchi iliyo moja na wananchi wasiobaguana na kupigana hata kama wanapingana kuhusu namna ya kuendesha nchi yao.

Ni vizuri kuzungumza kuhusu namna tulivyoingia katika mfumo huu. Rais Ali Hassan Mwinyi aliunda Tume ya Jaji Francis Nyalali iliyokuja na majibu kwamba ni asilimia 20 tu ya

Watanzania ndiyo walitaka mfumo wa vyama vingi. Ni busara ya Mzee Mwinyi na viongozi wenzake wa wakati huo walioamua kusikiliza wachache.

Kama wazee wetu wangesubiri mpaka asilimia 80 itake vyama vingi ndiyo tukubali, pengine leo tusingekuwa tulipo. Hili ni miongoni mwa mafunzo makubwa kwa wanasiasa wa kizazi changu na watakaokuja baadaye.

Kwenye jambo la maslahi ya nchi, maarifa na busara ndiyo muhimu kuliko namba.

Kutoka kuwa na chama kimoja cha siasa – Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa tuna vyama vilivyosajiliwa takribani 20.

Badala ya kusikia sauti moja na wakati mwingine tukisema “Zidumu Fikra za Mwenyekiti”, sasa Watanzania wanasikia kuhusu fikra za sauti tofauti. Kwa bahati nzuri, hata Mwenyekiti Mao alipata kusema “Acha maua 100 yamee kwa pamoja”.
Kipekee kabisa, nitumie nafasi hii kuwapongeza wote waliofanikisha safari hii.

Viongozi wa CCM na Serikali walioona umuhimu wa kuruhusu vyama vingi kabla vita na vurugu havijatulazimisha na wanaharakati na wasomi waliokuwa wakisaidia kutuonyesha kuwa tunatakiwa kuingia katika mfumo wa vyama vingi.

Hata hivyo, yatakuwa makosa makubwa kama tutaona kuwa kazi ile imemalizika. Ninaamini, sasa tunapita katika mazingira yale yale magumu yaliyokuwepo wakati tunaanza mfumo wa vyama vingi.

Kuna vita katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo kwenye nchi zilizoendelea, mfumo wa kidemokrasia wa kiliberali unapitia katika changamoto na nchi kubwa zinapambana kuwania kutawala dunia.

Ni changamoto ambazo viongozi wa kizazi chetu wanatakiwa kuzivuka kama walivyofanya watangulizi wangu.

Ndiyo sababu kwenye uongozi wangu ninaamini katika kile kinachojulikana kama 4R – ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya Kiingereza; Reconcilation (Maridhiano), Resiliency (Ustahamilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding ( Kujenga Upya).

Maridhiano

Katika tamthilia maarufu ya karne ya 19 ya Iolanthe, waandishi Gilbert na Sullivan walieleza jambo moja kuhusu taifa la Marekani wakati huo; ” Kila anayezaliwa ni ama mtoto mhafidhina au mtoto mliberali”. Mimi siamini kwenye misimamo ya namna hii.

Kwamba mwanadamu, awe mwanasiasa, kiongozi au mwananchi wa kawaida, kuwa na msimamo usiobadilika kuhusu mambo yenye maslahi kwa taifa. Msimamo au hali fulani inaweza kueleweka au kukubalika wakati fulani lakini si wakati wote.

Si wakati wakati wote ni wa kupongezana na si wakati wote ni wa kupingana.
Kwenye kujenga Tanzania bora ninatamani kujenga jamii yenye maridhiano na maelewano.

Ninatamani kujenga umoja pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kikabila na nyingine zote. Hili litawezekana kwa kujenga jamii inayopata haki sawa mbele ya sheria, isiyobaguana na inayotoa fursa sawa za kiuchumi kwa wote.

Ninaamini maridhiano hayawezi kupatikana penye ubaguzi na pale ambapo kuna wanaokosa fursa na haki zao za kiuchumi na kiraia.

Ustahimilivu

Kama alivyopata kuasa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ujenzi wa taifa si lelemama. Tanzania hii haiwezi kusonga mbele kama sisi wananchi na viongozi wenu tutakuwa legelege kulinda yaliyo yetu.

Wahenga walisema Umoja ni Nguvu na namna pekee ya kupambana na changamoto zote zinazoikumba dunia kwa sasa ni kwetu sisi kufanya hivyo kwa Umoja na Mshikamano.

Huko tuendako tutatikiswa na kuyumbishwa. Iwe kiuchumi, kimazingira, kijamii na kisiasa lakini ni lazima tujenge ustahamilivu.

Hii ni kwa sababu hakuna nchi nyingine zaidi ya hii na hapa ndiyo kwetu. Nilitiwa nguvu sana na namna Watanzania walivyopokea tukio la Royal Tour kwa uzalendo wa kipekee.

Mabadiliko

Kuna msemo mmoja maarufu kwamba kitu pekee cha uhakika kwa mwanadamu ni mabadiliko.

Nimedhamiria kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi, serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.

Lengo ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na – kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika.

Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza. Kwenye uchumi, mabadiliko yatakuwa na lengo la kutoa fursa zaidi kwa watu wengi zaidi kunufaika kiuchumi badala ya wachache.

Kujenga Upya

Ninafahamu kwamba wananchi hawali maridhiano, ustahamilivu wala mabadiliko. Mwisho wa siku – kama walivyofanya watangulizi wangu wengine kwenye karne hii; Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, lengo kuu linatakiwa kuwa ukuaji wa uchumi wetu. Uchumi utakaoongeza ajira kwa vijana wetu na utakaofungua fursa kwa makundi yote ya kijamii yaliyo nchini.

Tayari tunaendeleza miradi mikubwa ya miundombinu na mengine kwenye sekta ya madini na nishati. Juhudi zilizofanywa kupitia kampeni ya Royal Tour zina lengo la kuzimua sekta muhimu ya utalii iliyoathiriwa sana na ugonjwa wa Covid 19.

Katika kilimo tunakwenda kufanya mabadiliko mengine makubwa ili sekta hiyo muhimu ianze kuwa na mchango inaostahili kwenye uchumi wetu.

Ninaamini kwamba kwa jitihada zetu za R nne, tutaweza kutimiza malengo ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Lengo kuu halikuwa kuwa na vyama vingi vya siasa bali lengo lilikuwa kujenga jamii yenye uzalendo, maridhiano, ustahamilivu na yenye uchumi unaokua kwa wote na endelevu. Hii ndiyo namna bora ya kuendeleza ndoto za wale waliopigania vyama vingi.

#AlipoMamaVijanaTupo
#2022ShirikiUchaguziKwaUadilifu
#2022JiandaeKuhesabiwa
#KaziIendelee.
 

Attachments

  • FWlrAe8XkAEapCA.jpg
    FWlrAe8XkAEapCA.jpg
    95.8 KB · Views: 13
  • FWlrLAUXgAAQfG7.jpg
    FWlrLAUXgAAQfG7.jpg
    17.4 KB · Views: 14
  • FWlrAe_WIAIDkg6.jpg
    FWlrAe_WIAIDkg6.jpg
    16.2 KB · Views: 15
MIAKA 30 YA VYAMA VINGI: Changamoto na Mustakabali kusonga mbele

Na Samia Suluhu Hassan
.

Mabadiliko

Kuna msemo mmoja maarufu kwamba kitu pekee cha uhakika kwa mwanadamu ni mabadiliko.

Nimedhamiria kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi, serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.

Lengo ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na – kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika.

Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza. Kwenye uchumi, mabadiliko yatakuwa na lengo la kutoa fursa zaidi kwa watu wengi zaidi kunufaika kiuchumi badala ya wachache.
Nimeguswa, Jumapili nashuka na Mama kwenye "Kwa Maslahi ya Taifa".
P
 
Take my words Rais Samia anaweza kuwa Best President Ever wa nchi hii,na angeukuta Uchumi haujaharibiwa angeweka Historia ya pekee Afrika na kuliliwa na kila mtu siku akiondoka hapa Duniani.
Seriously....!? Hakuna binadamu aliyewahi kulilipa na kila mtu.

Anyway, so far sijaona tatizo kubwa na huyu Maza........ Binafsi bado namsoma.
 
Tamko la Rais limekaa vizuri Kama TU amelitoa kwa dhati kutoka moyoni.Tatizo litakuwa Ni kwenye utekelezaji Kama ambavyo imekuwa ikifanyika siku zote.Nakumbuka aliyeshauri kwamba maoni ya wachache yasikilizwe wakati wa kuruhusu vyama vingi alikuwa Ni Mwl.Nyerere Ila wakati wa utawala wa Mwinyi.Kama kweli Mama yetu ameamua kulijenga taifa lenye maridhiano,Atuletee Ile Katiba ya wananchi ya Jaji Warioba.Na Sio Ile Katiba iliyochakachuliwa ya marehemu Samweli Sita.Kwa Namna hii Atakuwa Amejijengea heshima kuubwa Sana na atakumbukwa na vizazi vingi vijavyo.Tujifunze kwa wenzetu Kenya kwa Sasa Wapo vizuri Sana.Nampongeza pia Rais Uhuru Kenyata.Anaingoza nchi yake bila ya Mihemko Wala Pressure.Hakuna Rais Kama Kenyata Hapa Africa nzima ambaye angekubali uchaguzi ambao Yeye ameshashinda ati urudiwe.Huyu Kenyata anastahili Nishani ya heshima kwa kitendo Hiki.MAMA YETU NAYE AELEKEE HUKO HUKO,na Mungu Atambariki Sana.
 
Ameandika Rais Samia Suluhu Hassan:

Tanzania inatimiza miaka 30 tangu turejee rasmi katika siasa za mfumo wa vyama vingi katika kipindi hicho, Taifa letu limepitia kipindi cha furaha, majonzi, misukusuko na changamoto zote wakati Taifa linapoanza njia mpya. Jambo hili si jepesi, kwa sababu nyakati hizo hazikuwa rahisi duniani kote.

Miaka ambayo Tanzania ilirejea katika mfumo huo ilikuwa migumu. Miaka ya mwanzoni ya 1990, ndiyo ilishuhudia changamoto kama vile kuanguka kwa iliyokuwa Urusi, vita vya wenyewe kwa wenyewe Afrika, mauaji ya Kimbari na migogoro mingi ya kisiasa na kiuchumi katika nchi zinazoendelea kama yetu

Lakini Watanzania walipita wakati wote huo, wakiwa wamoja na tumeendeleza utamaduni huo miaka 30 baadaye. Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza wote, na ni matumaini yangu makubwa, kwamba viongozi watakaokuja miaka 50 hadi 100 baadaye wataendelea kuongoza nchi iliyo moja na wananchi wasiobaguana na kupigana, hata kama wanapingana kuhusu namna ya kuendesha nchi yao

Ni vizuri kuzungumza kuhusu nana tulivyoingia katika mfumo huu. Rais Ali Hassan Mwinyi aliunde Tume ya Jaji Francis Nyalali iliykuja na majibu kwamba ni azilimia 20 tu ya Watanzania ndio walitaka mfumo wa vyama vingi. Ni busara ya Mzee Mwinyi na viongozi wenzake wa wakati huo walioamua kusikiliza wachache. Kama wazee wetu wangesubiri mpaka asilimia 80 itake vyama vingi ndiyo tukubali pengine leo tusingekuwa tulipo. Hili ni miongoni mwa mafunzo makubwa kwa wanasiasa wa kizazi changu na watakaokuja baadaye.

Kwenye jambo la maslahi ya nchi, maarifa na busara ndiyo muhimu kuliko namba.

Kutoka kuwa na chama kimoja cha siasa – Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa tuna vyama vilivyosajiliwa 20. Badala ya kusikia sauti moja. Badala ya kusikia sauti moja na wakati mwingine tukisema "Zidumu Fikra za Mwenyekiti". Sasa Watanzania wanasikia kuhusu fikra za sauti tofauti. Kwa bahati nzuri, hata Mwenyekiti Mao alipata kusema "acha maua 100 yamee kwa pamoja".

Kipekee kabisa, nitumie nafasi hi kuwapongeza wote waliofanikisha safari hii. Viongozi wa CCM na Serikali walioona umuhimu wa kuruhusu vyama vingi kabla vita na vurugu havijatulazimisha, na wanaharakati na wasomi waliokuwa wakisaidia kutuonesha kuwa tunatakiwa kuingia katika mfumo wa vyama vingi

Hata hivyo, yatakuwa makosa makubwa kama tutaona kuwa kazi ile imemalizika. Naamini, sasa tunapita katika mazingira yale yale magumu yaliyokuwapo wakati tunaanza mfumo wa vyama vingi. Kuna vita katika maeneo mbalimbali duniani, ikiwaqmo kwenye nchi zilizoendelea, mfumo wa kidemokrasia wa kiliberali unapitia katika changamoto na nchikubwa zinapambana kuwania kutawala Dunia. Ni changamoto ambazo

Viongozi wa kizazi chetu wanatakiwa kuzivuka kama walivyofanya watangulizi wangu. Ndiyo sababu kwenye uongozi wangu, naamini katika kile kinachojulikana kama 4R - ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya Kiingereza; Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (Ustahamilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya).

Maridhiano Katika tamthilia maarufu ya karne ya 19 ya Lolanthe, waandishi Gilbert na Sullivan walieleza jambo moja kuhusu Taifa la Marekani wakati huo; "kila anayezaliwa ni ama mtoto mhafidhina au mtoto mliberali", Mimi siamini kwenye misimamo ya namna hii. Kwamba mwanadamu, awe mwanasiasa, kiongozi au mwananchi wa kawaida, kuwa na msimamo usiobadilika kuhusu

Mambo yenye maslahi kwa Taifa. Msimamo au hali Fulani inaweza kueleweka au kukubalika wakati Fulani lakini si wakati wote. Si wakati wakati wote ni wa kupongezana na si wakati wote ni wa kupingana. Kwenye kujenga Tanzania bora natamani kujenga jamii yenye maridhiano na maelewano. Natamani kujenga umoja pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kikabila na nyingine zote.

Hili litawezekana kwa kujenga jamii inayopata haki sawa mbele ya sheria, isiyobaguana na inayotoa fursa sawa za kiuchumi kwa wote. Ninaamini maridhiano hayawezi kupatikana penye ubaguzi na pale, ambapo kuna wanaokosa fursa na haki zao za kiuchumi na kiraia.

USTAHIMILIVU
Kama alivyopata kuasa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ujenzi wa Taifa si lelemama, Tanzania hii haiwezi kusonga mbele kama sisi wananchi na viongozi wenu tutakuwa legelege kulinda yaliyo yetu.

Wahenga walisema Umoja ni Nguvu na namna pekee ya kupambana na changamoto zote zinzoikumba Dunia, kwa sasa ni kwetu sisi kufanya hivyo kwa umoja na Mshikamano.
Huko tuendako tutatikiswa na kuyumbishwa. Iwe kiuchumi, kimazingira, kijamiii, kisiasa, lakini ni lazima tujenge ustahimilivu. Hii ni kwa sababu hakuna nchi nyingine zaidi ya hii na hapa ndiyo kwetu. Nilitiwa nguvu sana namna walivyopokea tukio la Royal Tour kwa uzalendo wa kipekee

MABADILIKO
Kuna usemi mmoja maarufu, kwamba kitu pekee cha uhakika kwa mwanadamu ni mabadiliko.

Nimedhamiria, kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi. Serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.

Lengo, ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo, hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika. Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza. Kwenye uchumi, mabadiliko yatakuwa a lengo la kutoa fursa zaidi kwa watu wengi zaidi kunufaika kiuchumi badala ya wachache. Kujenga upya Ninafahamu, kwamba wananchi hawali maridhiano, ustahamilivu wala mabadiliko. Mwisho wa siku kama walivyofanya watangulizi wangu wengine kwenye karne hii, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, lengo kuu linatakiwa kuwa ukuaji wa uchumi wetu. Uchumi utakaoongeza ajira kwa vijana wetu na utakaofungua fursa kwa makundi yote ya kijamii, yaliyo nchini.

Tayari tunaendeleza miradi mikubwa ya miundombinu na mengine kwenye sekta ya madini

Na nishati. Juhudu zilizofanywa kupitia kampeni ya Royal Tour, zina lengo la kuzimua sekta muhimu ya utalii iliyoathiriwa sana na Uviko-19. Katika kilimo tunakwenda kufanya mabadiliko mengine makubwa ili sekta kubwa ya miundombinu na mengine makubwa ili sekta hiyo muhimu ianze kuwa na mchango inaostahili kwenye uchumi wetu. Ninaamini, kwamba kwa jitihada zetu za R4 tutatimiza malengo ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lengo kuu halikuwa kuwa na vyama vingi vya siasa, bali kujenga jamii yenye uzalendo, maridhiano, ustahamilivu na yenye uchumi unaokua kwa wote na endelevu.

Hii ndiyo namna bora ya kuendeleza ndoto za waliopigania vyama vingi.

Kazi na iendelee
View attachment 2278102
View attachment 2278096
Tunashukuru rahisi wetu mpenda maana kwa kutumia asali umewafanya wapnzan kwa sasa wanaota kama wanafanya mikutano ya sihasa hahahaha kwa sasa mtaani huku full uhuru watu wanaandamana, wanatume huru. Hahahaha nimeamini asali ni dawa rahisi wangu endelea ivoivo tunakushukuru kwa kutupatia katiba mpyaaa maana naona mtaa umetulia baada ya asali katiba is no more
 
Take my words Rais Samia anaweza kuwa Best President Ever wa nchi hii,na angeukuta Uchumi haujaharibiwa angeweka Historia ya pekee Afrika na kuliliwa na kila mtu siku akiondoka hapa Duniani.
KWA mtazamo wako lakin
 
Ametoa mawazo mazuri sana ambayo sasa yanahitaji utekelezaji usiokuwa na siri kubwa. Jamii ya Kitanzania sasa imechoshwa na usiri uliopo kwenye mambo yanayohusu uongozi wa nchi pamoja na mikataba mikubwa ya miundombinu nk. inayohusu Taifa.
Katiba mpya ifanyiwe kazi na watu ambao hawana tamaa ya kuteuliwa, wawe neutral na Tume iwe neutral kabisa. Na ihakikishwe kuwa mambo kadhaa yanazingatiwa kwa umakini kabisa. Moja wapo ni haya matatu: 1. Katiba ihakikishe kuwa inaangalia vizuri maswala ya uteuzi wa viongozi ili tuweze kupata viongozi wenye uwezo na uzalendo wa kuliendesha Taifa. Public Vetting izingatiwe! Isipokuwa kwenye nafasi sensitive kama Mkuu wa Majeshi nk. 2. Katiba iangalie na kupendekeza vyema idadi ya Vyama vya siasa isiwe kubwa kama ilivyo sasa, ni vyanini vyama 20? Ni kuchezea fedha na muda wetu bure. Yaani kutokee kuna mikutano 20 mkoa mmoja kwa wakati mmoja? Upuuzi mtupu. Tukubaliane vyama vya siasa viwe vitatu tu basi! Aliye na mawazo mazuri atajua ajiunge na kipi. Lakini tusijiaminishe kuwa na utitiri wa vyama ndiyo kutatufanya tuwe na demokrasia nzuri! 3. Viongozi wa Tume ya uchaguzi wasiteuliwe na Raisi. Ufanyike utafiti wa kuwapata hawa na wasiwe karibu na ikulu wala wasijihusishe na siasa za vyama. 4... tuendelee kuchangia..
 
Ni maono mazuri ambayo yanahitaji kuungwa mkono. Rais huyu anaweza kuwa rais wa kihistoria ambaye atakumbukwa kama Mama wa Taifa!
Umewaza kama nilivyowaza juzi juzi hapo mkuu.
 
Makala yenye maono?
Nchi hii ina majuha mengi
Ni kweli ina majuha mengi ila ina wehu na mashoga na mamento kama unavyojiita ukimaliza kublid soma tena hiyo makala kama haina maono endelea kukata mauno bumbafu baba yako heri angepiga punyeto kuepusha Taifa kuwa na vijana wa namna yako shenz type
 
madam President anastahili pongezi kwa makala yake yenye maono haya mambo ya kuandika alifanya Mzee Nyerere na Mkapa viongozi wengi wenye maono huandika....Fidel Castro...Nkurumah...Mandela...Samora na wengine wa calibre hiyo...waliandika sana
Utekelezaji ndiyo shida zaidi ya maneno matamu kwa wafadhili
 
Back
Top Bottom