Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,718
- 3,465
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Jana tarehe 01.07.2022 aliandika makala Kwenye gazeti la mwananchi yenye kichwa Cha habari miaka 30 tangu turejee katika mfumo wa vyama vingi.
Katika makala hiyo mhe Rais ameandika mambo mengi yenye masrahi mapana na ustawi wa nchi yetu kwa ujumla.Binafisi ninafurahishwa sana na dhamira njema ya Rais wetu mpendwa hasa alipotaja 4R.Lakini hofu yangu kwa dhamira njema ya Rais wetu mpendwa ni maadui wa hizi 4R ndani ya chama Chama chake Cha CCM.
Ndani ya chama chake mheshimiwa Rais Kuna wahafidhina wasiotaka , Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (uvumilivu),Reforms (Mabadiliko) na Wala Rebuilding(kujenga upya).
Hawa wahafidhina wataweza kumkwamisha mhe Rais kuweka legacy ambayo itaandikwa kwa wino wa dhahabu katika nchi yetu na hautafutika kamwe vizazi na vizazi.Baada ya kusema haya mwenyezi Mungu akutie nguvu mhe Rais ili uweze kuvuka salama vizingiti vilivyo mbele yako.Kazi iendelee.
We should be smart enough not to fall for this political chicanery!