#COVID19 Rais Samia: Miji mikubwa ya Tanzania tayari imekumbwa na wimbi la tatu la Covid-19

#COVID19 Rais Samia: Miji mikubwa ya Tanzania tayari imekumbwa na wimbi la tatu la Covid-19


mnafiki sana wewe mbowe sijui unamdanganya nani ? sasa watu wajihadhari na corona wakati unaendesha mamikutano yakoyasiyo na umuhimu wowote eti umekatisha ziara visiwani wewe ndiyo unaeneza corona kwa watu inabidi wakuepuke kama ukoma mbuzi wa kafara weeee
 
Kwani anayetakiwa kuahirisha mbio za mwenge ni nani? Anayeweza kuongoza hatua zaidi kupambana na ugonjwa ni nani ? Hizo kelele za kovidi sio kwa ajili ya wananchi, ni kwa ajili ya wenye hela watupe mikopo.

Anaongelea wimbi la tatu lakini la pili liliwahi kutangazaa lini rasmi na serikali ? Inawezekana tupo hata wimbi la nne, na litapita kama yalivyopita mengine, bila hatua zozote madhubuti za kukabiliana nalo, watakaobaki poa, watakaoenda poa.

Mikopo na misaada ya Corona? Acheni utani mazee:

IMG_20210706_203616_157.jpg
 
his third wave is already in the country and there is nothing to hide. We have patients in Kagera, Arusha, Mwanza, Dar es Salaam and even Dodoma,” she said.
hata Kilimanjaro hali sio nzuri hata kdg.
 
Sasa kwa nini Rais Samia anakusanya watu kwenye hizo ziara zake na kuwahutubia?

Ndo maana nasema hayuko serious kabisa.

Anafuata mkumbo tu!

Hii ni jana/ juzi alipokuwa Morogoro.

Hapa na Mimi anajichanganya sana, anasema tuchukue tahadhari tuepuke mikusanyiko alafu anatuita tena tukusanyike
 
Kajazana na watu kwenye mpira wa Simba na Yanga, watu wamejazana Sabasaba.

Does she even know what she is talking about?
Huyu mama anajichanganya sana, ni Bora hili suala la corona angeachana nalo
 
K

Jamani, Kenya na Uganda wanaokufa ni wazungu???, naomba tusikejeli haya mambo, na cha msingi tu kila mtu achukue tahadhari....
Kenya na Uganda wanakufa kwa njaa. Wameyumbishwa kiuchumi kiasi kwamba hawapati menu vizuri kwahiyo kinga za wananchi walio wengi zimeshuka.

Korona kama korona haijauwa watu ktk mataifa hayo. Uganda pia kuna bongo movie ya kuxika masanduku tupu ili wazungu wamwage hela zaidi.

Yaani kama ugonjwa wa korona kweli ungekuwa unauwa hapo nchi za majirani kwanini Tanzania haipo? Kwamba sisi tuna akili Sana ama sisi tunamjua Mungu Sana kuliko wenzetu? Afrika korona haitupendi
 
Rais Samia akiwa katika ziara yake mkoa wa Morogoro maeneo ya Kibaigwa amewataka wananchi wote kuchukua tahadhari juu janga la Covid-19.

Katika kufafanua jambo hili Rais Samia amesisitiza kuwa wimbi la tatu la ugonjwa huu limeshaanza kutikisa katika miji mikubwa ya taifa la Tanzania.

Aidha, Rais Samia amesema "Wimbi la tatu la Covid-19 tayari lipo nchini na hatua cha kuficha, tuna wagonjwa mkoa wa Kagera, Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Dodoma.

“Chukueni tahadhari hili wimbi la tatu ambalo linapukutisha wenzetu lisije kupukutisha hapa kwetu, gonjwa hili likianza kutuangusha halina kusimama linapukutisha tu”

===

Zaidi soma
Tanzania’s major cities are worst hit by a third wave of the Covid-19 pandemic, President Samia Suluhu said, while urging citizens to take precautions to protect themselves.

Speaking at Kibaigwa, Morogoro in central Tanzania, on her way from the capital Dodoma on Wednesday, President Suluhu expressed her shock when she saw hundreds of people without masks.

“This third wave is already in the country and there is nothing to hide. We have patients in Kagera, Arusha, Mwanza, Dar es Salaam and even Dodoma,” she said.

“I have seen here that just a few people are wearing masks and doing so incorrectly with only their mouths covered leaving open their noses. Therefore, I call upon everybody to take precautionary measures against Covid-19 as directed by health experts,” she said.

The President said in Dodoma, while the number of patients is small, the cases should sound a warning to citizens to be more alert in order to prevent deaths as reported in other countries.

Ms Sululu urged wearing masks whenever in public gatherings.

Source: The Citizen
Kwanini tangu achukue madaraka na kuamua kuchukua tahadhari ya UVIKO kwa kiwango kikubwa ndio maambukizi yameongezeka ziaidi?

Wametegemea sayansi bila Mungu ni ubatili mtupu na huenda linaenda kupiga hodi tena sebuleni.

Kuna mahala viongozi wamepungukiwa maarifa sio hizo tahadhari na kinga zilizopo ambazo tayari wengi wao wamepata lakini 'delta variant' anawaibukia ndani ya AC.

Watanzania mrejeeni mwenye Mungu ndio kimbilio la pekee kuepusha madhara zaidi.
 
Kama unaishi nje ya Tanzania unaugua. Lkn kama upo ndani ya ardhi ya mwalimu Nyerere nakuhakikishia hakuna korona.
BTW, ugonjwa huu hauwaui Sana watu weusi, ndiyo maana Afrika siyo issue sana.

Hata SA wanaokufa ni wazungu siyo wazulu wa Kwazulu Natal

Hivi mnaona mataifa mengine wanavyokufa jamani?
Kaka hujaelewa bado? Virusi vinaua kwanza wazee, pili watu wengine wenye udhaifu kutokana na magonjwa au menginevyo.
Kote Afrika hadi sasa vifo vimekuwa vichache kwa sababu
1) wazee ni wachache, vijana ni wengi
2) watu wengi bado wako vijijini, hivyo hawasafiri sana, hawakutani na watu wengi sana, virusi huwa na nafasi ndogi kusambaa
3. watu wengi, hata Dar es Salaam, wanaishi hewani wazi, yaani hawana makazi ambako madirisha ya kioo yamefungwa (kule Ulaya hata masoko mara nyingi yamo ndani ya ukumbi)

Haidhuru kama ni Mzungu au Mwafrika. Umri, kiasi cha kuwa karibu na watu wengi na muda wa kukaa ndani ya vyumba vilivyofungwa ni sababu ya kuwa na maabukizi mengi au machache.
Kwa hiyo kwa chi kama Tanzania ni rahisi zaidi kuepukana na wimbi kubwa kama Ulaya. Ila tu wale wanaojitahidi wataambukizwa, wakiwa vijana labda bila dalili, lakini hata hao vijana wanaweza kuambukiza wengine, na hapo unaona hasa wazee na wenye magonjwa mbalimbali wanaathirika vibaya hadi kufa.
Na asilimia ndogo ya vijana wanaathirika pia;
ila tu, ukijua hisabati: Asilimia ndogo ya watu wengi = idadi kubwa kiasi.
 
Back
Top Bottom