Nyuki Mdogo
JF-Expert Member
- Oct 31, 2021
- 4,134
- 10,644
Kusingekuwepo na sherehe za Uhuru tusingejenga hayo mabweni?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Amesema mabweni sio madarasKwani madarasa hayakuisha kwenye ile hela ya covid?
Hela zote hizi mlitaka kuua watu?Milioni 960 tungeigawanya kwa kila mmoya tupunguze ukali wa jua
Safi sana.
Upigaji in the building
Unauhakika kuwa zilifika zote?Mheshimiwa Rais Dr. Samia S.Hassan zile milioni 500 ulizotoa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje (OPD) Hospitali ya wilaya ya Nyamagana zimepigwa zote, jengo halijaisha watumishi wapo wanarushiana mpira! Mh. Rais pengine una nia nzuri ila tunajua huku chini wanasubiria huo mgao wa madaraja wazitafune kama mchwa!
Hizi sherehe kutengewa hela hizo na kuna matatizo kibao ni ujinga,kuiga jambo zuri siyo ujingaSio kila kitu ni Cha kuiga kwamba Hakuna haja ya sherehe si ndio?
Nilivyoona hiyo 500 nikadhani zile milioni 500 kila kijiji.Mheshimiwa Rais Dr. Samia S.Hassan zile milioni 500 ulizotoa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje (OPD) Hospitali ya wilaya ya Nyamagana zimepigwa zote, jengo halijaisha watumishi wapo wanarushiana mpira! Mh. Rais pengine una nia nzuri ila tunajua huku chini wanasubiria huo mgao wa madaraja wazitafune kama mchwa!
Uhuru gani huo unaouzungumzia kama bado kuna watu wanasafiri kilometers kadhaa kufuata huduma za afya? Maji tatizo,Umeme shida,Barabara kikwazo.....ungejua maana ya neno Uhuru kwanzaUhuru wa taifa letu ndiyo msingi wa taifa husika. Kama tunaweza kufanya sherehe za kuzindua matundu ya vyoo, miradi ya maji nk kwa gharama kubwa tunashindwaje kuona umuhimu wa sherehe ya kumbukumbu ya siku ya uhuru ambayo inabeba alama na historia ya taifa letu?. Kwa viongozi mliopo madarakani kunahaja ya kuweka vipaumbele vya taifa hili vizuri kwani vinginevyo taifa litaangamia.
Labda kama kuna nadharia nyingine kwamba uhuru waliopigania wakati huo umeshaporwa hivyo hakuna haja ya kufanya sherehe hizi kwa maana kwamba walichopigania kutoka kwa utawala wa mkoloni hakipo tena.
Mimi sioni tatizo kuadhimisha miaka ya uhuru wa Tanganyika kwa kufanya kazi za ujenzi wa taifa.Sio kila kitu ni Cha kuiga kwamba Hakuna haja ya sherehe si ndio?
Kila mmoja angepata mil 1.5Milioni 960 tungeigawanya kwa kila mmoya tupunguze ukali wa jua
Ingetufaa sanaKila mmoja angepata mil 1.5
Umetumia kanuni ipi mkuu kukokotoa?Kila mmoja angepata mil 1.5
Mil 960 gawa kwa mil 61 ambayo ndiyo idadi ya watanzania kwa mujibuwa sensaUmetumia kanuni ipi mkuu kukokotoa?
Kwahiyo Sherehe za Uhuru mwaka huu zingefanyika March 2023!? Na mbona Simbachawene anasema wameshazituma maeneo husika...au katuma makaratasi tuu.Milioni 960 ziko kwenye karatasi ( Bajeti) kama figure .
Hadi zitumwe eneo husika ni March 2023.
Zile mlizowapa simbion si zingetosha kabisaView attachment 2436580
NB: Ya Magufuli ni yake Samia.
====
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza TZS milioni 960 ambazo zilitengwa katika bajeti kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za Uhuru inayoadhimishwa kila Desemba 9, zipelekwe Ofisi ya Rais TAMISEMI na zitumike kujenga mabweni katika shule nane za msingi zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 5, 2022 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, George Simbachawene amezitaja shule hizo kuwa ni Buhangija (Shinyanga), Goeko (Tabora), Darajani (Singida), Mtanga (Lindi), Songambele (Manyara), Msanzi (Rukwa), Idofi (Njombe), na Longido (Arusha).
Amesema shule hizo zimekwisha ratibiwa na TAMISEMI na tayari zimekwisha gawiwa fedha hizo kwa ajili ya kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
“Ikiwa ni dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwajali na kuwajengea mazingira rafiki watu wenye mahitaji maalum hapa nchini, hili ni jambo kubwa na la kishujaa na la kupongezwa sana,” amesema.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika midahalo na makongamano katika wilaya zote na kujadili kwa kina kuhusu maendeleo endelevu katika siku ya maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania.
View attachment 2436676