Rais Samia: Milioni 960 za sherehe ya Uhuru zikajenge mabweni shule nane za wanafunzi wenye mahitaji maalum

.
Imagine tangu tupate uhuru pesa ngapi imeenda kwenye sherehe za uhuru?
.
Imagine ni mambo mangapi ya maendeleo yangefanyika kwa fedha hizo?
 

Amefanya vizuri sana. Tupungeze pia safari, sherehe, makongamano, semina ambazo sio muhimu.

Tulete maji Safi na salama kwa kila Mtanzania.
 
Hii siku ni muhimu sana kwa Taifa letu. Wangeachana na vitu kama mwenge na vingine ningeelewa!
 
Rais Samia Suluhu amefanya maamuzi sahihi katika hili kujenga mabweni kwaajili ya wanafunzi wenye uhitaji hii sio tu kwamba ni sherehe bali hii ni sadaka haijawai tokea toka Tanzania ipate uhuru
 
Big up Mh. Rais haya maamuzi yanachochea maendeleo kwa kiasi kikubwa, hayamalizi matatizo yote ila yanapunguza. Hongera sana mama.
 
Pesa za sherehe ya Uhuru ni pesa ndogo sana ukilinganisha na zile zinao pigwa Billions of shillings zinapigwa Daily na wala kwa urefu wa kamba, na huko hutamsikia huyu mama anaongelea wala kukemea labda wanao piga ni wanajuana. Sasa anaona njia pekeee ya kutengeneza attention ni kusema hakuna sherehe za uhuru. na tulivyo wajinga tusha ingia king kuona mama kweli mzalendo kumbe hakuna kitu.

Sasa kuja na swagwa za kuzuia pesa za uhuru eti zikajenge sijui mabweni ni usaniii mtupu na wakutafuta sifa mbele ya wajinga walio jaaa nchi hii na walamba asali.

Kama swala ni kupunguza matumizi basi isi ishie kwenye sherehe za uhuru bali iwe ni kote huko hasa kwenye Magari yao yale, Mama mwenyewe msafara wake unaweza kuwa ni zaidi ya pesa za sherehe za uhuru, lakini huko hazungumziii.

Watawala walisha soma raia wakajua ni wapenda mambo ya zima moto that is whay wanakuwa wanachomekea vitu vidogo vidogo kutengeneza attention.
 
Zinapigwa wapi mbona mnakazana kupigwa kwa pesa wakati hamtowi wapi ufafanuzi, mtaangaika mpaka mtakapo choka, hizi propaganda hazitasaidia
 
Zinapigwa wapi mbona mnakazana kupigwa kwa pesa wakati hamtowi wapi ufafanuzi, mtaangaika mpaka mtakapo choka, hizi propaganda hazitasaidia
Unasomaga Report za CAG? au unasoma magazeti ya uhuru muda wote? Tafuta report za mkaguzi usome uone upigaji
 
Zinapigwa wapi mbona mnakazana kupigwa kwa pesa wakati hamtowi wapi ufafanuzi, mtaangaika mpaka mtakapo choka, hizi propaganda hazitasaidia
So report za CAG huwa ni propaganda? Mnakuwa wajinga kiwango hiki?
 
Samia hawezi fanya hayo labda nchi ifirisike kabisa.Wao walivyomwona Magufuli anafanya hayo aliitwa mshamba na limbukeni,Samia na kundi lake niwatu wa bata Sio kujenga nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…