Rais Samia: Mimi ni Mzanzibari

Huyu bibi ni mbaguzi balaa
Wewe jamaa una nongwa sana.....

Kwako hakujawahi kutokea kiongozi wa CCM akawa mwema....

Endelea kuufukuza upepo...labda iko siku CDM mtaipata dola kwa staili hiyo ya kupinga ,kuzusha na chuki.... 🤣🤣
 
Mtu aliyezaliwa Zanzibar mwaka 1960 ni Mzanzibari. Tanzania haikuwepo huo mwaka 1960.
Kama hivyo ndivyo basi Nyerere aliyezaliwa 1922 enzi za ukoloni asingejiita Mtanzania na kudumu katika hilo hadi kifo chake!!! Mtu aongee ni Mzanzibari akiwa ndani ya eneo la Zanzibar pekee sio nje ya hapo. La sivyo watu wa jamii zingine wanapotoka kwenda mataifa mengine wasijitambulishe wao wanatokea Tanzania bali kwa mfano Mbena wa Njombe, Mruri wa Mara, Mmanyema wa Kigoma, Mkaguru wa Gairo nk

Inawezekana hata huko UNGA utambulisho ulikuwa ............
 
Amesema hana kabla. Kwa hiyo alitakiwa kusema kuwa yeye ni Mtanzania..... Period. Kujiconnect nakule aliko toka ni sawa na kusema mimi ni kabila fulani.

JF humu kuna watu wengi tu ambao hawajui lugha nyingine yeyote nchini zaidi ya kiswahili. Ila pale watakapotumia makabila ya wazazi wao kujitambulidha tayari wanakuwa wamechanja upande.
 
Tunataka Rais mtanzania siyo mtanganyika wala mzanzibari. Tunataka Rais asiyebagua nchi kikanda, Tunataka Rais anaejivunia Utanzania wake siyo utanganyika wala UZANZIBARI wake.
Kama JPM vile alivyokuwa hana ubaguzi kikanda
 
Inamaana hujui kua hao Wazanzibari asili yao si bara, ambako watumwa walikua wanachukuliwa na kusafirishwa kupitia Soko la watumwa huko Zanzibar kwenda ughaibuni!?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Tukianza hivyo .wabara wenyewe watabaki wachache.kiasili watanzania wengi ni wahamiaji.
 
Wewe jamaa una nongwa sana.....

Kwako hakujawahi kutokea kiongozi wa CCM akawa mwema....

Endelea kuufukuza upepo...labda iko siku CDM mtaipata dola kwa staili hiyo ya kupinga ,kuzusha na chuki.... [emoji1787][emoji1787]
Kuna kiongozi gani mwema kutoka CCM? Mtaje hata mmoja
 
Mi sijaona kosa lake kwa kauli hiyo. Infact, alikuwa anawapiga dongo watanganyika. Tanzania ni Muungano wa nchi mbili. Tanganyika na Zanzibar. Bara ndio kuna huo ujinga wa Kabila ila kule ZANZIBAR haupo. Hivyo anawaambia nanyi achaneni na ujinga wa makabila. Yeye amesema wazi kwamba KABILA lake ni Mzanzibari. Hajasema utaifa wake. Kwanini kuna watu mna nongwa kwa kila jambo. Mna lengo gani kwani?
 
Alitakiwa aseme mimi ni MTANZANIA! Lakini kinywa cha mtu husema yaliyojaa moyoni!! Uzanzibari umejitokeza kuwa umejaa moyoni kuliko Utanzania!! Very unfortunate!! Imeshatoka hiyo live!!

Mkuu umeandika sahihi kabisa kabisa.

Rais kama alitaka kukosoa ukabila, angejinasibisha na u Tanzania na si uzanzibari.

Alikosea, aliharibu badala ya kutengeneza.

Watu wanarefer Magufuli kuwa aliongea kisukuma, hata yeye tulimkosoa hapa kama tunavyomkosoa Samia. Kosa la aliyepita halijustify kosa la aliyepo.
 
Tunataka Rais mtanzania siyo mtanganyika wala mzanzibari. Tunataka Rais asiyebagua nchi kikanda, Tunataka Rais anaejivunia Utanzania wake siyo utanganyika wala UZANZIBARI wake.
Sahihi kabisa and well stated
 
Wafuasi wa mwendazake ndio wanalialia mara tunaonewa, mara, tunatumbuliwa,....
 
Ulitaka aseme ni ngosha au mangi wa kibosho
Sijui kama umeelewa hoja hapa
Yeye ni Mzanzibari kwa kuwa Zanzibar hakuna makabila kama yangekuwepo angejitaja kwa kabila lake
Kwetu Bara makabila yapo kwanini nisiseme mi mchaga au msukuma?

Angekuwa mfano kwa kusema mimi ni mtanzania na siyo kujitaja kwa eneo analotoka tungemuelewa

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mimi binafsi sioni tatizo. Inaonekana wewe ndio wale wale wa lile kundi. Mnatumia kila kisingizio ili kumuharibia sifa rais wetu.
 
Dah Hilo jina Mkuu ni la kipekee kweli kweli [emoji38]
 
Tusikuze mambo hapa hana tofauti na Magu kusema yeye ni msukuma. Zanzibar hawana makabila ni wahamiaji hivyo wanatumia neno mzanzibari sio kitaifa lakini kijamii kama wachagga, wapare, wasambaa, wahehe, wasukuma. Magu alikuwa akisema yeye ni msukuma hakuna aliyesema chochote sasa Samia ni kabila gani? Wote kule wanatumia neno mzanzibari kwa maana ya jamii na sio utaifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…