Rais Samia: Mimi ni Mzanzibari

Rais Samia: Mimi ni Mzanzibari

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"

Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.

Samia umekosea sana!

====


Samia Suluhu ninapotoka hatuna makabila. Kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo...

Kwenye system ya makuzi – shule na siasa – tunamshukuru sana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kwahiyo, tunapofanya kazi hapa, na mimi binafsi, ninafanya kazi bila kuangalia kabila fulani.

Sasa watu wakifanya makosa, “nimewajibishwa kwakuwa ni kabila Fulani”. Sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia ni Mzanzibari.

Sasa kosa lake nini apo? Kwani yeye co mzanzibar na wewe co msukuma!!!!


Mungu ampe afiya njema mama samia suluhu hassan, mzanzibari mwenye hekima na busara.


Haya nawasubili wazee wa RIP MAGU, TUTAKUKUMBUKA BABA PUMZIKA KWA AMANI. mutaongea sana lakini uyu ndiye rais we2 bandugu.
 
Naona mama ana jaribu kuwajibu sana watu wa mitandao, mi nadhani ange wapotezea hawafiki hata 10% ya watanzania
Hata wangekuwa 1%, wingi si hoja. Kinacho angaliwa ni mantiki ya hoja zao.
 
Safi sana yupo sahihi...

Hata mimi ukiniuliza kabila nitakuambia mimi ni mTanzania...
 
Lakin ukweli utabaki kuwa ukwel tu yeye ni Mzanzibar hlo tunajua na halpngik na litabk kuwa hvyo. japo kama Rais hakutakiwa kusema hvyo[emoji120]
Mimi ni Mtanganyika na si Mmakunduchi, Mtumbatu, Mngazija, Mshirazi n,k.
 
Jamaa zangu wale wa team JPM hawaaminiki kama alishakufa na imeshatoka. Wamejawa na vinyongo visivyo na sababu. Wanamshikia bango mama kwa kusema yeye ni mzanzibari.

Wanashindwa kuelewa kwamba ni katika kujenga hoja kwamba anapomtumbua mtu haangalii suala la yeye kwao ni wapi.
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"

Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.

Samia umekosea sana!

====


Samia Suluhu ninapotoka hatuna makabila. Kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo...

Kwenye system ya makuzi – shule na siasa – tunamshukuru sana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kwahiyo, tunapofanya kazi hapa, na mimi binafsi, ninafanya kazi bila kuangalia kabila fulani.

Sasa watu wakifanya makosa, “nimewajibishwa kwakuwa ni kabila Fulani”. Sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia ni Mzanzibari.
Kujuana kwa maeneo ndio regionalism yenyewe kujuana kwa makabila ndio tribalism yenyewe , so hakuna tofauti kati anayejitapa kwa kabila na yule anayejitapa kwa kanda.....

Viongozi wa Afrika bhana
 
Watanzania tuna Mambo mengi tena Muhimu tu ya Kufanya na siyo huu Upopoma ( Upuuzi ) wako uliouleta hapa.

Sijaona tatizo kwa Rais kutamka hivyo.
Sijawahi ona uwezo wako wa kuona. Rais ndie alfa na omega, lolote alitamkalo linatatafsiriwa kwa mapana.
 
Hana kabila, lakini ni mdini mzuri.

Hamkupenda Muisilamu aongoze co!!!! Since aingie uyu mama maneno meengi, mara baadhi wam2kane, wamukashifu. Wakati wa magu waisilamu hawakuwa wakimtukana wala kumkashifu. Muheshimuni uyu mama bandugu.
 
K
Angejitambulisha kwamba yeye ni Mkojani au Mnungwi isingekuwa na tatizo lolote. Ni sawa na ilivyokuwa haina tatizo kwa JPM alivyokuwa akijitambulisha kwamba alikuwa Msukuma. Pamoja na kwamba tulikuwa tunafahamu kwamba JPM alikuwa Mtanganyika, lakini ingeleta kero sana kama kwa siku yoyote angejitambulisha kwamba alikuwa Mtanganyika. Hata Samia kwa kujitambulisha kwamba yeye ni Mzanzibar kakosea na nadhani haina afya kwa taifa. Kujitambulisha kwa kutumia utaifa wetu wa zamani ambao kimsingi ulishakufa siyo vyema sana.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mh Rais hayo uliyotaja si makabila yeye pia aliyataja baadhi na akasisitiza 'Zanzibar haina makabila.'
 
Vp kwani ugali umepanda bei? Baada y kusema ivyo?
 
Yuko sahihi 100%, Mike ni MTANGA, sio MSAMBAA, MDIGO,MBONDEI wala MZIGUA, bali MTANGA. sasa hapo ukabila uko wapi?

Tuache unafiki Mama yuko sahihi
 
Zanzibar hakuna makabila eti?
Makbila ni mengine tena yakiwa na asili ya bara hasa unakuta Waha, Wamakonde, Wangoni, Wadigo, Wamanyema, Wasukuma, Wanyamwezi, na masalia ya mwambao wa Pwani na visiwa vya Komoro kwa hiyo kila mtu ana kabila la asili na dini aliyokuzwa nayo kama hakubadili mwenyewe.

Maneno yakuitana Mtanganyika na Mzanzibari yanatakiwa yafe na badala yake yeyote anayetoka upande wowote aitwe Mtanzania kwa kutofautishwa tu na ama bara au visiwani basi maana ndicho kiini cha mtengamano kuja kubomolewa hapo.
 
....basi walikuwa na sababu zao muhimu, labda. Unasema mimi ni muafrika kutoka Tanzania. Ukiwa Kenya unasema mimi ni mkenya kutoka Kericho. Hutakiwi kusema mimi ni mkabarneti kwa sababu utaamsha hisia za kikabarneti na kimakonde!!!
 
Back
Top Bottom