Rais Samia: Mimi ni Mzanzibari

Rais Samia: Mimi ni Mzanzibari

Keshajitenga yeye ni Mzanzibar wadanganyika mtajiju ila kakosea kutamka vile haya mwalimu aliyakataa bora angesema ye mtanzania angeeleweka
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"

Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.

Samia umekosea sana!
Sasa ulitaka aseme nini? Kwani kaongopa
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"

Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.

Samia umekosea sana!
Alijaribu kujenga hoja kwamba anapotumbua mtu haangalii kabila. Wanataka kumbananisha na uzanzibari wakati hajajikita huko.

Wakubaliane tu na maamuzi ya kiongozi mkuu wa nchi.
 
Tumeona mama akiwaondoa wazalendo wenye Phd na kuweka watu wenye kutiliwa mashaka na umma kama wajuzi wa kupiga hela ya umma. Tanesco wamewekwa wafanya biashara wakubwa kwenye bodi na waziri mpya kwa kazi gani? Huko nyuma tumeona wafanyabiashara binafsi wakifilisi mashirika ya umma kwa maslahi yao.

Sekta ya umma tangu lini imeonyesha mafanikio kwa kuwekwa wafanyabiashara kwenye management na body ya wakurugenzi? Kama inafanyika kwingine uzoefu kwa tanzania ni kwamba unawapa ulaji na kulifilisi shirika.

Kuhusu wizara ya nishati wengi tumeona ni upendeleo umetumika kwa lengo hasi kwa maslahi ya nchi. Aliyewekwa wala hana uwezo kama aliyeondolewa.
 
Mkuu jitahidi tu usije kupata msongo wa mawazo, au shinikizo la damu. Umeandika kwa uchungu sana.

Na kwa bahati mbaya sana haya malalamiko yako ni sawa tu na machozi ya samaki ndani ya maji.
 
Wakuu,

Waliosikia hotuba vizuri hawa wakati wa uapisho wa viongozi , Rais kakemea ukabila ni sawa kabisa Udini na ukabila ukishamea mizizi nchi kamwe haiwezi kutulia.

Nilitarajia Rais ajiite Mtanzania na sio kusema yeye Mzanzibar hii haijakaa sawa hasa kwa sisi Watanganyika tuliopoteza Identity yetu kirahisi.

Au hii imekaaje ni sahihi kweli kuanza kuutupa Utanzania na kuutukuza Uzanzibar?
 
Ndiyo Utajua Kuwa Hujui
Serikali Yangu Hakuna Kubembelezana
Ngojeni Atakaye Kuja Ndiyo Atawabembeleza
By Jiwe
 
Wewe ni moja kati ya watu wapuuzi humu. Nyerere alikikubali kizanaki na kukiongea hadharani. Maghufuli jukwaani alikuwa akihutubia live kisukuma . Hatukuwahi kukuona wala kukusikia ukihoji [emoji102].

Bora hata huyo Samia kasema ukweli. Licha ya kuwa mZanzibari hapendi ukanda. Tuondolee usukumagang hapa [emoji107]

..sikumbuki Nyerere kupanda jukwaani na kuzungumza Kizanaki na kutoa ujumbe mahsusi kwa Wazanaki wenzake.

..alichokuwa akifanya Nyerere ni kutolea mifano na vichekesho vya Kizanaki ktk mazungumzo yake. Na alikuwa akitafsiri kwa Kiswahili hapo hapo, on the spot.

..Nyerere alipozungumza Kizanaki aliwalenga watu wote, na alitoa tafsiri kwa Kiswahili.
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"

Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.

Samia umekosea sana!
Hii tabia ya kuchukua neno moja ili kupotosha kauli za Rais inakera sana! Rais kazungumza Uzanzibar kuua primitive notion ya ukabila. Kwamba mtu akitenguliwa anasema kisa kabila lake. Ili uelewe ni hivi; hakuna kabila la Zanzibar.
 
Back
Top Bottom