Kusema yeye ni Mzanzibari tayari ni ukabila au ukanda ni bora angesema mimi ni Mtanzania Visiwani/Zanzibari.
Kila Mtanzania ana kabila la asili ambalo linasaidia kufahamu na kutambulisha mila na desturi pamoja kwa yakini uraia wa mtu hata huko Zanzibari kuna Wakoja, Wangazija, Wamakunduchi, Wamvita, Watangana, Wakilindini, Wabarawa, Wakiamu, Wapokomo, Wapemba, Wakivanga, Wakiriama, Wakiduruma, Wakijibana nk.
Kuna makabila zamani nchini Tanzania yalikuwa yakwepwa kupewa nafasi za uongozi ngazi za juu kwenye utumishi wa umma na serikali kwa hofu ya uwiano wao kuhitaji wawe wengi ili kuridhika kwamba ni sehemu ya ujenzi wa taifa. Kuna baadhi ya makabila tangu yalisikika yenyewe tu ikidaiwa kwamba wamesome sana ndio maana walipewa nafasi za uongozi wakati sio kweli.
Ukichukuwa kwa mfano Wanyakyusa walioko wilaya za Rungwe na Kyela mkoani Mbeya, Wasukuma walioko mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Tabora na Simiyu kwa kipindi kirefu hawakuwa washirika wakubwa wa kiuongozi wa juu sio kwamba hakuna aliyesoma au uwezo ila ni hofu ya uwingi wao kumeza nafasi za wengine kitu ambacho pia sio kweli.
Taifa linatakiwa likwepe sana dhana ya kutoa uongozi kwa mtu kwa taswira ya UDINI, UKABILA, UKANDA na ITIKADI za chama cha SIASA kudhibiti mawazo mbadala yenye kuleta tija kwa Taifa la Tanzania (Bara & Visiwani).
Zamani kabla na wakati wa ukoloni kulikuwa na tawala zenye nguvu sana zikijulikana kama
1. Meruland
2. Chaggaland
3. Pwaniland iliyoanzia Somalia, Kenya, Tanganyika, Zanzibar, Comoro hadi Sofala Msumbiji,
4. Sukumaland
5. Songealand
6. Nk
Enzi za Mwalimu Nyerere wilaya ya Mwanga huko Kilimanjaro chini ya waziri wa fedha na baadae akawa waziri mkuu ndio iliyoonekana kuwa na maendeleo makubwa ya miundo mbinu za barabara za lami, maji na umeme huku wila jirani yake ya Same ikiwa baki kuwa hoi katika nyanja zote; leo hii wilaya hiyo rasilimali zote zimechakaa hakuna wakuziendeleza huku wilaya iliyokuwa nyuma kimaendeleo ya Same iking'ara kwa miundo mbinu ya aina zote mpaka wazekezaji wanavutiwa kuwekeza huko (suala ni mipango inatakiwa iwe ni endelevu hata aliyekuwa ameanzisha akiondoka anayekuja anatakiwa kuendeleza kwa faida ya wananchi sio kuendekeza ukomoaji kwa visingizio vyovyote vile.
Maumbile ya kijiografia ya uliokuwa mkoa wa Shinyanga yafanana na jinsi ulivyo mkoa wa Morogoro kwa sasa ambapo unakuta wilaya moja iko mbali karibia kilomita 300. Shinyanga iligawanywa kutokana na ongezeko la watu hivyo mahitaji ya kiutawala kuongeza kuwa karibu zaidi wakati Morogoro kwa wilaya za Mahenge na Malinyi umbali unawatesa sana wananchi kupata huduma stahiki kwa wakati. Laiti kama kungekuwa na uwezekano wa wilaya hizo kuhamishiwa Iringa ambapo ni kati ya kilomita 140-150km wangehama zamani maana ni karibu kwao.
Kuiita Uzanzibari, Uunguja, Upemba au Utanganyika ni ubaguzi ambao mwisho wake wengi wakikasirika wachache wanaweza kuja kupata shida sana huko mbeleni.
Kwa mfano Watanzania Zanzibar wa Pemba ya kasikazini wanamanung'uniko ya kutothaminiwa na kubaguliwa kwamba wana nasaba na waaarabu wa kishirazi; siku wakipata madaraka ya kuongoza nchi taifa litagawika vipande kadhaa hatarishi kwa umoja wa kitaifa.
Kwa sasa kuna chuki inayoenezwa na baadhi ya Watanzania wenye chuki binafsi dhidi ya JPM kwamba alipendelea wasukuma, alikuwa hashauriki, alikuwa dikteta (kila mmoja ni dikteta kwa nafasi ya dhamana aliyokabidhiwa kuisimamia ili atekeleze kile alichoagizwa na wananchi afanye) hoja ambayo haina ushahidi thabiti ukilinganisha na wingi wao nchini. Watu wanathubutu kumtupia lawama zote bila mamlaka ya nchi kukemea kitu kinachotengeza chuki nyingine dhidi ya nyingine ndani ya chumba kile kile. Siku wakiacha kusemeshana wenyewe ndani wananchi watakipata cha mtema kuni.
Kwa muda mrefu utamaduni wa kila mtumishi kuwajibika kutumikia wananchi kwa ufanisi uliachwa kusimamiwa kwa kisingizio cha demokrasia hivyo kupelekea kila mmoja hasa wasio na maadili mema kutumia nafasi hizo kujinufaisha wenyewe huku wakiwadharau raia waliowapa kazi na kuwalipia mishahara yao kupitia tozo, kodi na michango lukuki bila manung'uniko yoyote.
Viongozi wa nchi acheni kuongoza au kutawala kwa kuelemea UDINI, UKABILA, UKANDA, RANGI ya mtu na ITIKADI Kinzani yenye tija.
Viongozi msitumie vitisho mnapokosolewa kwa kuwa ndio kioo chenu kujirekebisha ili kufanya vema zaidi (dhana ya KUKOSOA na KUKOSOLEWA) ifanye kazi kwa vitendo bila kuangalia nafasi ya mtu mkubwa akubali kukosolewa kama yeye anavyokosowa kwa wanaofanya kinyume na matarajio yake kwa niaba ya wananchi.
Wananchi ndio waajiri wa watumishi wa umma na serikali hivyo kujirekebisha kutokana na kukosolewa huongeza imani, heshima na kutahaminiwa nao.