Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 96
- 1,745
Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.
Mama wakati uko bize kujiandaa na mkutano wa Nishati Chalamila amemdihaki na kumdharau mwanamke wa Tanzania.
Mama wewe ni mwanamke, ulipata mimba, ulipata uchungu, na kisha uliingia Lab kujifungua.
Unajua vizuri kadhia wakati wa mchakato huu . Fikiria upo ndani ya mchakato huu hasa hii ya mwisho ya kujifungua.
Fikiria unaenda hospitali hukuti vifaa. Fikiria unaomba ufafanuzi kwa kiongozi wako wa Mkoa halafu kiongozi huyo anakujibu hivi " TOKA NJE CHUKUA BAJAJI, NENDA ZAKO NYUMBANI KAMWAMBIE MUMEO ACHUKUE VISU NA MIKASI AKUSAIDIE KUJIFUNGUA"..*
Hata kama ingekuwa ni kweli kuwa mjamzito anatakiwa kujinunulia vifaa vya kujifungua, je hii ndio namna bora ya kiongozi kumjibu mama aliye katika uchungu wa kujifungua aliyeomba tu kupata ufafanuzi kutoka kwa kiongozi wake.
Je tumemuacha Chalamila aendelee kutamba kwasababu ni Mkuu wa Mkoa !!, vipi kama maneno haya yangetamkwa na Daktari wodini.
Mama, wanawake wa Tanzania wameghadhabishwa sana sana na maneno ya huyo mteule wako, na wanasubiri kuona ni hatua gani zinachukukiwa dhidi yake.
Uchaguzi ni mwaka huu na hakuna shaka unahitaji kura za wanawake ambao wengi wao ndio wapiga kura, chukua hatua mtu wa hovyo kama huyu asikuharibie.
Ikiwa upinzani utachukua ile Clip na kuzunguka nayo katika kampeni na kuwasikilizisha wanawake kila wanapoenda, na wakaambiwa kuwa mtu huyu kwa baraka za rais bado yuko ofisini, basi huenda ikabadili matokeo pakubwa.
Soma Pia: RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani
Mama jitenge na Chalamila katika hili na namna ya kujitenga naye unaijua. Waoneshe wanawake wenzio ambao ni WAJIVUNI kwa kuwa kwako madarakani kama rais mwanamke mwenzao.
Mtu ambaye haheshimu Mama wa Kitanzania hawezi kukuheshimu na wewe pia kwasababu na wewe pia ni Mama kama huyo aliyemdhihaki.
Mtu ambaye haheshimu hata mchakato uliomleta duniani hawezi kuheshimu lolote. Kama mama yake Chalamila angejibiwa vile wakati akimzaa huenda leo asingekuwa duniani na asingekuwa Mkuu wa Mkoa.
Chalamila hawezi kujificha kwenye mkutano wa Nishati na ikapita bila kushughulikiwa.
Wakati dunia ikipambana kumuinua mwanamke bado tunao viongozi MAJUHA ambao hawajapata vizuri hii dhana.
Ukiacha maeneo muhimu ya kumuinua mwanamke kama Kumtua ndoo kichwani, nishati mbadala ya kupikia, haki katika umiliki mali, usawa katika nafasi za uongozi, usawa katika elimu, eneo jingine muhimu sana ni masuala ya UZAZI kwa mwanamke. Kiongozi anayeleta mzaha katika haya hawezi kuendelea kuwa kiongozi.
Mama JITENGE na Chalamila upate kura za wanawake.