Unashughuki
Unashughulikiaje masuala hayo ya msingi chini ya uongozi kama wa Chalamila. Huoni uhusiano uliopo kati ya uongozi wa hovyo na kukosekana kwa huduma za kijamii zikiwepo huduma za kiafya? Matatizo ya nchi za kiafrika yanatokana na uongozi mbovu. Hatua ya kwanza ya kukabiliana na matatizo yetu ni kuukubali ukweli huu na kuufanyia kazi.Issue ya Chalamila ni petty kwa sababu siyo issue ya msingi. Kushughulika na Chalamila ni sawa na kushughulikia mahali alipoangukia na ukaacha mahali ulipojikwaa!
Issue za msingi ninazoziona mimi ni hizi:
Kwanza, kushughulikia huduma za afya zenyewe na kuziboresha ili zitoe huduma insyokidhi mahitaji ya wananchi.
Pili, tunapaswa kujiuliza ni kwa nini huyo mama anakosa elfu 50 kwa ajili ya matibabu? Hapa ninalenga kuimarisha uchumi wa wananchi ili wajiongezee mapato yatakayowawezesha kulipia huduma za afya, na nyingine zinazotolewa.
By all means, kumshughulikia Chalamila hakutaweza kutatatua changamoto za kiuchumi na huduma za afya zinazotukabili.
Tushughulikie masuala ya msingi.