Wakuu,
Kwani nyinyi mliokuwepo mliona nini? 🤕
==
Rais Samia amewashukuru wananchi wa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kwa imani kubwa waliyompatia katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akiahidi kurejea tena Mkoani Arusha kutoa shukrani zake kwa wananchi.
Samia amesema hayo Ijumaa Novemba 21, 2025 alipotua katika Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) na kuzungumza na wananchi waliofika uwanjani hapo Kumpokea, akianza ziara yake ya siku mbili Mkoani Arusha. Ambapo leo Jumamosi Novemba 22, 2025 anatarajiwa kutunuku Kamisheni na Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha.