voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
Kuyajua madini ni suala la Proffesional ya miner's na sio ya waziri.Kwenye mada moja kwa moja bila kuchoshana.
Kwako Mh. Rais, naomba kama itakupendeza mtumbue Waziri wa Ardhi Anjelina Mabula na nafasi yake mpeleke Dotto Biteko huku Prof. Sospeter Muhongo achukue nafasi ya Waziri wa Madini.
Dotto atafaa Sana Wizara ya Ardhi Ili kuwanyoosha matapeli wa Wizara ya Ardhi kuliko huyu Anjela wa Sasa maana hakuna anachofanya.
Nasema kwa sababu Wizara ya Madini inahitaji mtu mwenye exposure kama Muhongo,huwa anatoa mchango mzuri Sana Bungeni na anaweza kutuvusha zaidi.
Kama ukifanya hivyo Kwa Bashe na Bashungwa ambao tunaona wanafanya Vizuri basi ni muda Sasa wa kutumia potential za Prof. Muhongo.
Natambua Rais hapangiwi ila sio vibaya kutoa ushauri..Na yule Mzee Naibu wa Madini.sijui anafanya Kazi gani maana hata kiswahili hajui anajua kimasai tuu angefaa kuwa Naibu wa Mifugo na WA mifugo aje Wizara ya Madini..
Kuna ma geologist kibao huko wizarani.
Uwaziri unaendana na uadilifu wa mhusika na jinsi ya kusimamia miongozo ya wizara bila kuwa na tamaa za fisi.
Muhongo ungemshauri aombe kazi BARRICK na angepokea mshahara mzuri kuliko wa uwaziri kama anatosha.
Lakini pia umeongea jambo la msingi sana kuhusu hii wizara ya ardhi.
Tatizo ni kwamba Mabula amewekwa pale kama kiini macho tu.
Mambo yote ni Riziwani.
Ndio maana uliiona jeuri ya GSM kupata kwa haraka Nyaraka mpya za umiliki wa kiwanja walichomuuzia Makonde huko kitambo.
Mambo ni mengi sana
The Sunk Cost Fallacy !
Mengine tumebaki kama watazamaji uwanja wa Mkapa.