Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Kwa habari nilizonazo ni kwamba Kampuni ya Sahara Media inayomilikiwa na ANTHONY DIALLO iko katika kipindi kigumu kuelekea kufilisika au kupigwa mnada kutokana na madeni makubwa yanayo mkabili mmiliki wake hasa kutoka kwa wafanyakazi wake wa vituo vya Star TV, Radio Free Africa na KISS FM.
Wafanyakazi wa vituo hivyo wanadai malimbikizo ya mishahahara kuanzia miezi mitatu hadi mitano.
Baadhi ya wafanyakazi wameanza mgomo toka Jumapili kushinikiza kulipwa pesa zao na huku wakijipanga kumpeleka mahakamani mzee Diallo na kuiomba mahakama kupiga mnada kampuni ya Sahara ili kulipa madeni yao ambayo wamekuwa wakiyadai kwa muda mrefu sasa.
Ni wakati wa Rais Samia na CCM Kumsaidia mzee Diallo katika kipindi hiki kigumu anachopitia maana yeye ni mwanaccm mzalendo.
Na wasilisha kwaajili ya utekelezaji