Rais Samia na CCM yake, 'Acheni Jeshi la Polisi lifanye kazi zake'

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Mnyonge mtamnyonga lakini haki yake hupewa.

Rais Magufuli kama angeaamua kucheka na nyani, kama angeaamua kutolipa Uhuru Jeshi la Polisi kwenye kudeal na waalifu, basi Tanzania ingeogopwa Duniani.

Nani asiyekumbuka Yale ya Kibiti? Nani asiyekumbuka Ujambazi ulokithiri wakati wa Uongozi wa JK? Nani asokumbuka Visa na Mauaji yalofanywa na Vijana wa Panya road wakati wa JK? Nani asokumbuka utekaji wa MaBUS? Nani asokumbuka biashara za magendo barabarani zilivyokua zimekithiri?

Taifa Mungu akalipa JPM, naye akasema Polisi msionee huruma Mualifu, mshughulikieni kwelikweli. Akawapa nguvu, akawaongezea POSHO, Polisi wakafurahia kazi, Kazi ikapigwa usiku na Mchana, Wahalifu wakatiwa nguvuni, Wahalifu wakakimbia Nchi, Nchi ikatuliaa kwelikweli.

JPM amerudi Kwa Baba yake, Taifa likapata Mwanamama, yeye anataka Wafungwa wabembelezwe , walishwe Kwa Tozo za Watanzania, yeye anataka watu wawekwe Mahabusu pale tu Uchunguzi utakapokua umekamilika, yeye analitaka "Jeshi la Polisi lijichunguze"? Eti mpaka ameunda Tume ya kulichunguza Jeshi la Polisi? Sahizi wammpelekea SHERIA, Et Wauza Madawa ya Kulevya wawe na Magereza Yao ya Kifahari. Hatujakaa sawa, Makamo Mwenyekiti naye, anawataka Polisi barabarani kupunguzwa, Kisa? Et ni wengi, Kila Mara kusimamisha Magari!

Kwa Teknolojia gani Barabaran tulonayo mpaka uondoe Polisi barabarani? Ukweli ni Kwamba, Wafanyabiashara za magendo Sasa wana uhakika wa kuhonga Mara Moja tu na mizigo Yao ikafika pale inapotakiwa kufika.

Katika kupambana na Uhalifu, Polisi inapaswa kuachwa ifanye kazi zake Kwa weredi bila Maneno ya Wanasiasa.

Oneni sana, Panya road wanamapanga tu ila Sasa Dar yote imetulizwa. Je, Wakianza kutumia Silaha za moto?

Matukio ya Ujambazi yameongezeka,, matukio ya vikundi vya unyang'anyi yameongezeka.

Hii yote ni matokeo ya Rais Samia, baadhi ya Viongozi wa CCM kuliingilia Jeshi la Polisi Et tu "Kutafuta Umaarufu wa Kisiasa, Tena Umaarufu wenyewe mwepesiiiiiiii usomgusa Raia wa chini".

Bahati mbaya pia, JESHI la Polisi Kwa kuhofia Nafasi zao, nao wameingia mkenge na Sasa wanaonekana hawafanyi kazi.

Mwaka 2025, Msituletee Huyu Mama, Apumzike aendelee kula Pensheni yake ya Tozo za Watanzania. Ameshindwa kila Mahali Kila kitu yeye ameshindwa, alichoweza ni kuwafurahisha watu wachache tu, MIKOPO isoonekana inafanya nn, Kuruhusu watu wale sawa na UREFU wa kamba zao!
 
Rais azungumze aache huruma
Atoe tamko ya kuwapa polisi wawashugulikie hawa panyaroad

Ova
 
Kama mnataka sheria zivunjwe tunaposhughulikia wahalifu, basi tusilalamike tena pale wakuu wa nchi wanapovunja sheria za hii nchi, naona mnataka hili taifa lijiendee tu bila kufuata sheria liwe la gangsters.

Watanzania kuna wakati tuna mawazo ya ajabu sana, kwa nje ukitutazama ni kama tunajitambua, lakini kwa ndabi hatujielewi kabisa, ndio maana tuko hapa sio kwa bahati mbaya.

Linaweza kutokea kundi kubwa la watu, lika support jambo la ajabu kwa nguvu mpaka ukashangaa, halafu madhara ya jambo hilo yakianza kuturudia tunaanza kulalamika kama kawaida yetu.

Huyu mleta mada ana support sheria zivunjwe ili kuwashughulikia panyarodi, lakini akija kugeuka upande wa pili akakuta watawala nao wanavunja sheria kwa kutoruhusu haki za wengine kutekelezwa, mfano, mikutano ya hadhara kwa wapinzani, au jamaa zetu kufia vituo vya polisi ataanza kulalamika.

Polisi wanatakiwa kuachwa wafanywe kazi yao kwa misingi ya kukamata wahalifu, ambao ni watuhumiwa, kisha wawapeleke mahakamani, huko nako mahakama ziachwe zifanye kazi yao kutoa vifungo stahiki kulingana na rekodi za mtuhumiwa.
 
Mie pia najiulila Police wa wakati wa Magufuli walifanya kazi kwa Sheria ipi ambayo huu wakati wa Samiah imefutwa
 
Hapo mwishoni kabisa ndio umeharibu kuweka siasa. Huyu huyu Samia Mungu akituweka hai tunakwenda nae 2025-30.


Umeandika mengi ukasahau kuwa hata awamu iliyopita ilikuwa ikilalamikiwa hivi hivi kama hii ya sasa, tena hali ilikuwa mbaya zaidi katika suala zima la haki za binadamu.

SSH ameshakwenda huko nje na kukutana na wakubwa wa dunia mara nyingi tu ndani ya mwaka wake wa kwanza, ameshaeleweka miongoni mwa wafanyabiashara lengo lake haswa ni lipi na litafikiwaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…