Anna Nkya
Member
- Oct 21, 2021
- 69
- 341
Sijui sana kuhusu awamu nyingine za uongozi, lakini nimemuona Kikwete, nimemuona Magufuli, na sasa namuona Samia.
Kati ya Marais hao, siajona aliyepitia mambo mazito ndani ya muda mfupi kumzidi Samia:
1. Kuchukua uongozi kufuatia kifo cha mtangulizi wake.
2. Suala la Corona. Huu umekuwa mtihani mzito hasa kwa kuangalia mtazamo wa Magufuli hususan kwenye Chanjo. Imekuwa ngumu sana kwa Samia kushawishi watu kukubali chanjo kutoka kwenye nyungu, lakini sasa wanakubali.
3. Machinga. Huu ndio mfupa mgumu zaidi. Machinga wamejazana kila kona huku wakitetewa na wanasiasa wenye nia ya kuwatumia kama mtaji wa kisiasa. Samia anapambana kuhakikisha wanakaa kwenye utaratibu.
Haya ya kelele nyingi za wapinzani hasa kuhusu kesi ya Mbowe na Katiba Mpya sio mageni, ni vitu vya kawaida sana na vitaendelea kuwepo.
Hapana shaka Samia atatuvusha salama katika haya yote, na 2025 atakapogombea tena tutampima kwa haki.