Rais Samia na Waziri Mkuu wanunua tiketi 4000 mchezo wa Tanzania vs Uganda

Rais Samia na Waziri Mkuu wanunua tiketi 4000 mchezo wa Tanzania vs Uganda

Hivi wanajua kuwa kuna shule hazina madawati wala vitabu kweli!!!
Siyo vyote ni vya kubeza, lkn najua hiyo ni moral support kwa wananchi na wachezaji.

Mh. Rais ameamua kuwakusanya watanzania pamoja kuwajengea ari ya uzalendo kwenye sports hasa football (kwa case hii), jambo ambalo litaleta hamasa kwa wachezaji na wananchi. ushindi utakaopatikana ni zaidi ya fedha ambazo zimenunua tiketi leo.

Ushindi huo ni sifa na itafanya taifa kuwa katika rank nzuri kimataifa jambo ambalo linatengeneza goodwil na footbal trust hata kwa wengine wanapoamua kuja kuwekeza hapa nchini katika nyanja ya football!

Tusiwaze Mil 12 iliyonunua tiketi tuwaze yale yatakayotokana na ushindi baada ya uzalendo kupadnikizwa kwa wachezaji na wananchi pia!!
 
Simba na Yanga ina make sense kwa sababu kwanza wanaujaza uwanja, pili hawawezi wote kukubaliana kuacha kuutumia wakati anayeenda kufaidika ni mmoja...
Umesema vyema, twende hata Azam Complex
 
Labda !!

Sionipo mtu hapo wa kutuvusha. Simba & Yanga wanafanya vizuri sasa baada ya kugundua kuwa Petre Tino, Gibson Sembuli, Zamoyoni Mogella etc. hawakuwazalisha wanawake wengi Tanzania hii.
Kama tulimpa uraia Kibu tunashindwa nini kwa Mayele
 
Umesema vyema, twende hata Azam Complex
Nadhani wa Azam haujakidhi viwango pia, labda pia kwa sababu ya nyasi bandia ila bila hivyo ungefaa na kutosha kabisa kwa mechi kama hizi.
 
Golini akikaa asha manula tu tufungwa
 
View attachment 2563576
Picha: Rais Samia Suluhu Hassan

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa wamenunua jumla ya tiketi 4,000 za mechi ya kufuzu AFCON 2023 kati ya Tanzania na Uganda.

Tiketi hizo zitagawiwa kwa mashabiki ili waende kushuhudia mechi hiyo itakayochezwa uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Machi 28 mwaka huu.

===
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hasaan na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa wamenunua tiketi 4,000 kwa ajili ya mashabiki kwenda uwanjani kuishangilia Taifa Stars itakapokuwa inacheza dhidi ya Uganda.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kupitia simu ya Meneja wa Habari wa Simba Ahmed Ally alitoa taarifa ya kununua tiketi hizo wakati wa kampeni ya kununua tiketi ili kuhamasisha mashabiki kwenda uwanjani kuishangilia timu ya Taifa.

Jumanne Machi 28,2023 Taifa Stars itacheza mechi ya marudiano dhidi ya Uganda kuwania kufuzu Fainali za AFCON 2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Tukakandwa
 
Back
Top Bottom