Rais Samia: Naamini Tanzania bila Rushwa inawezekana

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Maendeleo ya Nchi huletwa na Wananchi wake. Amesema hayo akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Zanzibar.

Amesema Sheria za Tanzania Bara na Zanzibar zimetoa Uhuru (usiovunja Sheria) kwa watu kufanya kazi. Ameongeza kuwa ataendelea kushirikiana na Rais Hussein Mwinyi kwa maslahi ya Watanzania wote.

Ameeleza, "Ninaamini Tanzania bila Rushwa inawezekana iwapo tutawaunga Mkono Viongozi wetu katika vita hii. Sote tutimize wajibu wetu".
 
Inawezekana vipi wakati juzi tu ametoka kumuhonga jaji wa kesi ya Mbowe mpaka akaamua kukimbia kesi, na huyu aliepo nae anajipendekeza anajua akiitumia vizuri nafasi nae atapewa zawadi yake, kila siku anakataa mapingamizi ya utetezi bila sababu zozote za maana.
 
Mkono Viongozi wetu katika vita hii. Sote tutimize wajibu wetu".
Binafsi nadhani ni kwa pande zote, viongozi nao watuunge mkono katika mapambano haya dhidi ya rushwa! Pia KAKUKURU iwe huru kufanya kazi yake bila kuingiliwa na viongozi.
 
Kwa kuongea tu inawezekana ila kwa vitendo haiwezekani. Waziri wake mchengerwa ni bingwa wa ru..... Na analijua hilo mbona hamuwajibishi
Kuna ushahidi wowote ili hoja ikamilike?
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Maendeleo ya Nchi huletwa na Wananchi wake. Amesema hayo akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Zanzibar.

Amesema Sheria za Tanzania Bara na Zanzibar zimetoa Uhuru (usiovunja Sheria) kwa watu kufanya kazi. Ameongeza kuwa ataendelea kushirikiana na Rais Hussein Mwinyi kwa maslahi ya Watanzania wote.

Ameeleza, "Ninaamini Tanzania bila Rushwa inawezekana iwapo tutawaunga Mkono Viongozi wetu katika vita hii. Sote tutimize wajibu wetu".
Hata ugaidi inawezekana usiwepo ikiwa tutakubali kukosolewa.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Maendeleo ya Nchi huletwa na Wananchi wake. Amesema hayo akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Zanzibar.

Amesema Sheria za Tanzania Bara na Zanzibar zimetoa Uhuru (usiovunja Sheria) kwa watu kufanya kazi. Ameongeza kuwa ataendelea kushirikiana na Rais Hussein Mwinyi kwa maslahi ya Watanzania wote.

Ameeleza, "Ninaamini Tanzania bila Rushwa inawezekana iwapo tutawaunga Mkono Viongozi wetu katika vita hii. Sote tutimize wajibu wetu".
LABDA CCM IONDOKE MADARAKANI NDIO NA RUSHWA ITAONDOKA
 
Kauli ya Kwanza kuhusu rushwa tangu kutwazwa. Tuzidi kuomba labda Mungu atatuona watanzania
 
Ila kati ya vitu magufuli aliweza, ni kupoteza rushwa kwa watumishi wa umma. hicho aliweza na sijui nani mwingine ataweza.watu walikuwa wanapelekewa pesa wanazikimbia kwasababu hawajui kama ni pesa kweli au ndoana ya kuwakamatisha.
 
ila kati ya vitu magufuli aliweza, ni kupoteza rushwa kwa watumishi wa umma. hicho aliweza na sijui nani mwingine ataweza.watu walikuwa wanapelekewa pesa wanazikimbia kwasababu hawajui kama ni pesa kweli au ndoana ya kuwakamatisha.
Huyu alikuwa exceptional...Let him rest in eternal peace
 
Hakuna kipindi wafanyakazi wa uma walikuwa na adabu kama kipindi chake, mtu masikini ametoka kijijini huko akifika ofisini wanamgombania kumhudumia kwasababu hawajui asije kuwa amejivalisha nguo chafu kuwakamata toka tiss...hahaha, miungu watu utumishi wa umma hawatakuja kumsahau.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom