Rais Samia: Naamini Tanzania bila Rushwa inawezekana

Rais Samia: Naamini Tanzania bila Rushwa inawezekana

Ni utashi tu Hangaya kapewa majeshi yote Hadi anajivalisha magwanda Yao for free halafu atuambie hawezi kudeal na Rushwa .CCM subiri akili itawarudi soon
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Maendeleo ya Nchi huletwa na Wananchi wake. Amesema hayo akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Zanzibar.

Amesema Sheria za Tanzania Bara na Zanzibar zimetoa Uhuru (usiovunja Sheria) kwa watu kufanya kazi. Ameongeza kuwa ataendelea kushirikiana na Rais Hussein Mwinyi kwa maslahi ya Watanzania wote.

Ameeleza, "Ninaamini Tanzania bila Rushwa inawezekana iwapo tutawaunga Mkono Viongozi wetu katika vita hii. Sote tutimize wajibu wetu".
Huenda hukumtendea haki kwa kuripoti hotuba aliyotoa kikamilifu, lakini kama ndiyo hotuba yenyewe hiyo, basi ni kama alikuwa anafanya mchezo fulani na maneno.

Unasema "Anaamini Tanzania bila rushwa inawezekana iwapo tutawaunga mkono viongozi katika vita hii...? Ni kiongozi gani anapigana vita na rushwa, wapi?
Na kama viongozi wenyewe ndio mafisadi..., huko ndiko kupigana vita na rushwa?

She is not serious. Ni dhahiri hii kazi ni ngumu sana kwa kiongozi huyu.

"Maendeleo ya nchi huletwa na wananchi wake"
Kwa hiyo, kafanya nini kuhakikisha wananchi wanajiletea maendeleo wenyewe. Mbona kila siku nyimbo ni wawekezaji, wawekezaji na kufungua nchi tu basi? Ni wapi aliposimama na wananchi akawachochea kweli na kuwatia moyo waone kwamba kazi ya maendeleo ya nchi yao ni ya kwao na siyo ya watu toka nje kuja hapa kutuletea maendeleo?
Hotuba kama hii kweli inatia msisimko mwananchi yeyote aone umuhimu wake katika maendeleo yake na nchi yake?
 
Anaamini tu bila bila kua na vyombo huru 😳 usikute anaamini yeye na jiwe walishinda kwa haki uchaguzi 2020
 
Kivitendo haviwezekani.Sheria zetu za hovyo kabisa,kibaka anafungwa miaka mingi fisadi anagongwa fine mtu anafisadi milioni 100 anapigwa fine milioni 5 au jela miaka 2 ataache huyu kuiba tena akipata fursa.Thus joka la makengeza KILA mipigo mikubwa yote yupo anajua udhaifu wa sheria zetu zinafunga masikini tu.
 
Tanzania bila rushwa inawezekana kabisa wakuu ila,natudia Tena ila kwa kuboresha mifumo mbalimbali ya kutolea huduma kwenye jamii zetu tofauti na hapo tutakuwa tunacheza tuu pili kazi ya kupambana rushwa siyo ya Takukuru pekee Bali sisi wananchi na wao, huwa nashangaa watuwnasema napenda kuwa afisa usalama bila kujua kuwa Kila mwananchi ni mwana usalama tofauti ni kwamba Kila mmoja anasehemu yake ya kuripoti so tumshauri Mh rais aboreshe mifumo ya kutoa huduma na malipo mbalimbali
 
Back
Top Bottom