Rais Samia: Naanza kupunguza matumizi ya mafuta ofisini kwangu, kwenye msafara wengine nitawaweka kwenye kibasi kimoja

Rais Samia: Naanza kupunguza matumizi ya mafuta ofisini kwangu, kwenye msafara wengine nitawaweka kwenye kibasi kimoja

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais Samia ametangaza hatua mpya ya kubana matumizi ya mafuta ndani ya serikali, akieleza kuwa matumizi hayo yamekuwa makubwa kutokana na wingi wa magari na safari za kikazi.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi katika Ikulu ya Chamwino, amesisitiza umuhimu wa taasisi za umma kuanza kuchukua hatua za makusudi kupunguza gharama zisizo za lazima.

"Ndani ya Serikali tuna matumizi makubwa sana ya Mafuta, magari ni mengi, safari zetu ni nyingi, niwaombe sana tuanze kupunguza matumizi ya mafututa na ninaanza na ofisi yangu. Kuanzia sasa, ninapokwenda popote, maafisa wote nitawaingiza kwenye kibasi kimoja. Msafara utakuwa na eskoti yangu, polisi na gari ya akiba nyuma. Wanaobakia wote wataingia kwenye kibasi ili kupunguza matumizi ya mafuta." - Rais Samia Suluhu Hassan akitangaza kuanza kubana matumizi ya mafuta serikalini, akianza na ofisi yake.

Rais Samia ameyasema hayo Aprili 8, 2026 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.

Hizo V8 zingepelekwa huko vijijini ndani ndani ,huku mjini tafuteni hata Coaster kama Halmashauri nyingi ...Fresh tu ,maisha safi mbona huko Geita na Kahama zinapiga kazi vizuri hizo V8 ; hiyo ndiyo kazi yake.

Kwa sasa safari za nn wakati watu wamehamia mjini ,tengenezi hata commuter system kama Udom kurahisisha usafri kutoka wizara moja kwenda nyingine ndani kwa ndani.
 
20260406_074133.jpg
 
Ndiyo muelewa kwamba its not about the people kwani kama ni kweli alikuwa anajali maisha ya watu wa tanzagiza angeshapunguza matumizi yasio ya lazima na anasa tangia zamani sana, nani amesahahu magoli ya mama na kutapakanya mamilioni kwenye mipira?

Wameamua kufanya hivyo kwa sababu kila mtu anafanya hivyo huko asia "kubana matumizi" ili na wao waonekane kama wapo relevant duniani, ni fashion tu kama ilivyokuwa lock down ya corona kila mtu alifanya lock down ili uonekane ni sehemu ya dunia na hii ya sasa ni kwa kuwa asia wanafanya kusaidia watu wao na wao tanzagiza kama kawaida wamerukia on the band wagon ili kufurahisha foreigners overseas, kama ni kweli wanataka kubana matumizi waanze kwa kupiga marufuku safari za nje rasmi tuone kuanzia juu kwa wastaafu mpaka chini, vinginevyo ni danganya toto kuwazuga international community, lkn its not about helping the people ...
 
Wabongo bado hawajafikia ustaarabu wa kuombwa kufanya mambo yatakayoenda kinyume na maslahi yao. Ilitakiwa kuwe na muongozo rasmi wa serikali kuhusu gharama za mafuta na matumizi ya hayo maviete(V8) kwa wafanyakazi wa serikali.
 
Rais Samia amesema "Ndani ya Serikali tuna matumizi makubwa sana ya Mafuta, magari ni mengi, safari zetu ni nyingi, niwaombe sana tuanze kupunguza matumizi ya mafututa na nina anza na ofisi kwangu, kuanzia sasa kwenye msafara wangu wengine nitawaweka kwenye kibasi kimoja kukataka matumizi ya Mafuta"

“Tunaanza kupunguza matumizi ya mafuta… ninaanza na ofisi yangu. Kuanzia sasa, ninapokwenda popote, maafisa wote nitawaingiza kwenye kibasi kimoja. Msafara utakuwa na eskoti yangu, polisi na gari ya akiba nyuma. Wanaobakia wote wataingia kwenye kibasi ili kupunguza matumizi ya mafuta,” Rais Samia Suluhu Hassan akitangaza kuanza kubana matumizi ya mafuta serikalini, akianza na ofisi yake.

Rais Samia ameyasema hayo wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.

Hizi akili zimekuja leo kama ufunuo kwa Yohana?
 
Yale mayai ya samaki na maji toka Amerca vipi ataacha pia? aache usanii Samia hana mapenzi na Tanganyika everyone knows!!! unless you are blind
 
Back
Top Bottom