Rais Samia: Naanza kupunguza matumizi ya mafuta ofisini kwangu, kwenye msafara wengine nitawaweka kwenye kibasi kimoja

Rais Samia: Naanza kupunguza matumizi ya mafuta ofisini kwangu, kwenye msafara wengine nitawaweka kwenye kibasi kimoja

Mimi naona nchi zetu kama za kiafrika mambo ya kidunia tuko nyuma sana ,tuishi bila ya kuforce ...Yaani tulitakiwa tuishi kama vile tunajikwamua yaani kizalendo zaidi na tukubaliane.

Kutokana na umaskini wetu ,kuanzia serikali mpaka watu binafsi tusitumie gharama katika vitu vya kuagiza labda kujenga viwanda ..Watu wasiagize nagari ya bei mbaya ili tuishi tukijua sote kama nchi tuko nyuma...Isiwe mtu anaagiza vitu vya billion of money ,ambavyo ni lavish labda iwe ishu za uzalishaji kama mashine au magari ya kibiashara.
 
Hivi huyu anajitambua kweli?

Dola 8000 [$8000] / Tsh 20,000,000 ?? kwa lita moja?

Halafu nani alimdanganya U.S. inatumia mfumo wa liter , asichokijua ni gallon ndio kipimo cha mafuta na sio liter na gallon 1 ni liter 3.785.

U.S. mafuta yapo pia katika category tofauti kuna premium, mid grade na regular.
 
Katika hotuba hiyo, Samia alinukuliwa akisema bei ya lita moja ya mafuta barani Ulaya imefika Euro 6,000 (takriban Tsh. Milioni 18), kabla ya kufanya marekebisho ya papo hapo kuwa ni kati ya Dola 500 na 800—kiwango ambacho bado kimezua taharuki kwa kuwa ni kikubwa mno kulinganisha na hali halisi ya soko la dunia.
 
Hivi mh. Hana maarifa kiasi hiki? Hana taarifa za dunia miasi hiki, hajui hata dolar moja ni kiasi gani, kweli lita moja ikawe dola 8000!? Hii kwa mtu wa kawaida ukimwambia hili bado atagoma, mpaka unapewa taarifa mbovu hizi nawe unazitoa lazima kicjwa yako iwe haiko sawa.
 
Rais Samia ametangaza hatua mpya ya kubana matumizi ya mafuta ndani ya serikali, akieleza kuwa matumizi hayo yamekuwa makubwa kutokana na wingi wa magari na safari za kikazi.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi katika Ikulu ya Chamwino, amesisitiza umuhimu wa taasisi za umma kuanza kuchukua hatua za makusudi kupunguza gharama zisizo za lazima.

"Ndani ya Serikali tuna matumizi makubwa sana ya Mafuta, magari ni mengi, safari zetu ni nyingi, niwaombe sana tuanze kupunguza matumizi ya mafututa na ninaanza na ofisi yangu. Kuanzia sasa, ninapokwenda popote, maafisa wote nitawaingiza kwenye kibasi kimoja. Msafara utakuwa na eskoti yangu, polisi na gari ya akiba nyuma. Wanaobakia wote wataingia kwenye kibasi ili kupunguza matumizi ya mafuta." - Rais Samia Suluhu Hassan akitangaza kuanza kubana matumizi ya mafuta serikalini, akianza na ofisi yake.

Rais Samia ameyasema hayo Aprili 8, 2026 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.
Anawaomba au ni agizo?
 
Unapunguza matumizi ya mafuta katika ofisi yako hiyo itasaidia kushusha bei ya mafuta ?
Nilitarajia matumizi yote ya hovyo uyazuiye alafu pesa utakazookoa upeleke kama ruzuku ya mafuta ili mafuta yashuke bei
 
Hivi mh. Hana maarifa kiasi hiki? Hana taarifa za dunia miasi hiki, hajui hata dolar moja ni kiasi gani, kweli lita moja ikawe dola 8000!? Hii kwa mtu wa kawaida ukimwambia hili bado atagoma, mpaka unapewa taarifa mbovu hizi nawe unazitoa lazima kicjwa yako iwe haiko sawa.
ANA D YA KISWAHILI TU, MENGNE NI FA FA FA
 
Hapo tunakwenda kuivaa hasara nyingine, hayo magari hususani range rovers yanapokaa bila kutumiwa au kuwekewa mafuta ya kutosha mara kwa mara yataharibika tu.

Tuna haja ya kuangalia zaidi ya kubana matumizi ya mafuta
 
Samia kwa hiyo kauli yake ya kupunguza msafara wa viongozi kwenye safari zake, namuona ni sawa na mgonjwa wa malaria aliyeamua kutibu homa.

Watanganyika tunataka bei ya mafuta ishushwe ili tuwe na nafuu ya kupata huduma, sasa yeye anapoamua kupunguza msafara wa viongozi wake, huku bei ya mafuta ikiendelea kuwa juu anamsaidia nini mtanganyika?

Asitudanganye tunaumia wote, ukweli ni kwamba mtanganyika ndie anaeumia zaidi, kwani yeye ndie anaepambana na kodi za kila aina na tozo zinazotengenezwa na serikali yake.
 
Back
Top Bottom