Rais Samia ametangaza hatua mpya ya kubana matumizi ya mafuta ndani ya serikali, akieleza kuwa matumizi hayo yamekuwa makubwa kutokana na wingi wa magari na safari za kikazi.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi katika Ikulu ya Chamwino, amesisitiza umuhimu wa taasisi za umma kuanza kuchukua hatua za makusudi kupunguza gharama zisizo za lazima.
"Ndani ya Serikali tuna matumizi makubwa sana ya Mafuta, magari ni mengi, safari zetu ni nyingi, niwaombe sana tuanze kupunguza matumizi ya mafututa na ninaanza na ofisi yangu. Kuanzia sasa, ninapokwenda popote, maafisa wote nitawaingiza kwenye kibasi kimoja. Msafara utakuwa na eskoti yangu, polisi na gari ya akiba nyuma. Wanaobakia wote wataingia kwenye kibasi ili kupunguza matumizi ya mafuta." - Rais Samia Suluhu Hassan akitangaza kuanza kubana matumizi ya mafuta serikalini, akianza na ofisi yake.
Rais Samia ameyasema hayo Aprili 8, 2026 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.