Rais Samia: Nakwenda kufungua Nchi, mmekuwa mkinitukana sana mitandaoni

Wanapoteza muda.
 
uchumi unaujadili hapa jukwaa la siasa!!!!na hutaki siasa zijadiliwe hapa.unatumia pombe zilio expire???

kama hujui kupigwa na ccm kukoje,huna uwezo wa kujua wanapokupa faida ccm.
 
Nadhani nchi yetu kufikia maendeleo itakuwa challenge kidogo, ukisema unafungua nchi kwani nchi hii imefungwa? nchi iko wazi tu kwa uwekezaji miaka yote muda wote, suala la muhimu ni kuangalia he ni uwekezaji upi? una maslahi? kumbukeni suala la uwekezaji sio geni Tanzania, suala la uhusiano na Kenya sio geni ni la kawaida tu na huwezi ukategemea uwekezaji wa Kenya ututoe katika umasikini labda kama tunataka uchumi mdororo.
 
Asante

Kutatua tatizo la ajira Paypal Tanzania iruhusiwe kama ilivyo kenya

Tanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au Marekani

Pia, mtu waweza chora hata katuni, ramani za nyumba n.k ukauza online. Au, ukajitungia wimbo wako wa kienyeji binafsi nyumbani kwako bila hata kwenda studio, ukauweka kwa mfumo wa video au audio ukauuza online kwenye maduka kibao ya online.

Tatizo kwa Tanzania haijaruhusu matumizi ya kupokea pesa kwa njia ya PayPal ambapo mtu aki-click tu kununua bidhaa yako, pesa yako inaingia chapchap kwenye PayPal account yako.

Kenya walisharuhusu; vijana wengi hushinda mitandaoni wakitengeneza pesa wakiuza bidhaa zao, viwe vichekesho, michezo ya kuigiza n.k ambavyo huviuza online. Wanaweka clip zao kwenye maduka ya online mtu ananunua anamlipa online kupitia Paypal.

Kuna shughuli nyingi za ujasiliamali online. Kikwazo kwa nchi yetu ni upataji wa pesa wa kazi yako au mauzo yako online. Bado tuko enzi za mawe tukiamini minjia ya kizamani ya kupokea hela. Na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa ni ya kulipa zaidi pesa za kigeni na si ya kupokea pesa za kigeni.

Serikali ikiruhusu upokeaji pesa kupitia PayPal itafanya vijana wengi waingie mitandaoni kutafuta pesa.

Biashara za online zaweza kufungua Watanzania wengi kupata pesa toka nje, sababu ni juhudi ya mtu binafs na ubunifu wake tu auze nini. Waweza kujirekodi unarukaruka kama ngedere ukiimba hovyohovyo tu bila hata vyombo halafu ukaita wimbo Crazy Monkey Song ukauweka online na ukauza. Wapo watu wana pesa wanapenda vituko wananunua.




Taasisi za elimu nazo ziweke kwenye mitaala ujasiliamali wa online wasibakie tu kufundisha ujasiriamali wa kuzurura tu juani wa kimachinga.

Tumepiga kelele mno humu

Source:Kupunguza tatizo la ajira serikali iruhusu huduma ya kupokea pesa kupitia PayPal
 
Na madawa ya kulevya yameshafunguliwa!

Wauza ngada wataneemeka mno!

Riziwani anakenua sasa hivi....
Chunga watoto wako wasile, fundisha familia yako adabu maana Madawa DEA wameshindwa sisi tutaweza wapi kuyakomesha?

Kikubwa tu zama za kuaminishana kila Tajiri anauza Madawa au kuna vita za Kiuchumi zimezikwa Chato
 
'Industrial parks' ni eneo gani hilo...
 
uingereza ikajitoa baada ya kugundua inajila.
Uingereza wanajiona hawako ulaya na hivyo kujiona si mmoja wao.
Amini usiamini ilipofikia waingereza wanajiona wajinga kwa ule uamuzi wao lakini kwa hatua iliyofikiwa ni lazima waondoke.

Boris anapiga danadana anasogeza mbele kwa visingizio lukuki lakini wenzake wamesema hawamwitaji tena. Nguvu ya nchi za Ulaya ni umoja wao, bila hiyo ni wepesi sana.

Tukiimarisha uhusiano wetu tutakuwa na nguvu kuliko hapo zamani.
Naombea tuje tufikie kwenye fedha moja na hata jeshi la pamoja.
 
FUNGUA NCHI MAMA! KONGOLE TUNATAKA WIN WIN

TUPATE AJIRA NAWE UPATE KODI YAKO.
 
Mama anatufungulia dunia tuwe tunachotaka.....

Kikubwa ni kufuata taratibu na sheria na kuweka maslahi ya taifa mbele
... mashaka ni akili zilizoko Bungeni kama zitaweza kweli kuboresha na kutunga sheria za maana za kutuvusha! Kama mipasho yenyewe ndio ile kuna kazi sana Bungeni.
 
Akifeli au mnaombea afeli?!

Nimekuuliza kuna ubaya upi kwa Samia kama Rais kutaka kuongea na business community, na kufungua milango ya biashara?

Sina kawaida ya kutojibu post, na wala sijaona hiyo post yako kuhusu mahindi... weka hapa!!!

Post zako 3 za mwisho ni:-
Sasa unaniuliza habari za makada wa chama wakati post yangu haikuhusiana na habari za makada?

Na kama anatekeleza ya wenzake, sasa hizi legacy mnazoimba zinatokana na nini?! Kwanini mnadhani yeye ndie anastahili hizo legacies wakati kuna miradi kaikuta imetafutiwa hadi pesa, na yeye katekeleza tu lakini bado mnaimba legcy ya JPM!!

Post yako nyingine ni hii:-
Mara ya kwanza nilikuambia wewe ndo wale wanaodhani urais wa JPM ni wa Wasukuma wote kwa sababu ulionekana unawafahamu sana Wasukuma kuliko Wakwere?!

Lakini uliposema wewe Mhehe, wala sikuendelea kusema wewe ni Msukuma... sasa ulikuwa na sababu ipi ya kusisitiza kwamba "...nimekuambia mimi ni mhehe" wakati post yangu ilikuwa inasema:-
Hiyo post unaona inakulenga wewe?

Lakini sitaki kuwa mnafiki... WEWE HUONGOZWI NA ITIKADI BALI NI MFUASI WA MTU!! Anayeongozwa na itikadi hawezi kupinga kila kinachofanywa na rais aliyetoka chama kile kile!!! Na wengi wa aina hii ni watu wa kanda maalumu ingawaje wapo wanaojitambua miongoni mwao!!

Wana-CCM wa kweli wanamuunga mkono Mama kwa sababu kwao, JPM na Mama ni kitu kimoja!!

Aidha, post yako nyingine miongoni mwa zile 3 za mwisho inasema:-
mbona hujiamini ndugu yangu,nafsi inakusuta eh???

nasemajee jpm hakuna akichofanya,vyote ni bure.
Sasa hiyo post ya mahindi ni ipi?!

Btw, kwanini nishindwe kujibu hoja nyepesi kama ya mahindi?!

Anyway, jibu maswali niliyokuuliza kuhusu ubaya wa Samia kutaka kufungua milango! Au unaona anam-challenge Malaika Mtukufu Mungu ambae bila aibu mnafikia kumlinganisha hadi na Nyerere!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…