Rais Samia: Nani atazikwa na hela?

Hii sio kauli ya amiri jeshi mkuu hata kidogo. Mwizi wa hela, hela ilivyo tamu, hela ni madaraka, hela kwa sasa ndio kipimo cha utu/ubinadamu, hela ni pesa...then unakuja na simple statement, unadhani mtu anashtuka?
 
Samia badala asimame kama Rais, anasimama kama mchungaji ama mtume.

Watu wanakula hela yeye anawahibiria.

Mifumo ni mibovu ndio maana mnataka rais achunge hela. Kwenye mifumo yenye nguvu, CAG angejiridhisha na wezi amgewapeleka mahakamani kwa kesi. Sio mambo ya kusubiri rais wakati hakuna uhakika kama rais ni muadilifu. Kuna mwingine hivi majuzi alikuwa anajifanya mzalendo, matokeo yake imekutwa account huko China.
 
Rais Samia S
Rais Samia Suluhu alionyesha kukerwa sana na wezi wa pesa za umma kwaiyowasijidanyanye kuwa kuongea vile ndio imeishia hapo hapo Hapana Mama hawezi kuruhusu ubadhilifu wa fedha za umma na akakaa kimya lazima awachanie mkeka siku zinahesabika
 
Lazima wawajibike mkuu we subiri tu mkeka mpya
 
Hiyo kauli ni kama ile ya yule shoga aliemumwagia mwizi shombo ya samaki kwamba akaliwe na mijipaka.
 
Exactly: Reward & Punishment
mwizi lazima aadhibiwe
hodari apewe motisha
 
Misikitini hakuna mitume,acha ujinga,uwe unajielimisha kabla ya kuzungumzia Jambo hadharani
 
Mhusika au wahusika mpaka sasa walipaswa kuwa wameshazikwa, mali zao zote mufilisi.... short and clear, kuendelea kupoteza muda na wajingawajinga matokeo yake ndio haya.

Wajinga wakiwa wengi wanachagua Rais na kuiweka serikali madarakani, wajinga wakiwa wengi wanatunga katiba yao yakuwalinda, Wajinga wakiwa wengi hata uwe na katiba bora kiasi gani watateka kila njia ili wawe salama.

Dawa ya mpumbavu na mjinga ni risasi au jela na mateso makali.
 
Huyu mama ni dhaifu hilo halina ubishi.

Hilo la china ni propaganda tu.

Rais anahubiria wala rushwa na waiba mali za umma, amekua mtume mwamposa?

Kwa nchi yenye watu wanaojielewa Samia hana sifa ya kua hata balozi wa nyumba kumi.

Ajabu ndio rais, ndio maana haya yanatokea, sasa acha ahubirie wezi kwa miaka 7 ijayo kama hii nchi itakuwepo.
 
Rais anaetegea watu kama Makamba ndio wamshauri unategemea atakua na sauti tena juu ya wizi.

Eti Rais anawaomba wezi waachie nafasi ama wezi warudishe pesa ama wasiibe eti hataenda nazo mbinguni, yeye mbinguni nani alimwambia ipo?

Rais sasa anategemea huruma za mafisadi na wezi wa mali za umma ili waache kuiba, huruma iwaingie waache kuiba, isipowaingia basi anawaambia hawataenda nazo mbinguni.

Hii nchi, tumioiga hatua mbili mbele za maendeleo, kidogo tunarudi nyuma hatua 9. Imekua ni mzunguko wa umasikini na ujinga usio isha.

Ngoja tuone kama wezi watatuhurumia waache kuiba.
 
Wanaona aibu kusema huu ukweli, wanamtetea kwa visababu vyepesi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…