Rais Samia: Nani atazikwa na hela?

Pamoja na JPM alikuwa na hofu ya Mungu hizo pesa jamaa wangezitapika..

Na huyo jamaa aliekimbia na pesa nchini angetafutwa kwa gharama zozote...

Kwake kikubwa ingekuwa pesa zirudi....uibe pesa uachiwe kirahisi eti mwizi apelekwe mahakamani ..pesa irudi kwanza ndio habari za mahakamani mtajuana wenyewe...alah!
 
Unaona ni sawa kiongozi mkuu kulalamika?

Ridhaa ya kununua Treni chakavu, mitumba Kwa Bei ya treni mpya aliitoa wapi?

Na nani aliwajibishwa Hadi sasa?
Ofcoz, si sawa kwake kulalamikia..

Na ndicho hicho kilichosemwa na mleta hoja kavulata kuwa tatizo ni kutokuwepo kwa mifumo imara ya utawala isiyomtegemea mtu mmoja aitwaye "Rais" kuchukua hatua..

Laiti tungekuwa na mfumo mzuri wa kiutawala kupitia katiba na sheria imara, basi vyombo vya kuzuia na kupambana na uhalifu i.e wizi na ufisadi ambavyo ni UWT, Polisi, TAKUKURU nk visingesubiri kupewa maelekezo au amri ya Rais ili kutenda...

Kwa hiyo, hakuna anaye support kulalamika kwake. Anapaswa kutumia mamlaka yake kuchukua hatua. Au la, basi kungekuwapo na sheria zusizohitaji ridhaa ya Rais kushughulikia uhalifu..!
 
Walitaka waone Ile ya "niwatumbue au nisiwatumbueee?" Style za uongozi ziko nyingi sana ila matokeo yake ni yaleyale TU hata ukifoka au ukisema
 
Mkuu kwani hatuna katiba?
Katiba yetu inaruhusu watu kuiba?
Katiba yetu inasema mhujumu uchumi na mwizi aachwe?
Kama Kuna Rais anaogopa kutia Saini mwizi wa Mali ya umma anyongwe alistahili kuwa Rais? Adhabu za wezi wa Mali ya umma ni ndogo mno, zinatia hamu ya kila mtu kuiba kabla hajastaafu na kabla hajaondolewa kwenye nafasi na kabla awamu haijaisha ili mtu asije kujilaumu.
 
Wewe ukimsikia Mzee makamba akiongea utajuwa TU anafunga kama, fix, porojo na uongo juu ya anachokiongea, anaona kama vile anaongea na watu wajinga wasiokuwa na elimu. Na watu wa hivyo wako wengi sana, wanaishi kwa vimemo. Wanajiona eti wao ndio wenye hati miliki ya nchi yetu, wao ndio wanaojua nchi inaendeshwaje. Hata mama Samia bila shaka wanamtaka awaulize ushauri wao kuhusu hili na lile, kama Rais ataamini kuwa Kuna watu wanaojua sana hii nchi kuliko yeye basi attashindwa mambo mengi sana ya kuisogeza na kuibadilisha nchi.
 
Kila anaekuja anakemea na mda wake ukifika anaondoka na kuacha madudu yaleyale
Viongozi wanajua fika kwanini wanaiogopa katiba
Utakuta kila Rais anaambiwa umefika hapo kwa hela za kupigwa sasa jifanye kiherehere uone

Nakumbuka Magu alikuwa analalamika sana anaposikia mtu analia kwa kudhulumiwa haki yake

Ila anapouliza huyu mtu yuko wapi anaambiwa kahamishwa au wamehamishwa
Anakaripia na kusema badala ya kumhamisha kwanini asifukuzwe hapo hapo?

Sasa hata yeye kama alilijua hilo kwanini hakupeleka hoja ikajadiliwe bungeni na kupitishwa badala yake kalalamika mpaka kaiacha Dunia na watu bado wanadhulumu na kuiba kutwa

Wanaogopa sana ila wajinga ni sisi tunaona majengo yakijengwa ya kifahari kila mkoa kwa pesa zetu huku tukiyajua kuwa kwa mshahara wao hawawezi kujenga majengo ya mabilioni
 
Hayo uliyopendekeza yatafanywa na nani kama wajinga ndio watakua wameunda serikali?
Watendaji wengi wamepata nafasi hizo kwa njia ya memo, ni ngumu sana kuwaadhibu Huku ukifikiria uchaguzi hauko mbali. Ili kuuvunja huu mnyororo wa wizi ni kumpata Rais atakaesema sitaki kura za kinafiki za machawa na waramba asali bali kura za watanzania wanaoguswa na kazi zangu za kutatua KERO zao, nikishindwa sawa na nikishinda sawa TU pia.
 
Kauli kama hii ya mkuu wa nchi, kiongo wa juu kabisa kuliko wote serikalini na katika taifa, ni dhahiri ameshindwa kutekeleza majukumu yake.

Eti rais naye analialia!
 
Sasa ww unataka wasile kama huko juu wanavyofanya
 
Rais aliposema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake alidhani kuwa wezake wana kama za katani tu, kumbe wana kamba za mipira ya manati zinazovutika zaidi umbali mrefu kuliko alioufikiria yeye. Kama hatutawapa adhabu kali wanaofuja mali za umma kama adhabu wanazopewa watu wa aina hii kule China, Ulaya, Marekani, Uarabuni na kwingineko ambako tunaona wanafanya vizuri kiumi hata wanaotupatia mikopo na misaada wanafanya kazi bure. Maana uchumi sio mapato bali matumizi ya mapato.
 
Wataachaje kuiba hela huku wamezoea hata wakikamatwa hawafanywi kitu!
Uzoefu unaonyesha kuwa kila uchaguzi mkuu wa wabunge na Rais unapokaribia fedha za umma huwa zinaibwa sana. Inaonyesha kuwa Kuna watu wanatafuta fedha ya kampeni, kubeba watu kwenda kwenye mikutano ya hadhara, takrima na mbinu nyingine. Ndio maana hao wezi miaka nenda Rudi huwa hawatajwi na hawachukuliwi hatua stahili. Mtu akihoji sana na kujifanya kutaka kuchukua hatua kali kwa wezi ataonyeshwa bajeti ya kampeni ya uchaguzi uliomuweka madarakani au itakayomuweka madarakani, ataambiwa hebu tuambie wewe hela ya kampeni Chama kitaitoa au kimeitoa wapi? Kimyaaaa!!!!
 
Nakazia..

Unyama unyama ndo mfumo..

Hawa ukiwachekea unaingia kwenye mfumo wao
 
Bora hata angewalinda tungesema Rais ni kauzu, the fact anawaogopa inanikera sana.
 
Asante sana, wewe ndiyo mzalendo wa kweli wa nchi yetu. Hayo yote ni mambo tunayotaka ikiwemo kiongozi kama rais kushtakiwa pia, mbona Israel mawaziri wakuu wanafungwa jela, USA, Korea na duniani kote isipokuwa kwenye nchi maskini tu ingawa baadhi kama Malawi, Zambia wanashtakiwa pia.
 
Ni kweli. Kwanza hiyo ni kauli ya kuonyesha kushindwa. Mwizi hatishiwi bali anakamatwa na kuadhibiwa.
Mwana mama hayo ni mambo yasiyoingia akilini mwake kabisa!

Kuna watu wameumbwa kipekee sana!
 
Ni kauli fupi sana lakini nzito kwelikweli.
Eeeehee Bhwanah!

Hiyo ni "kauli NZITO SANA"?

Huyo aliyetoa kauli nzito ya namna hiyo alikueleza kwamba hayo mahela yanapelekwa kunua mahekalu Dubai, huku ndugu zako hapo kijijini wakinywa maji ya tope?

Kwa hiyo, kwa vile hao wezi "hawatazikwa na hizo hela" basi haina maana yoyote kwa wananchi kujitahidi wapate vijisenti angalau waweze kupata milo miwili kwa siku?

Hivi nyinyi watu, na huyo unayemsifia mnazo za kutosha humo vichwani mwenu?
 
Bora hata angewalinda tungesema Rais ni kauzu, the fact anawaogopa inanikera sana.
Kinachotokea kuna watumishi na viongozi wengi ambao wana vinasaba (DNA) na viongozi waliopigania uhuru na waliowahi kuwa viongozi kwenye awamu zilizopita. Ukiwagusa hawa utakutana na manung'uniko ya waliokuingiza madaraki, wanaokutetea na watakaokuunga mkono kwenye kaampeni zako mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…