Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Ni ukosefu wa fedha tu,pesa ingekuwepo angeshusha kitu cha muitaliano " PENDOLINO" ,mtu kula miguu na vichwa vya kuku si kupenda ni kukosa pesa ya kununua mapaja
 
Naona design nyingi kutoka kwa hawa jamaa, either picha/toleo lililotumika imekuwa special product kwa Afrika.
 
hapa jamaa hata sielewi tatizo liko wapi, unacho lalamika ni uzuri wa treni au? Maana hizo mbona zinatuika nchi nyingi tu na hazina tatizo lolote. Kumbuka kuna treni za abiria pekee na kuna za abiria na mizigo.
 
Hapo ng'ombe akijichanganya sijui itakuwaje.....
Ngoma inakata kama kisu maana inakimbia kwa speed ya 350km/h mpaka 600km/h yani hapo kwa kweli hamtoona kitu zaidi ya masalia ya ng’ombe tu! Labda wawekee wavu pembeni mdudu asikatize
 
Ngoma inakata kama kisu maana inakimbia kwa speed ya 350km/h mpaka 600km/h yani hapo kwa kweli hamtoona kitu zaidi ya masalia ya ng’ombe tu! Labda wawekee wavu pembeni mdudu asikatize
Hiyo tuachane nayo kwanza tunusuru hawa ng'ombe wetu.....
 
Tatizo watu wanajifanya kujua kila kitu. Hii treni ya Hyundai ina viwango bora tofauti na Mtoa mada anavyosema na propaganda zake . Hyundai ni kampuni kubwa duniani . wangekuwa wanatengeneza India au Indonesia au Vietnam au Malaysia tungekuwa na Shaka .
Hio treni hapo chini ya ujerumani inafanana na hio ya Hyundai

 
Humu ndani watu wanavyongea utadhani wao wana drive ma ferrari na ma Bugatti...kumbe vi baby walker second hand...bora ht serikali inanunua brand new...[emoji1787][emoji1787]

kifupi ni kua serikali imenunua hizo treni kulingana uwezo wake ki fedha na uwezo wa reli yenyewe...huwezi kununua bullet train ya 350km/h ukaileta kwenye rail yetu ya 160km/h hio ni under utilization na matumizi mabaya ya fedha za umma.
But still train zetu zitakua bora kuliko za Majirani zetu.
 
Tuliahidiwa hivyo kuwa tutapata High speed trains. Hayati Magufuli na Mh Kadogosa wakati ule walikuwa wakiimba hivyo.
Hata mabasi ya mwendo kasi siyo ya mwendo kasi kweli. Watu mnataka bullet trains wakati hata reli yenyewe haikidhi vigezo vya bullet trains achilia mbali kuwa ni nchi chache zenye bullet trains.
 
Mkuu yani watu wanashangaza sasa, wanataka train ya bullet iwekwe kwenye kireli chetu, pia zile train technolojia yake ni ghali sana na ziko sehemu chache duniani. Hiyo train mimi naona nzuri sana na zinatumiaka sehemu kibao
 
Jikune pale mkono unaweza kufika! Sio unakimbilia kununua treni za bei kubwa wakati sehemu nyingi bado watoto wanakaa chini mashuleni, huduma ya maji na umeme bado shida. Kisha watu waseme Tanzania ina treni za kisasa Kupita nchi nyingi za Africa!!
 
Mkuu.zina nyuma.sasa unaposema hakuna nyuma ni kwamba dereva yuko mbele na nyuma ?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulaya hasa Ujerumani kuna baadhi ya Railway Station kama ya Munich au Frankfurt wanaziita Sackbahnhof, wakimaanisha kuwa Railway stations ambazo treni hazipiti moja kwa moja. Kwenye Stations kama hizi treni inaingia kwa mbele na kutokea kwa nyuma na kuendelea na safari. Mbele na nyuma kwote ni sawa.

Angalia hii clip utaelewa nini namaanisha. Usijali lugha. Wewe angalia mandhali yake tu.

 

Unamlaumu mama bure mzigo umechaguliwa Msoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…