Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Hiki kizazi kimejaa watu wapumbavu sana. Hiyo tender ilipita wakati wa Magufuli na mnataka kumlaumu Rais wa sasa ili mfiche madhambi ya mungu wenu aliyekufa kwa Covid.

Tafuteni lini hiyo tender ilikuwa awarded kwa hao Hyundai ndio muelewe.
Mama yako kama yupo hai unajua atakufa kwa ugonjwa gani?
 
Mmehamishia magoli kwenda kwenye muonekano wa treni kutoka kwenye "haiwezekani" mdogo mdogo tutafika tu kwenye "wahudumu wake Wana sura mbaya"
Hiyo picha ni "kielekelezo" tu cha kampuni kama nembo ya Bibi na bwana ya taifa letu, subiri picha halisi za mabehewa zije!
Dah! Mkuu umenikumbusha mbali!
 
Tumesoma na tumeona. Lakini bandiko limetolewa na manufacturer. Sasa kama alimaanisha treni nyingine basi tulitegemea angeweka picha inayo fanana na kile tulicho kubaliana nacho. Na kama sio basi mtoa taarifa ya kushinda kwa hiyo zabuni atakuwa ametudhalilisha sisi sana watabzania kwa kuonyesha kuwa hiyo ndiyo treni ambayo sisi tumestahili kuitolea Tender.
Unbelievable negative reaction to speculation

Just unbelievable
 
Wewe unangalia muundo. Sisi tunaangalia uimara na utendaji kazi. Hakuna kitu cha kumridhisha kila mtu. Pita huko usipande tumia gari
[emoji3][emoji3][emoji3] Ungejua Material Science ni nini? Usinge andika utumbo kama huo. Lakini kwa vile hujui nini maana yake na aplication yake iko vipi, ngoja nikuache kama ulivyo.
 
Nimeishia kwenye kuburudisha macho.. nikaona utakuwa hauna tofauti na vile wanawake huchagua magari kwa kuangalia rangi[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]...

Wanaume lazima aulizie engine, Mama Samia kakushinda kwenye hili mkuu.
Ningekushauri kasome tena vitabu vya kisayansi ili ujue kama treni za umeme zina engine au zina kitu kingine ambacho kinazipa power ya drive. Iangalie Fan yako ya kitandani alafu niambie kama kuna kuna engine kwenye ile housing.
 
Mkataba haukuingiwa kuleta maboksi badala ya treni za kisasa zinazotumia umeme. Umbo lililopo kwenye picha ni wazi haina uwezo wa kusafiri kwa kasi kwa kutokuwa na mizania ya upana na urefu lakini hata kukata upepo bila ukinzani hatarishi..

Usikimbilie kudai kuna upotoshaji
High speed trains zote lazima ziwe zimeundwa kwa misingi ya aerodynamic. Bila hilo CW Values zake zitakuwa kubwa na hivyo kuzifanya zitumia energy kubwa kwa matokeo madogo ya speed.
 
Haijalishi kama niko kiwandani au sio. Hii ni digital era, kwa hiyo ni busara nasi tukawa na vitu vya kuvutia na sio kuendelea kusafiri na treni ambazo zinaonekana kama ma-Container ya HAPAG Lloyd. Kwani tumekuwa mizigo sisi?

Inategemea na speed ya train maana hizo za mchongoko ni bullet train [emoji583] na hizi tunaletewa speed ndogo lazima maumbile yawe tofauti

Angalia hata train za miji mikubwa sura mbaya na ni karne hii hii
Sidhani kama bullet train zitahimili reli yetu na ndio maana wanaleta za hivyo
 
Hiyo ya juu ni High speed train, ya katikati ni treni ya kupiga masafa ya ndani ya mji na kando kando kama tuseme posta mpaka kibaha au Mkuranga. Haina speed kubwa sana. Max. Speed ni 80-100 km/h. Hiyo ya chini inaweza unganisha miji miwili na kuwa na speed mpaka 150 km/h.

Kweli
Naaafiki haya
 
Kwa uelewa wangu kutokana na kutembea nchi kadhaa pamoja na kuona kupitia media mbali mbali ni kwamba treni ya mizigo haina muonekano Sawa na treni za abiria. Hii upo hivyo China, Japan, ujerumani, Sweden na hata Korea kwenyewe. kuna picha mdau mmoja ame share hapa akijaribu kulinganisha utaona zile alizoweka ni treni za abiria. Hivyo basi hii picha inayosambaa ni kichwa cha treni ya mizigo. Ya abiria ya kwetu nayo itakua tufauti kidgo.
 
Kwani hizo ni za hii kampuni inayotajwa humu, kwa sababu hatujui muundo wake ndani na uwezo wa injini wanaweza ku-opt yoyote kati ya hizo. Kama mambo mengine mfano bei yapo constant wanaweza kuchanganya design zote kwa idadi sawia au kwa upendeleo wa design moja dhidi ya zingine....kitu kingine wangejitahidi kukamilisha kipande kizima cha SGR kutoka Dar-Dodoma ili hizo treni zianze kuleta manufaa ya haraka.
Treni za umeme basically hazina engine, zinaendeshwa kwa Rotation energy kutoka kwenye generator kama.magari ya umeme yanavyo endeshwa.

Kabla ya kuingia makubaliano ya ununuzi serikali yetu inatoa purchase offer, yaani ina bid na makampuni yanayo manufacture hizo products wanakuja na quatations na conditions zao za uuzaji.

Wataalam wetu wa serikali walio bobea katika maswala kama haya ya treni za umeme na watu wa manunuzi wanapitia quatations na conditions hizo za hayo makampuni tofauti, yaani wanaenda mpaka viwandani wanako tengeza hayo matreni na kuangalia michoro (texhnical drawings) ya hizo treni na pia kubadilishana Information za kitaalam.

Makubaliano yakifikia sisi upande wa serikali na wataalam wetu wanatoa kitabu kiitwacho requirements document ambamo ndani yake maelezo yote ya jinsi sisi treni yetu hiyo inavyo takiwa ionekane. Sijui kama sisi tunafanya hivyo. Wanunuzi wengi wa nchi tofauti huwa wanafanya hivyo.

Kwa mfano DB (DEUTSCHE BAHN) ya Ujerumani na China Railway wanafanya hivyo na hata wanawapeleka wataalam wao kwenye viwanda vilivyo pewa zabuni na kufanya kazi huko za kuzisindikiza products zao na kuhakikisha kama kila kitu kinakuwa kama kilivyo kwenye makubaliano ili kupata kitu cha uhakika na kwa bei ridhishi kwa kuangalia pia uwezo wetu.
 
Kweli mkuu hata mimi nina mashaka na hii kampuni ya Hyundai kwenye swala la ubora, vinginevyo wangechanganya na zile za kijapan na kichina...
Wachaina bado hawako vizuri katika treni mkuu. Treni nyingi unazo ziona China ninzile ambazo wameshirikiana nanmakampuni mengine kama Siemens ya ujerumani, Bombardier ya Canada, KAWASAK ya Japan na kadhalika. Sidhani pia kama Hyundai wako vizuri kwenye huu utaalam. Ndiyo kwanza nimesikia sasa hivi.
 
Back
Top Bottom