NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 9,863
- 20,806
Jinsia yake haihusiki. Dini yake haihusiki. Sehemu ya Kijiografia anayotokea nayo haihusiki.
Kinachohusika hapa ni uwezo wake mdogo alionao.
Uwezo mdogo wa kiuongozi. Uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. Na uwezo mdogo wa kujenga hoja.
Mara kadhaa sasa nimeona ona humu baadhi ya watu wakisema kwamba Rais Samia kaonyesha na kuthibitisha kuwa wanawake hawafai katika nafasi kiuongozi.
Mimi hilo nalikataa. Mtu mmoja mwenye uwezo mdogo si mwakilishi wa wanawake wote nchini wala duniani, kwa ujumla.
Uwezo wake mdogo alionao ni wa kwake yeye tu, Rais Samia.
Kilichonisukuma kuileta hii mada hapa ni yale maoni yake aliyoyatoa hapo jana.
View: https://youtu.be/O8SVrOeYtck?si=zAtsS1VP_q_B5Hmo
Rais anahoji kuwa kwani katiba ndo inaleta maendeleo?
Hivi huyu Rais hajui kuwa katiba ya nchi ndo framework ya uongozi na utawala ulio bora?
Bila uongozi na utawala ulio bora, kuna maendeleo gani yaliyo ya maana yanayoweza kupatikana?
Huo ni uwezo mdogo sana wa kufikiri ambao siutegemei utoke kwa kiongozi aliye wa juu kabisa nchini.
Au labda yeye anadhani maendeleo yanatoka wapi au yanakujaje?
Jingine la ajabu alilolizungumzia ni suala la elimu. Kwamba eti watu walio wengi hawajui hata katiba ni kitu gani. Hivyo ni lazima kwanza watu wapewe elimu kabla ya kuiandika hiyo katiba mpya.
Nilichoking’amua hapo ni ‘projection’ yake yeye kuhusu katiba.
Kulingana na kauli zake kuhusu katiba, nadhani yeye ndo hajui katiba ni kitu gani na hivyo anadhani hata wengine nao hawajui katiba ni nini!
Kenya waliandika katiba mpya mwaka 2010 [kama sijakosea].
Afrika Kusini waliandika katiba mpya baada ya kuachana na sheria za ubaguzi wa rangi kwenye miaka ya 90.
Marekani waliandika katiba yao miaka zaidi ya 200 iliyopita na ambayo wameifanyia marekebisho mara 27.
Sehemu nyingi tu duniani zimeandika katiba mpya na zingine kuzifanyia marekebisho katiba zilizopo.
Ni wapi ambako waliielimisha jamii kwanza kabla ya kuandika mpya?
Afrika Kusini walifanya elimu gani kwa wananchi kabla ya kuandika katiba yao mpya?
Waliwakalisha watu madarasani na kuanza kuwafundisha somo la katiba?
Katiba iliyopo sasa hivi wakati inaandikwa elimu ya katiba ilitolewa na nani? Lini? Wapi?
Naona sasa suala la kwamba wananchi hawana elimu ya katiba ndo litakuwa ‘narrative’ ya CCM kukwepa kujadili hoja za katiba mpya.
Kwa nilichokisikia jana, ni dhahiri shahiri kwamba anayehitaji elimu ya kujua katiba ni nini, ni Rais Samia.
Samia hafai kuwa Rais. Alichaguliwa kuwa mgombea mwenza kwa sababu zingine na si kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye uwezo unaofaa.
Tuna Rais bomu ambaye hafai kuwepo madarakani hata kwa sekunde moja.
Nadiriki kusema kuwa Samia ndo Rais bomu kushinda marais wote tuliowahi kuwa nao Tanzania.
Najuta sana watz wanisamehe sana niliwahi kumshauri kitu kuhusu kuandika katiba na yeye anatekeleza ushauri ule Aiseh!
"Mheshimiwa Rais kuliko kusitisha mchakato wa katiba mpya,bora uendeleze pole pole Ili usikosane nao"
Sikumbuki vizuri ile tittle lakini ilisomeka hivyo,nikimwambia apige siasa pole pole HADI 2025 aseme muda hautoshi hivyo tufanye uchaguzi KWA hii iliyopo kwa marekebisho FULANI halafu mbeleni tutaendeleza!
SASA naona anafanyia KAZI ushauri ule!SASA sijui wale jamaa wenye mamlaka watamvumilia!!?
Maana walisema kabisa kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 usubiri HADI katiba mpya !!
Hao hao wamesema operation inaanza ile iliyositishwa yaani "original plan is on" yaani ile ya FDR!
Ngoja tuone!