Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Najuta sana watz wanisamehe sana niliwahi kumshauri kitu kuhusu kuandika katiba na yeye anatekeleza ushauri ule Aiseh!

"Mheshimiwa Rais kuliko kusitisha mchakato wa katiba mpya,bora uendeleze pole pole Ili usikosane nao"

Sikumbuki vizuri ile tittle lakini ilisomeka hivyo,nikimwambia apige siasa pole pole HADI 2025 aseme muda hautoshi hivyo tufanye uchaguzi KWA hii iliyopo kwa marekebisho FULANI halafu mbeleni tutaendeleza!

SASA naona anafanyia KAZI ushauri ule!SASA sijui wale jamaa wenye mamlaka watamvumilia!!?

Maana walisema kabisa kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 usubiri HADI katiba mpya !!

Hao hao wamesema operation inaanza ile iliyositishwa yaani "original plan is on" yaani ile ya FDR!

Ngoja tuone!
 
Huyu maza Kizimkazi hana akili
 
Kunwakati anajitoa ufahamu kama c katiba angekwepo alipo
 
Rais yuko sahihi kbs, amesema kinachohitajika si karatasi but the political will za viongozi. Kwamba pamoja na CDM kuwa na katiba nzuri lkn mbowe kabakia kuwa kiongozi wa milele yote.
 
Kama hakina umhimu basi na hiki tuachane nacho! Mbona teuzi mnatumia kanuni za kitabu mnachoona hakina maana sana ktk shughuli za kitafa?
 
Hapo samia yuko sawa kwani inaelekea wapinzani wanapewa agenda na nchi za magharibi kuyumbisha nchi zetu tu kwa faida yao.
 
Hana jipya huyo. WADANGANYIKA tumeibiwa bandari, wanyama kwenda zenji, hela za misaada kugawana pasu Kwa pasu wakati zenji na pemba ni kama ka wilaya tu, wabunge wao kulipwa mara 2, ardhi yao kwetu NO NO. Yaani kunyonywa, kuibiwa, kuburuzwa mtindo mmoja! Bila kusahau wakina Masai kunyang'anywa ardhi na kupewa waarabu!
Wacha niamie Burundi aisee..
🤬😤😡😠👺
 
Anasema kitabu hakina maana ila waliotaka asipewe uraisi kioindi kile alilia kilio hadi nje kilisikika kuwa kitabu kinakiukwa. Mpaka akamtaja pm kwa jina lake kuwa walitaka awe raisi wa mpito wakati katiba haisemi hivyo. Leo kaingi pale juu mara kawa mjuaji na machino!! Kweli madaraka ni ulevi kuliko bangi.
 
Huwa nasema siku zote maendeleo yanaletwa na kiongozi mwenye maono na mwenye kujua nini anafanya. JPM alikuja kuumbua sana watu, kwa katiba hii hii tunayosema mbovu alifanya mambo mazito yaliyowashinda wengine tena ndani ya muda mfupi. Alikomesha ujambazi, wezi na mafisadi. Alianzisha miradi mikubwa na kuitekeleza kwa kasi ya 4G. Wananchi wa kawaida wao hawana shida na katiba mpya watu wanataka kiongozi bora atayowatumikia wao na sio kuitumikia katiba. Hivyo vyama vihakikishe vinatuchagulia viongozi wenye sifa na uchungu na nchi wenye kusimamia ukweli kama alivyokuwa JPM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…