Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Tumepata habari rasmi kuwa kuna ujio wa ugeni mzito tika Marekani. Zaidi soma Makamu wa Rais Marekani, Kamala Harris kuitembelea Tanzania
Makamu wa Rais Marekani mama Kamara Harris anakuja ziara ya kiserikali nchini mwetu Tanzania.
Hii ni heshima kubwa kwa Tanzania.
Hapa nchini watakuwa wameisha fika marais watatu kwa kumbukumbu zangu, Rais Bush, Rais Obama na sasa Makamu Kamara Harris.
Ila kwa vuguvugu la huu ushetani unaoongozwa na serikali ya Marekani, hasa chama cha Democrats, kutetea ushoga, mimi binafsi natofautiana na Wamarekani.
Kwa sisi waafrika ushoga ni mwiko, haramu, chafu.
Naomba Mama Samia mkaribishe mama Kamara Harris ambaye tabasamu lake ni la kukata na shoka, nalipenda sana.
Lakini ushoga mwambie si sera ya CCM, wala CHADEMA, wala ACT.
Sera za ushoga mwambie zisije na Airforce Two.