Rais Samia: Nawashukuru wote mlionitakia heri ya kuzaliwa na siha njema

Rais Samia: Nawashukuru wote mlionitakia heri ya kuzaliwa na siha njema

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
"Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia neema ya kutimiza miaka 63. Nawashukuru nyote kwa salamu zenu nyingi za upendo katika siku hii. Ahsanteni sana kwa dua za siha njema, umri mrefu na utendaji bora, ninapoendelea na jukumu hili la kulitumikia Taifa letu kusonga mbele zaidi," Rais Samia.

20230127_230351.png
 
Hakika Mwenyezi MUNGU Aendelee Kumjalia Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania, Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kujivunia na kuiheshimu kwa Namna alivyojitoa na kujitolea kulitumikia Taifa letu kwa moyo wa uzalendo na upendo mkubwa Sana,Anastahili pongezi faraja na kutiwa moyo kwa kazi kubwa aifanyayo katika ujenzi wa Taifa letu
 
Madam Rais tunashukuru sana
Pia katusaidia kule kuteua wale wa juu kule chama kubwa la wafanyakazi
Katuondolea ugomvi
Mungu ni mwema tutaanza upya
 
Pia Kwa unyenyekevu tunashuuru umefanikisha ndoa ya zuhura yunis mana BBC hawakumuona bint Yako ,dadayetu ila viungani akaonekana
 
Wapi kaandika maneno hayo? Chawa mnamlisha mama maneno.
 
Hakika, kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu, muweza wa yote, azidi kumjalia afya njema na siku nyingi zenye heri.

Na katika uongozi wake, tunamwomba Mungu wetu amjalie ujasiri, uvumilivu na msimamo usioyumba katika mambo yote yaliyo ya haki na yenye heri kwa wananchi wote. Apuuze kila ushauri wenye dhamira mbaya iwe iliyo wazi ama iliyojificha.
 
"Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia neema ya kutimiza miaka 63. Nawashukuru nyote kwa salamu zenu nyingi za upendo katika siku hii. Ahsanteni sana kwa dua za siha njema, umri mrefu na utendaji bora, ninapoendelea na jukumu hili la kulitumikia Taifa letu kusonga mbele zaidi," Rais Samia.

View attachment 2497674
Tumesoma mahali eti yule toboatobo lema katabiri hufiki 2025.
Alaaniwe kabisa. Sisi tunakuombea dua njema ila 2025 utukabidhi wanamapinduzi ndani ya chama cha mapinduzi chama chetu.
 
Back
Top Bottom