Rais Samia: Nazunguka Ulimwengu Mzima Kutafuta Fedha Kuwawezesha wanawake Wa Afrika Wapate Nishati Bora ya Kupikia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa amesema ya kuwa ajenda ya nishati bora ya kupikia ni ajenda ya Afrika na ni ajenda ambayo ameianzisha yeye na yeye ndio champion katika kuchochea ajenda hiyo. Amesema ya kuwa anazunguka Ulimwenguni kwote kutafuta fedha kwa ajili ya kuwawezesha wanawake wa Afrika kupata nishati safi na bora ya kupikia.

Amesema ndio sababu hapa Nyumbani Tanzania serikali imefanya kazi kubwa sana katika suala zima la usambazaji wa umeme mpaka vijijini na kushuka kwenye vitongoji,ili kuhakikisha kuwa umeme unafika haraka haraka.

Amesema kuwa lengo ni kuachana na matumizi ya nishati ya kuni ambayo imeathiri mabibi zetu na Mama zetu kutokana na matumizi yake.lakini pia matumizi ya kuni yameathiri sana na kuchochea mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni za kupikia.

Rai yangu kwa watanzania ni kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa tunahamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia badala ya kutumia kuni na mkaa kupikia vitu ambavyo vimekuwa vikisababisha uteketezaji wa maelfu kwa maelfu ya miti kila Mwaka, na hivyo kuharibu mazingira na uoto wa asili.

Lakini pia kwa upande wa serikali ningependa kuishauri kuwa ifanye jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa nishati hizi safi na bora kwa ajili ya kupikia ,yaani umeme na gas vinapatikana kwa bei nzuri na ya chini ambayo hata mwananchi wa kule Isalalo wilayani Mbozi Mkoani Songwe ataweza kumudu gharama zake. Mfano kama mtungi mdogo ukajazwa kwa shilingi Elfu kumi au elfu 15 itavutia na kuwashawishi watu wengi sana kutumia nishati ya gas katika kupikia.

Kwa sababu ikiwa bei ya kujaza mitungi ya gas itakuwa juu,maana yake ni kuwa mwamko wa watu kutumia nishati safi kupikia nao utakuwa mdogo , hususani kwa watu wa vipato vya chini.na hivyo kukwamisha juhudi na ndoto za Mheshimiwa Rais kuona Taifa na wananchi wanatumia nishati safi na bora kupikia . Vile vile bei ya umeme kwa unit nayo ikipungua na kushuka maana yake watu watavutika wenyewe kutumia katika kupikia pasipo hata kutumia nguvu.

Kikubwa ni kuweka mazingira ambayo yatawashawishi na kuwahamasisha watu kutumia nishati safi badala ya kuni na mkaa. Na vishawishi hivyo ni kupunguza bei ya nishati hizi ambazo ni umeme na gas .bei iwe ni ile ambayo wengi watamudu kununua na kugharamia.

Kwa sababu hata ikitokea serikali ikawagawia watanzania wote mitungi ya gas bure kabisa nakuwajazia gas ya kuanzia .lakini bei ya kujaza mitungi hiyo ikawa juu bado utaona watanzania wengi wakirejea katika matumizi ya kuni na mkaa baada ya kuisha kwa gas ile ya bure waliyokuwa wamejaziwa awali. Hii ni kutokana na kushindwa kumudu gharama za kujaza mitungi ya gas tena au kununua umeme na kuutumia kupikia.
Screenshot_20240820-130839_1.jpg

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa amesema ya kuwa ajenda ya nishati bora ya kupikia ni ajenda ya Afrika na ni ajenda ambayo ameianzisha yeye na yeye ndio champion katika kuchochea ajenda hiyo. Amesema ya kuwa anazunguka Ulimwenguni kwote kutafuta fedha kwa ajili ya kuwawezesha wanawake wa Afrika kupata nishati safi na bora ya kupikia.

Amesema ndio sababu hapa Nyumbani Tanzania serikali imefanya kazi kubwa sana katika suala zima la usambazaji wa umeme mpaka vijijini na kushuka kwenye vitongoji,ili kuhakikisha kuwa umeme unafika haraka haraka.

Amesema kuwa lengo ni kuachana na matumizi ya nishati ya kuni ambayo imeathiri mabibi zetu na Mama zetu kutokana na matumizi yake.lakini pia matumizi ya kuni yameathiri sana na kuchochea mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni za kupikia.

Rai yangu kwa watanzania ni kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa tunahamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia badala ya kutumia kuni na mkaa kupikia vitu ambavyo vimekuwa vikisababisha uteketezaji wa maelfu kwa maelfu ya miti kila Mwaka, na hivyo kuharibu mazingira na uoto wa asili.

Lakini pia kwa upande wa serikali ningependa kuishauri kuwa ifanye jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa nishati hizi safi na bora kwa ajili ya kupikia ,yaani umeme na gas vinapatikana kwa bei nzuri na ya chini ambayo hata mwananchi wa kule Isalalo wilayani Mbozi Mkoani Songwe ataweza kumudu gharama zake. Mfano kama mtungi mdogo ukajazwa kwa shilingi Elfu kumi au elfu 15 itavutia na kuwashawishi watu wengi sana kutumia nishati ya gas katika kupikia.

Kwa sababu ikiwa bei ya kujaza mitungi ya gas itakuwa juu,maana yake ni kuwa mwamko wa watu kutumia nishati safi kupikia nao utakuwa mdogo , hususani kwa watu wa vipato vya chini.na hivyo kukwamisha juhudi na ndoto za Mheshimiwa Rais kuona Taifa na wananchi wanatumia nishati safi na bora kupikia . Vile vile bei ya umeme kwa unit nayo ikipungua na kushuka maana yake watu watavutika wenyewe kutumia katika kupikia pasipo hata kutumia nguvu.

Kikubwa ni kuweka mazingira ambayo yatawashawishi na kuwahamasisha watu kutumia nishati safi badala ya kuni na mkaa. Na vishawishi hivyo ni kupunguza bei ya nishati hizi ambazo ni umeme na gas .bei iwe ni ile ambayo wengi watamudu kununua na kugharamia.

Kwa sababu hata ikitokea serikali ikawagawia watanzania wote mitungi ya gas bure kabisa nakuwajazia gas ya kuanzia .lakini bei ya kujaza mitungi hiyo ikawa juu bado utaona watanzania wengi wakirejea katika matumizi ya kuni na mkaa baada ya kuisha kwa gas ile ya bure waliyokuwa wamejaziwa awali. Hii ni kutokana na kushindwa kumudu gharama za kujaza mitungi ya gas tena au kununua umeme na kuutumia kupikia.View attachment 3074836

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Unajipa kazi ngumu ambayo wala haikuhusu. Chema chajiuza kibaya chajitembeza. Mambo yaenda yakizidi kuharibika huko Northen Circuit wewe uko kwenye mapambio ya kikomedi hapa.
 
Mama yeye aseme tuu kwamba anapenda kula bata, aache mbambamba.
Bata wa wapi hao? Rais wetu mpendwa anafanya kazi kubwa sana .ndio maana unaona kila kitu kinaenda vizuri hapa nchini pasipo kukwama wala kusuasua .ukiona wawekezaji watalii wanamiminika na kufurika hapa nchini lazma ufahamu ni kazi ya mama hiyo.
 
Kila akidhurura, akirudi bandari na maziwa yake vimeuzwa. Kipindi iki ni Mlima Kilimanjaro na Mbuga za wanyama
 
Anazunguka kuuza Nchi yetu na siyo kuitafuta nishati safi.Tunakiongozi wa hovyo sana awamu hii
 
Ni heri akae kimya tu huenda akadhaniwa ana ..... Timamu kuliko kuongea ongea utumbo.
Hawezi kukaa mezani na mawaziri wake kupanga utilization ya gas asilimia akiwa hapa nchini?
 
Sote tunajua anazunguka kwa ajili ya masilahi yao wenyewe binafsi na watu wake wa karibu sio sisi watanzania! Anatafuta fedha ya nini wakati nishati mbadala ya gesi asilia ipo hapa hapa nchini kwa wingi?

Rais Samia aache kabisa kuhadaa watanzania. Rasilimali zote tunazo anakwenda kutembea kibakuli na kutuingiza katika madeni yatakayo gharimu vizazi vijavyo.

Bi mkubwa amefeli kabisa. 2025 arudi zake Kizimkazi akalee na kucheza na wajukuu zake.
 
Back
Top Bottom