Rais Samia ni kazi kwako kuwaacha au kuwaondoa ‘for the sake of the nation and the party’

Rais Samia ni kazi kwako kuwaacha au kuwaondoa ‘for the sake of the nation and the party’

Kodi halali ya Serikali lazima tulipe, tusitegemee kuonewa huruma kwenye mapato ya Serikali.
Kama yule mama anadaiwa Kodi ya billioni 3 halafu anataka kukwepa eti alipe milioni 150!!!
hili haliwezekani, Kodi halali lazima ilipwe.

Nasema wakwepa Kodi wa kubwa ni wafanyabiashara wakubwa hawa ndio wanaongoza kukwepa Kodi na kutoa rushwa kwa TRA
Ungetulia umsikilize huyu mama ungemuelewa, Kodi yake halali ni hyo 150m, hizo zingine ni wizi mkubwa! Jana wamempigia simu akachukue kontena zake, kwanini Jana na siyo siku zingine? TRA NI UOZO MKUBWA+MWIGULU
 
Simtetei mtu ila binafsi sioni kosa so Hakuna wa kuondoa na waondoke Kwa lipi? Kodi zote zimetungwa na Bunge ,hapo ni kubadili mechanism au approach ya kukusanya ila sio ishu ya Waziri hapo.
Sheria zenyewe ni wizi mtupu na dhulma
 
Hao Wafanyabiashara walimkataa Hadi Mkuu wa Mkoa walidai Rais huu ni utoto wa Nidhamu na kuyumbisha Nchi..

Rais atafanya kazi ngapi? Nini maana ya kuwa na wasaidizi?

Mwisho ndio maana katika mchango Fulani nilisema Kuna madai geguine mfano unaenda Polisi kumshitaki afisa wa TRA ,then wewe unakuja kugeuziwa kibao ,hii inatakiwa kuwa addressed..

Mojawapo ya njia za kutatua Hilo ni Kwa Mkuu wa Mkoa pamoja na maofisa wa TRA walau kuwa na mkutano mara 1 Kila baada ya miezi 3 kujadili kero na utatuzi wake,ikifanyika hivyo hatutafikia Kwa PM au Waziri..

Kama Kuna mambo ya kisera ndio Waziri anaweza kuja kutoa ufafanuzi au kuchukua kuyapeleka huko Baraza la Mawaziri Kwa hatua zaidi..
Ukiona watu wanamtaka mama maana yake hawasikikizwi! Nikuambie tu watanzania wetu tumechoka, TRA wamekuwa wezi wakubwa na rushwa mingi, acheni watu wagome
 
Ukiona watu wanamtaka mama maana yake hawasikikizwi! Nikuambie tu watanzania wetu tumechoka, TRA wamekuwa wezi wakubwa na rushwa mingi, acheni watu wagome
Basi Kuna mfumo mbovu sana wa uwajibikaji.
 
Ungetulia umsikilize huyu mama ungemuelewa, Kodi yake halali ni hyo 150m, hizo zingine ni wizi mkubwa! Jana wamempigia simu akachukue kontena zake, kwanini Jana na siyo siku zingine? TRA NI UOZO MKUBWA+MWIGULU
Huyo mama ndio mwizi, anataka kuiba Serikali mapato, eti anadai "tukae mezani tuzungumze"
Huyo mama ni mkwepa Kodi maarufu...anajulikana.

Ila Serikali isikubali kuhadaiwa na wafanyabiashara matapeli wakwepa Kodi
Iwe na msimamo vinginevyo ikiwachekea watu kama hao jua Serikali itavuna mabua.
 
Sasa anajikadiria Kodi mwenyewe eti alipe 150millioni!!!!!

Huyu ni mkwepaji mkubwa wa kulipa Kodi halali na anataka kutumia kichaka Cha mazungumzo haya, alipe anacho daiwa aache janjanjanja
Wewe unaona sawa kutakiwa kulipa 30 billions kwa Kontena 15 za Vitenge!?

Unafanya kazi TRA!?
 
Kwani wafanyakazi wa TRA wanakulaga kiapo? Wasingefanyaga haya
Una maana wakiapa ndio hawadai rushwa?
Viongozi wote wameapa tena kwa Bible na Misahafu ila wanaiba kila kukicha

Kuna watu hawamuogopi Mungu kabisa bali wanamkubali shetani kinyama
 
Nikuulize unafanya biashara ..?

TRA wanachukua VAT kwenye mtaji sio mapato. Hawaangalii tofauti ya revenue na profit bali annual income

Kama mimi nimefanya biashara ya 100 Million na nikapatq Faida ya 20 M kwa nini nilipe kodi kwenye 120 M badala ya 20 M ambayo ni profit..?
Asipokuelewa hapa basi atakuwa hana ubongo

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Kipekee nakushukuru kwa kuchukua hatua za dhati za kunusuru soko la kariakoo kwa kumtuma Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa. Kwa kweli amefanya kazi kubwa ya kunusuru uchumi wetu.

Pamoja na yote yaliyojadiliwa kuna kiu cha uwajibikaji. Imedhihirika baadhi ya watendaji wako wana uwezo mdogo na wengine ni wazembe na wenye zarau

Ni ombi letu na kama itakupendeza wachukulie hatua au wahamishe au wasimamishe kazi wote walioonekana ni kikwazo kwa wafanyabiashara na uchumi wetu. Na katika hili usiwaache kambare ukaondoa dagaa utakua haujafanya kitu.

Kwa macho yako umeona kiu cha wale ambao wanalalamikiwa ni kazi kwako kuwaondoa au kuendelea kuwafuga.

Nakukumbusha Mh. Jakaya alimuondoa Kalamagi, Nchimbi, Lowasa. Pia Chuma JPM aliwaondoa Kangi Lugola, Mwigulu, Simbachawene nk ili kuleta ustawi na kuonesha uwajibikaji kwa watanzania

Sasa kama hautakuwa na serikali ya uwajibikaji au hata kuhamisha watendaji na mawaziri au hata kuwaondoa basi madhara yatakayotokea ni juu yako na utawala wako.

Chukua hatua
Kuna mjumbe wa Tanga kasema watasoma albadiri na pia kamtaja Adam Malima kuwa alimsweka ndani kwa siku 10 baada ya kuripoti kwake kuwa kuna rushwa kwa watu wa TRA. Nadhani mama kayasikia yote yaliyosemwa kwenye huo mkutano, na hapo ni tone tu la machafu yanayoshamiri kila kukicha wasaidizi badala ya kumsaidia mheshimiwa raisi wamekuwa kikwazo, hata raisi akisema utawasikia ah hayo ni maneno ya wanasiasa tunasubiri waraka! nadhani leo watakuwa wamemsikia Waziri Mkuu kuhusu matamshi ambayo raisi,makamu wa raisi, raisi wa Zanzibar na waziri mkuu wakiagiza kufanyika jambo mambo ya hatujapata barua yakome.
 
Nikuulize unafanya biashara ..?

TRA wanachukua VAT kwenye mtaji sio mapato. Hawaangalii tofauti ya revenue na profit bali annual income

Kama mimi nimefanya biashara ya 100 Million na nikapatq Faida ya 20 M kwa nini nilipe kodi kwenye 120 M badala ya 20 M ambayo ni profit..?
Mkuu umenisemea niliwahi kumuuuliza afsa wa TRA kwanini unakata hela ya kuendesha biashara pamoja faida na kibaya ni kuwa mimi ni mtoa huduma na sio mfanya biashara halafu huu mchezo wa risiti kuwa ziandikwe Jina na tin no kwa kila matumizi ya mwenye VAT wakati huko ninakotoa huduma hata mashine ya EFD hawana, lakini tunachoambiwa eti sheria ndivyo zinavyosema na wao wanadai wanafuata sheria, sasa ndio nimeanza kuelewa udhaifu wa wanaopitisha sheria hizi ambao ni wabunge wetu, si ajabu wana PhD za kuwa promoter wa Diamond na wengine za uchumi wa tozo!
 
Sasa anajikadiria Kodi mwenyewe eti alipe 150millioni!!!!!

Huyu ni mkwepaji mkubwa wa kulipa Kodi halali na anataka kutumia kichaka Cha mazungumzo haya, alipe anacho daiwa aache janjanjanja
Alisema atoe 150m halafu wakae waangalie kodi halali alipe taratibu.

Wewe huoni tatizo? Ni kigezo gani kilisababisha B30 ikashuka mpaka B10? Unadhani kuna mtu anaweza risk B of money za mzigo kwenye mikono ya TRA sababu hataki kulipa kodi halali? Ukiona mtu kakuachia mzigo ujue hiyo kodi kaishindwa. Halafu ukumbuke tofauti na wapokea mishahara hawa wafanyabiashara wanakopa bank azungushe halafu hiyo pesa ndo TRA apate, Bandari wapate, mishahara ilipwe.

TUSIWASHAMBULIE TU, TUWASIKILIZE. W/MKUU YUPO SAHIHI SANA KUWASIKILIZA.
 
Mama kambeba mwingilu kwa kila aina ya mbeleko, lakini wapi! Yale yale ya jiwe na mwanawe, leo kaoga ya kuyaoga mbele ya kadamnasi huku East Africa na Dunia ikiwa inamtolea macho
 
Kipekee nakushukuru kwa kuchukua hatua za dhati za kunusuru soko la kariakoo kwa kumtuma Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa. Kwa kweli amefanya kazi kubwa ya kunusuru uchumi wetu.

Pamoja na yote yaliyojadiliwa kuna kiu cha uwajibikaji. Imedhihirika baadhi ya watendaji wako wana uwezo mdogo na wengine ni wazembe na wenye zarau

Ni ombi letu na kama itakupendeza wachukulie hatua au wahamishe au wasimamishe kazi wote walioonekana ni kikwazo kwa wafanyabiashara na uchumi wetu. Na katika hili usiwaache kambare ukaondoa dagaa utakua haujafanya kitu.

Kwa macho yako umeona kiu cha wale ambao wanalalamikiwa ni kazi kwako kuwaondoa au kuendelea kuwafuga.

Nakukumbusha Mh. Jakaya alimuondoa Kalamagi, Nchimbi, Lowasa. Pia Chuma JPM aliwaondoa Kangi Lugola, Mwigulu, Simbachawene nk ili kuleta ustawi na kuonesha uwajibikaji kwa watanzania

Sasa kama hautakuwa na serikali ya uwajibikaji au hata kuhamisha watendaji na mawaziri au hata kuwaondoa basi madhara yatakayotokea ni juu yako na utawala wako.

Chukua hatua
Hapa upo kwenye kampeni uijuayo mwenyewe.

Nchi hii imekuwa na wapuuzi wengi sana siku hizi.
 
Back
Top Bottom