Rais Samia ni miongoni mwa viongozi mashujaa na madhubuti sana barani Afrika

Rais Samia ni miongoni mwa viongozi mashujaa na madhubuti sana barani Afrika

Naunga mkono hoja
Karibu maktaba yangu ya Samia
P
P
Daah...! Naumia sana. Any way
 
Sote ni mashahidi kwamba,
Dr Samia Suluhu Hassan, alipokea nchi katika mazingira magumu ya kiuchumi katikati ya janga la COVID-19 na katika hali ya majonzi, masikitiko makubwa na huzuni ya kitaifa baada ya kufariki Rais hayati John Pombe Magufuli akiwa madarakani, na akatuvusha salama.

In fact haikua rahisi,
lakini katika ugumu huo na katika hatari zote za kiusalama, bado Dr.Samia Suluhu Hassan, alisinama imara na alithubutu kuipokea nchi katika mazingira hayo, akaidhibiti vizuri na akatuvusha salama katika jaribu lile zito lisilozoeleka.

Dr Samia Suluhu Hassan akaunda serikali na mara moja akaanza kazi ya kuliunganisha taifa na kuifungua nchi miongoni mwa mataifa ya ulimwengu, baada ya dhiplomasia ya Tanzania dhidi ya mataifa ya ulimwengu kuzorota kidogo.

Katika uongozi wake Dr Samia Suluhu Hassan tangu ashike hatamu,
zilianzishwa kampeni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zilizolenga kuidhoofisha nchi na serikali yake, lakini bado Dr.Samia Suluhu Hassan alisinama imara kama kiongozi mzalendo na kuivusha nchi katika yote hayo salama.

Ushujaa na umadhubuti wa Dr. Samia Suluhu Hassan ulidhihirika wazi zaidi kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa 2025, ambapo zaidi ya 90% ya wananchi wapiga kura wa Tanzania walimchagua na kumuidhinisha kwa kishindo kikuu, kua mkuu wa nchi na Rais wa Tanzania kwa muhula wa pili mfululizo.

Dr.Samia Suluhu Hassan kubadili serikali yake ngazi ya taifa katika kipindi cha chini ya mwaka mwaka baada ya uchaguzi mkuu, ni kielelezo tosha cha ushujaa wa kipekee sana na umadhubuti wa Rais huyu mwanamke barani Africa, kinachomfanya kua miongoni mwa Marais wenye nguvu zaidi Africa na dunia nzima.

Una maoni gani.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Screenshot_20260902-120602~2.png
 
Back
Top Bottom