Rais Samia ni mkombozi au tunafumbwa macho?

Rais Samia ni mkombozi au tunafumbwa macho?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
372
Reaction score
310
Wanabodi,

Nchi za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zilipata maafa makubwa sana baada ya vita vikuu vya pili vya dunia. Katika kipindi hicho ambacho Umoja wa Mataifa uliundwa, mpango wa kuzisaidia nchi hizi uliandaliwa. Hiki ndicho kipindi ambacho misaada na mikopo ilitumiwa kwa mara ya kwanza kwa madhumuni ya kuzikwamua nchi hizo kutoka kwenye hali waliyokuwa nayo katika kipindi hicho. Kwa haraka haraka, ni rahisi sana kwa yeyote kuona mafanikio ya nchi hizi katika uwezo wao wa kutumia rasilimali hii kwa manufaa yao.

Miaka kadhaa baadaye, iliaminika kwamba mafanikio ya mradi wa kwanza uliojumuisha nchi hizo za ulaya ungeweza kuleta manufaa hayo hayo kwa nchi za Afrika. Hili halikuwa kweli na badala yake ufisadi ulizidi, madeni yaliongezeka na mwisho wake, nchi za Afrika zilizidi kuwa masikini.

Sio sahihi kuona kwamba serikali inaelekeza nguvu kazi zaidi kwenye ujenzi wa miundombinu na vitu vingine huku tukimpongeza Rais na kusahau changamoto ambazo mwananchi wa kawaida anapitia kila siku. Takwimu za hapa na pale kuhusu maendeleo ya nchi au uendeshwaji wa serikali zimekuwa za kawaida bila kuwa na uhalisia wa hali ya mitaani.

Je, Rais Samia anaweza kuorodhesha mikakati yake ya kukabiliana na changamoto hii?. Kama Tanzania ilivyoingia kwenye nchi zenye uchumi wa kati, kuna mipango ipi ya kuhakikisha kwamba mafanikio ya serikali yanawafikia wananchi? Labda miradi mbali mbali ya Benki kuu kuweza kuongeza mzunguko wa hela na kuwafikia vijana, labda uboreshwaji wa VETA, labda kilimo cha kisasa, ni njia ipi inayotumiwa na serikali kukugusa wewe moja kwa moja?
 
Mkombozi anayezunguka duniani kutafuta wawekezaji na watalii huku akiwatishia kuwa nchini kwake kuna ugaidi na magaidi ya nchini kwake ni hatari sana kwani kwa shilingi 600'000 tu na bastola moja yenye risasi tatu wangefanya nchi isitawalike.

Yangekata miti yote barabarani kuanzia Morogoro hadi Mbeya.
 
Hoja nzuri, ila uandishi sio mzuri, hebu jaribu kuweka paragraph, itapendeza na kumvutia msomaji pongezi zako kwa mada nzuri
 
Back
Top Bottom