Rais Samia ni mpango wa Mungu kuwavusha Watanzania

Rais Samia ni mpango wa Mungu kuwavusha Watanzania

mapessa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
664
Reaction score
1,168
Tazama ni siku nyingi zimepita miongo na karne zimebadilika toka Uhuru Hadi hapa tulipo.

Mvua ya Chama kimoja hadi Mvua za Demokrasia tumekutana na masika za Utawala bora neema ya kuijenga nchi.

Tangu Awamu ya Mwl. Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa ni Mhe Samia Suluhu Hassan.

Awamu zote zimegawanyika kimamlaka na utendaji wake hata kutofautiana kifikra pamoja na kimtazamo kwa namna ya kuijenga Tanzania.

Sitaki kuwa Mwalimu wa awamu zilizopita nataka kusimama katika awamu ya sita awamu tuliyopo na tunayoishi kwasasa.

Hatuwezi kuikataka asili yetu abadani ila mifumo ya jambo lolote jipya linaegemea kwa kuchota asili zetu zilizopita. Mwalimu Nyerere alikuwa na falsafa ya Kujisahihisha.

Ni Wakati wa Kujisahihisha Na historia mpya...!!

Tangu alipokamata madaraka mapema mwezi Machi Mwaka huu Mhe. Samia Suluhu hassan amesimama kama alama ya historia mpya katika siasa za Afrika mashariki.

Mosi kuwa Mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Urais katika ukanda huu wa Afrika mashariki vizazi vingi vina la kujifunza na somo kubwa la usawa wa kijinsia Tanzania inakuwa imelifikia.

Uhuru wa kuheshimu Katiba hii ni historia kubwa ambayo inaandikwa ndani ya Tanzania kwani Rais Samia ameyachukua madaraka kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Aliyefariki Dunia machi 7, 2021.

Sifa hizi mbili hazitoshi kumpambanua Rais Samia Suluhu Hassan bali kuna sifa anuai zenye kumtofautisha Rais Samia na Marais wengine waliopita hapa ndipo tunaandika jina lake kwa kalamu ya dhahabu.

Rais Samia Suluhu Hassan amewiva kiitikadi amepikwa amehitimu na itikadi na amefuzu falsafa ya uliberali wa Jamii na uchumi ambaye anaamini ni wajibu wa serikali kuinua hali za Maisha ya Wananchi kwa kuwapatia Wananchi uhuru wa kuendeleza shughuli zao bila kuingiliwa na serikali, umiliki wa mali binafsi; Serikali kurekebisha Uchumi au kuratibu. Kutokuingilia uhuru wa Biashara na ushindani katika soko.

Hili limeonekana wazi baada ya serikali ya awamu ya sita kuelekeza kuwa tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali kwenye bidhaa za mafuta kupunguzwa ili kuwapa unafuu wananchi

Baadhi ya Taasisi zilizoguswa na maelekezo hayo ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Tozo ya udhibiti), Mamlaka ya Bandari (Tozo ya miundombinu) na Mamlaka ya Mapato (Tozo ya kuchakata taarifa)

Rais Samia amechukua hatua hiyo kukabiliana na upandaji wa bei za mafuta katika Soko la Dunia, hali ambayo imekuwa ikiathiri watumiaji hapa Nchini.

Mfano huu ni wazi ulio dhahiri kuwa Serikali ya Rais Samia inaunga mkono sera za kuondoa ukiritimba binafsi kwa kuwa ukiritimba unaumiza Wananchi maskini.

Rais Samia ni muumini wa ongezeko la kodi linaloendana sambamba na ukuaji wa vipato vya wananchi vitokanavyo na shughuli halali za uchumi wa Wananchi.

Rais Samia mara tu baada ya kuingia madarakani alinukuliwa akisema kuwa hataki ukusanyaji wa kodi kwa mabavuu, na kwa mantiki hiyo serikali ilifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 5.151, ikiwa ni asilimia 94 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 5.462.ambacho hakijawahi kufikiwa kwa miaka mitano iliyopita kwenye kipindi hicho pasi na kutumia mabavu. Kwa hili Rais anastahili pongezi kwani huu ni mwanzo mzuri ambao unaochochea watu wengi zaidi kulipa kodi kwa hiari.

Rais Samia ni Kiongozi anayesimamia sheria haki, kanuni na utaratibu bila uwoga wala ubaguzi.

Sifa kubwa kwa Rais Samia ni mtu wa kufuatilia jambo mpaka matokeo chanya yapatikane. Kwa kipindi cha miezi sita Rais ameweza kutatua kero 11 ndani ya Muungano ameishi ndani ya Muungano amefahamu Changamoto zote zilizopo ndani ya Muungano na kuzifanyia kazi kwa haraka zaidi.

Ametoa mtihani mkubwa kwa Waziri wa Tamisemi kuhakikisha shilingi Trilioni 1.3 zinaleta matokeo. Kwenye hili haya Mhe. Rais amehaidi kuionyesha Rangi yake kamili kwa watendaji wa hovyo na wabadhirifu na huu ni mtihani mkubwa kwa Baraza la Mawaziri ambao ndio askari wa mwamvuli wanaotakiwa kuhakikisha shilingi trilioni 1.3 zinaleta matokeo.

Kwa Mara ya kwanza tangu Uhuru wa nchi yetu mikopo imekuwa ikitolewa katika tarakimu tu bila kuwekwa matumizi yake huku deni la Taifa likizidi kupaa zaidi.

Samia ni wa tofauti vizazi mtamsoma miaka mingi zaidi kwa jina lake na sifa zake kwa utendaji wake uliotukuka!
 
Tazama ni siku nyingi zimepita miongo na karne zimebadilika toka Uhuru Hadi hapa tulipo. Mvua ya Chama kimoja hadi Mvua za Demokrasia tumekutana na masika za Utawala bora neema ya kuijenga nchi. Tangu Awamu ya Mwl. Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa ni Mhe Samia Suluhu Hassan.
Awamu zote zimegawanyika kimamlaka na utendaji wake hata kutofautiana kifikra pamoja na kimtazamo kwa namna ya kuijenga Tanzania.

Utakosa vinasaba na bwana Mahela kweli wewe kwa mtaji huu?

IMG_20211019_214417_996.jpg

Miaka 8 ya kazi!

Hiiiiii bagosha 😁😁!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tazama ni siku nyingi zimepita miongo na karne zimebadilika toka Uhuru Hadi hapa tulipo. Mvua ya Chama kimoja hadi Mvua za Demokrasia tumekutana na masika za Utawala bora neema ya kuijenga nchi. Tangu Awamu ya Mwl. Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa ni Mhe Samia Suluhu Hassan.
Awamu zote zimegawanyika kimamlaka na utendaji wake hata kutofautiana kifikra pamoja na kimtazamo kwa namna ya kuijenga Tanzania.
Uteuzi umeshakupita.Ulikuwa wPi ukachelewa.
 
Hii Aibu Mpaka Mwaka Gani
Wakati Wa Jiwe Haijapata Kutokea
Awamu Ya Sita Mnasema Haijawahi Kutokea

Haa Teh

Acheni Kutumika Hadharani, Vice President Kaenda Kwenye Bwawa Kasema Wazi Mradi Upo Nyuma Ya Muda
Mkandarasi Hana Uzoefu, Lakini Zamani Mlisema Upo Sawa
 
Tazama ni siku nyingi zimepita miongo na karne zimebadilika toka Uhuru Hadi hapa tulipo. Mvua ya Chama kimoja hadi Mvua za Demokrasia tumekutana na masika za Utawala bora neema ya kuijenga nchi. Tangu Awamu ya Mwl. Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa ni Mhe Samia Suluhu Hassan.
Ninaona kasi ya kumpumbaza rais kwa sifa za kijinga inaongezeka kila siku na huwezi kushindwa kuona anakwenda kuangukia wapi. Muulizeni Magufuli.
 
Tazama ni siku nyingi zimepita miongo na karne zimebadilika toka Uhuru Hadi hapa tulipo. Mvua ya Chama kimoja hadi Mvua za Demokrasia tumekutana na masika za Utawala bora neema ya kuijenga nchi. Tangu Awamu ya Mwl. Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa ni Mhe Samia Suluhu Hassan.
Awamu zote zimegawanyika kimamlaka na utendaji wake hata kutofautiana kifikra pamoja na kimtazamo kwa namna ya kuijenga Tanzania.
Sitaki
201101q.jpg
 
Hii Aibu Mpaka Mwaka Gani
Wakati Wa Jiwe Haijapata Kutokea
Awamu Ya Sita Mnasema Haijawahi Kutokea

Haa Teh

Acheni Kutumika Hadharani, Vice President Kaenda Kwenye Bwawa Kasema Wazi Mradi Upo Nyuma Ya Muda
Mkandarasi Hana Uzoefu, Lakini Zamani Mlisema Upo Sawa
2935090_IMG-20210717-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom