Mkuu
brazaj , kwa vile YEYE huzungumza kupitia watu tofauti tofauti, nao wakiambiwa kitu wanasema na mimi ninachoambiwa nasema, mwisho wa siku, ni wakati muafaka ukifika YEYE husema, na mtu usipo sikia, kisha yeye kutenda!.
Kwenye urais wa Samia, hakuna mtu yoyote alijua kuwa kuna siku rais wa JMT anaweza kufa akiwa madarakani!, hivyo siku zote Makamo wa rais alikuwa anateuliwa tuu bila kumhesabia anaweza kuja kuwa rais wa JMT kwasababu hakuna mtu aliyewahi kufikiri kuwa rais wa JMT anaweza kufa madarakani!, hivyo ma VP wetu tulikuwa tunajiteulia tuu kwa hoja ya yeyote ili mradi rais ukitoka upande mmoja wa JMT, VP atoke upande wa pili.
Hivyo naamini hata wakati Samia ni VP wa JPM, hakuna siku aliwahi kuwaza kuwa kuna siku JPM anaweza kuchomoka kwa kuitwa kwa Baba yake na yeye kuwa rais wa JMT!, hivyo ilivyotokea JPM akaitwa kwa Baba yake na Samia akawa rais, watu wote wanajua imetokea tuu!, kumbe kiukweli hakuna kitu chochote chini ya mbingu kinacho tokea tuu, kila kinachotokea ni kilipangwa na kutokea kwake ni mipango ya Mungu!.
Pamoja na kila kinachotokea ni mpango wa Mungu, lakini kuna watu walitoa "kauli umba " zenye nguvu ya uumbaji ndani yake, zilizo muumbia huo urais wa JMT kwa kauli hizo kumuomba Mungu, wakamuumbia urais wa JMT ili Samia awe rais na kweli Mungu akasikia hizo kauli, zikamuumbia Samia urais wa JMT hivyo ninavyo annika hapa, usikute hata Samia mwenyewe hajui imekuwaje kuweje mara ghafla yeye sasa ni rais wa JMT!, anajihesabu amekuwa rais wa JMT kwa kudra tuu za Mwenyeenzi Mungu, yaani kwake ni kama imetokea tuu akawa ni yeye!, kumbe hajui sio imetokea tuu kwa kudra tuu za Mwenyeezi Mungu, it's a premeditated events, kuna watu waliumba kwa kaul umba, na kauli umba hizo zikaumba na kutokea kilichomtokea!.
Kwanza anza kwa kuangalia ni lini watu wa kauli umba, walianza kumspot Mama Samia, na kumuumbia kauli umba!. Angalia hili bandiko ni la lini?
New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!.
Bandiko hili ni la 2010, angalia hiyo 2010 tulisema nini kumhusu Samia, na nini kilikuja kutokea... mkiambiwa baadhi ya kauli zinaumba, mjue ni kweli kauli huumba!.
Kisha 2015
Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?
Kauli Umba ya kuunda VP mwananke kwa Tanzania
Tanzania ilipata VP, mwanamke kwa mara ya kwanza, baada ya uchaguzi wa 2015, kuna wengi wanadhani ilijitokea tuu, Tanzania kuwa na VP mwanamke!, hawajui kuwa huo u VP wa mwanamke, kuna watu wenye kauli zenye powers za kuumba, walitoa kauli umba za kutaka tupate VP mwanamke, toka Machi 8, 2015!.
Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
Hii ni kauli umba ya kumuumbia mtu urais wa JMT.
na hili
"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Angalia kwa makini hii kauli umba hapa iliumba nini?
Hapa kuna mtu ameumbiwa urais wa JMT kwa kauli tuu!.
Naamini kama JPM angesoma hapa, halafu akaamua tangu ile ile ,2020 angempisha Samia, you never know by now labda...
Baada ya Samia kuwa rais wetu, sasa focus ni 2025, jee ataendelea...
Kwanza tumeanza na kauli umba ya wish
Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Kisha
Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Not a word more, not a word less!.
P