Rais Samia ni mtu makini sana

Rais Samia ni mtu makini sana

lukala

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Posts
594
Reaction score
590
Kwanza kabisa ni declare my interest, nimekuwa muumini sana na siasa za Mh, Jakaya Kikwete pamoja Ally Hassan Mwinyi.

Twende kwenye point yangu ya msingi, huyu mama ana siasa za kiustaarabu sana kama alivyopitia mzee wetu Jakaya Mrisho ni watu wanaoangalia misingi ya binadamu sana. Mfano Leo hatusikii kulundana ndani hovyo hovyo au kudharalishwa watumishi kwenye majukwaa au kutishiwa kutumbuliwa.

Kwenye uchumi pia naona anaendelea vizuri kwa kuendelea kureform na kurebuild tena uchumi ulioharibiwa. Mfano kati ya mwaka2010-2015 uchumi wa mtu umoja umoja ulikuwa mkubwa sana kulinganisha na 2017_siasa. Hii ilionyesha kwenye uwekeza watanzania, mfano ujenzi wa nyumba bora na za kisasa lakini pia uwekezaji wa mashambani nao ulikuwa mkubwa sana.

Nchi ilienda vizuri kwenye kilimo mfano mahindi mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Songwe, Rukwa na Sumbawanga. Korosho mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi ilipelekea sana kuboresha maendeleo ya watu. Lakini kuanzia 2017 hayo mambo yaliharibika had I sasa tunaona mama anajaribu kutuletea wanunuzi was mazao hayo. Tayari mikoa hiyo imeanza kunufaika tena mfano bei Mahindi, Ufuta, Mbaazi, na nk.

Kwenye ajira naona pia amejitahidi licha ya muda mfupi, watumishi was serikali kaongezea mshahara , kapandisha madaraja lkn pia katangaza ajira tofauti na awamu iliyopita.

Changamoto aliyokuwa NATO mama hana watu was propaganda kama mwenzake alivyofanya , hata akifanya kitu kidgo walikuwa wanampamba huyu hawapo. Tumpe muda
 
Kuhusu kilimo ungekaa kimya tu, watu sasa wananunua mbolea kwa bei zaidi ya Mara 3 kwa sababu za kijinga tu. Mfuko kutoka 50000 hadi 150000. Sasa hapo utafaanya propaganda gani ikiwa watu uhalisia wanauona?
 
Back
Top Bottom