Rais Samia ni Rais bora kuwahi kutokea kwenye Taifa hili


Hivi kijana una timamu kweli wewe..!? Au ndio pangu pakavu tia mchuzii.!? Bata Waheed.
 


1. Amani na utulivu upi wakati kuna watu wanatekwa mchana kweupe na kuchinjwa na hatujui sababu na wakipata hizo ripoti hatuoni walishitakiwa
2. Ruto kwa mfano mwenzake wa Kenya kwenye nyakati hizo kashapata mikaba kwa vijana ya kazi ya muda ujerumani zaidi ya 200,000 na USA zaidi ya 300,000 je Mama kazi za vijana ni zipi hasa kazileta?
3. Uandikishaji wa wapiga kura wa serikali za mitaa ni aibu umetawaliwa na uchama na uchawa na sio utaifa. Sina sababu ya kusema zaidi wakajibu hoja za Lema kama ni za uongo leteni ushahidi hapa
4. Katiba mpya na chakato ambayo aliahidi mpaka leo iko wapi??

Raisi Samia kitu pekee cha kusifiwa ambacho kakifanya ni kuongeza watalii nchini amechangia na kufanya vizuri kwenye hili. Mengine yote tusimsingizie haitaji pongezi badala yake anahitaji kuhimizwa afanye vizuri zaidi. Kikubwa wa Mama aangalie sana washauri wake hasa wa kisiasa na kiusalama. Pili Mama aache kuwa muongo kama Raisi ukisema kitu kwa jamii kifanyike na utangaze kwa jamii. Umedanganya kuhusu ripoti ya haraka ya mauaji, mikutano na Mbowe kumbe ulikuwa una tapeli. Lakini Mama ni hajaridhika na pesa mtoto na mkwe wako wanajaa tamaa za biashara sana badilika Mama
 
Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi,asomaye na aelewe.😉
 
Ripoti ya utekaji na mauaji hadi sasa bado lakini, hiyo ni sifa nyingine, ufisadi wa kila mwenye nafasi kula kwa urefu wa kamba yake. Ripoti ya CAG ina wizi wa ajabu wa mali ya umma na hawajachuliwa hatua ionekane. Labda kama hivyo ni VIJIDRAMA tu.
Na ndiyo ubora wenyewe anaouelezea mleta uzi huu.
 
kwakweli ameliunganisha taifa, na kuifungua nchi miongoni mwa mataifa ya ulimwengu,

anapendwa mno na waTanzania kila pembe ya nchi, anakubalika sana nchini na anaaminika mno kutaifa na kumataifa kutokana na nia na dhamira yake njema katika kuchochea mageuzi na kuwaletea waTanzania maendeleo endelevu kisiasa, kijamii na kiuchumi, ndani ya kipindi kifupi sana cha yongozi wake..

God bless Dr.Samia Suluhu Hassan
 
Mwanzoni nilikuwa sijakuelewa ila mwisho hapo sentensi hiyo imebeba maana nzima ya andiko..
 
Aaa yuu siriazi?
 
 
Mnatuvuruga sasa.
Nani bora, maana tukianza kumsifia Nyerere mnasema Kikwete ndio bora.
Tynaanza kwenda na Kikwete mnapiga u-turn kutuambia Magufuli balaa.
Tunavuta kiti tujiandae kumpigia makofi Magufuli ghafla tuko kwa mama.
Mnatuchosha, nchi haina tena vijana wa kujenga hoja na kukosoa. Kila mmoja anapigania ugali wake wala hajali kesho ya watanzania wenzake itakuwa chini ya mikono ya nani.
 
Nami naunga mkono hoja
 
Mtaani hela hakuna kabisa.

Watu wanaulizana tu huko kwenu hali ikoje.

Hakuna mwenye majibu.

Ila mkuu kama wewe umekamata chanel Well and good.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…