Rais Samia: Nilimwondoa Kidata TRA sababu niliona mwishoni atadata

Kwani kuna shida gani katika maneno hayo? Na je reality ni ipi? Kwani hizo tekniki alizozisema hazipo?

Au kwani wewe hufahamu mtu yeyote anayefanya kazi TRA au ndugu au jirani? Kuna unayemuona ni maskini?

Wanaposema wanataka mtu mwenye experience ya miaka kadhaa kwenye kazi na uzoefu fulani unadhani wanamaanisha uzoefu gani?

Nenda interview za madreva wa mabasi ya mikoani, unadnani kama hujawahi kuangusha gari au kugongana ndiyo utapata kazi kirahisi ? Hakuna mwenye biashara ya basi atakayetaka ukajifunzie kwake kuangusha basi.

Yusuf Juma Mwenda atapewa malengo ya kuvuka makusanyo ya kodi zaidi ya alivyofanya Kidata. Na kwa kuwa anajuwa wanavyoiba na kukwepa basi ndiye mtu sahihi. Kama hatatumia uzoefu wake, basi atampisha mtu mwingine
Hao punguani lengo lao ni kupotosha na Kwa kuwa wanamchukia Samia basi watatafuta Kila maneno.

Hao ndio wafanyabiashara wakigoma wanaunga mkono, Serikali ikiwabana wanalalamika eti Kodi kubwa,ikiwapa.shushu wanasema Samia hawezi yaani ilimradi waridhishe kijiba Cha roho zao.

View: https://twitter.com/MwananchiNews/status/1809244084726280593?t=OyxMP-Vd9bCm6qwdpOVT0A&s=19
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema amemuondoa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata kwenye nafasi yake kwakuwa aliona atadata kwa jinsi anavyoandamwa lakini amekiri kuwa TRA chini ya Kidata imefanya vizuri na kuongeza mapato hadi kufikia Tsh. trilioni 27.64, ambayo ni sawa na ufanisi wa 97.67% ya lengo la kukusanya Tsh. trilioni 28.30 katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/24 ambalo ni ongezeko la 14.50% ikilinganishwa na makusanyo ya Tsh. trilioni 24.14 katika Mwaka wa Fedha uliopita, 2022/23.

Akiongea leo July 05,2024, Ikulu ya Tunguu, Zanzibar wakati akiwaapisha Viongozi Wateule, Rais Samia amesema “Yusuph Mwenda kwanza hongera kwa kazi nzuri uliyofanya Zanzibar, tunakupeleka TRA (kuwa Kamishna mpya), TRA chini ya Kidata imefanya vizuri sana, mapato yamekua sana, sitegemei kama utashuka, kwanini nimemuondoa Kidata?, Kidata nimemuondoa niliona mwisho atadata, kazi kafanya nzuri sana lakini niliona atadata jinsi anavyoandamwa , sasa nakupeleka wewe Kijana wa Dar es salaam
Mtoto wa Mjini, uhuni wote ulioko TRA kule umefanywa na wewe ukiwa mulemule pengine uli-participate”

“Mipango yote mule ya kupenya, ya kufanyaje na Bandari mnatoa wapi mnapenyeza wapi unaijua Yusuph nenda kaizibe, nenda kaizibe, tunachohitaji ni mapato, tunachohitaji ni kupungua kukopa, tunakopa tunajichetua kila anayekuja akija European Bank yes yes, akija huyu Yes, World Bank wanatunyanyasa tumo tu, nini?, tuna miradi ya maendeleo inataka pesa, pesa hatuna tunakopa, tunakopa tunanyanyasika, je tukiwaomba itakuwaje?, kwahiyo twende tukanyanyue za kwetu”

“Serikali imefanya yote, tumeweka mazingira mazuri ya kufanya biashara, mazingira mazuri ya kufanya uwekezaji, Wawekezaji wanakuja, biashara zinafanyika kodi hazilipwi, Kariakoo pale tatizo ni kulipa kodi ukienda leo wanakuambia hiki kesho wanakuambia hiki, Kariakoo pekee yake kuna mapato kama yatakusanywa vizuri kwa mwaka yanaendesha Wizara tatu lakini hamkusanyi kuingia Serikalini, inawezekana mnakusanya kuingia mfukoni lakini hamkusanyi kuingiza Serikalini nenda kazibe hilo”

“Mwenda unaijua vizuri TRA ulikuwa sijui Mkurugenzi wa kodi zipi lakini ulikuwa unajua mnaibia vipi na wenzio kwahiyo yale mliokuwa mkiiba vichochoro vile nenda kazibe tunahitaji fedha, nimekuamini na najua utakwenda kufanya kazi”

#MillardAyoUPDATES

NB: Kiukweli 2025 tugangamale vingine tutakuja kuwa Zimbambwe iliyochangamka.
 
Huyu mama anacheka Na nyani, tuttavuna mabua
 
Wanateuana hata kama wamedata na hata kama wanahusika na michongo watoto wa mjini hawaachani.

Amemrudisha tena huku akimtuhumu kwamba huenda anashiriki kwenye michongo ya watoto wa Mjini.

Ccm ina wenyewe.

Wanaoendelea kupiga makofi na vigelegele endeleeni.
 
  • Thanks
Reactions: I M
Kwani kuna shida gani katika maneno hayo? Na je reality ni ipi? Kwani hizo tekniki alizozisema hazipo?

Au kwani wewe hufahamu mtu yeyote anayefanya kazi TRA au ndugu au jirani? Kuna unayemuona ni maskini?

Wanaposema wanataka mtu mwenye experience ya miaka kadhaa kwenye kazi na uzoefu fulani unadhani wanamaanisha uzoefu gani?

Nenda interview za madreva wa mabasi ya mikoani, unadnani kama hujawahi kuangusha gari au kugongana ndiyo utapata kazi kirahisi ? Hakuna mwenye biashara ya basi atakayetaka ukajifunzie kwake kuangusha basi.

Yusuf Juma Mwenda atapewa malengo ya kuvuka makusanyo ya kodi zaidi ya alivyofanya Kidata. Na kwa kuwa anajuwa wanavyoiba na kukwepa basi ndiye mtu sahihi. Kama hatatumia uzoefu wake, basi atampisha mtu mwingine
Aisee... huoni shida hapo?!

Mimi nimeona shida sekunde ya kwanza tu nilipoanza kumsoma, anamtoa Kidata TRA anayekiri kafanya vizuri eti kwasababu "atadata"!

Kwa hiyo sababu nyepesi aliyoitoa, nimeamini maneno ya wale waliosema anamuondoa Kidata kwasababu Abdul anataka mtu mwepesi ili am-control vizuri zaidi.

Hapo badala ya kumpeleka huyo Yusuph kuongeza mapato ya taifa, amempeleka kuongeza pato la familia yake kupitia mwanae.

Samia anatulaghai!.
 
Nyerere na hii ccm, ulituweza babu 🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌
Nyerere alikuwa mwadilifu mno mzee yule. Mpaka leo anachekwa pamoja na watoto wake ambao aliwaacha "hawana kitu". Sijui yeye alishindwa nini kumteua Dullah mmoja akaitajirisha familia. Babu yule alikuwa na matatizo yake ila hili la ufisadi hapana!

CCM iliachana na Nyerere rasmi ilipoamua kuachana na Azimio la Arusha na kuja na lile la Zanzibar. Ni mtoto aliyeasi!
 
Back
Top Bottom