ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Rais Samia amefurahishwa na kuendelea kuhimiza jamii ya Watanzania Kuunga mkono juhudi alizozianzisha za Matumizi ya Nishati Safi.
Akizungumza huko Namtumbo wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Samia,amesema alibuni mradi huo baada ya kuona wanawake wanapata upofu na vifo kutokana na matumizi ya Kuni na mkaa.
Aidha anasema Mpango huo inalenga Kuokoa amazingira. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Samia amesema malengo ya serikali ni kuona asilimia 80 ya wananchi wawe wakitumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030, miaka takribani sita ijayo.
Ili kufikia malengo hayo, Rais Samia amesema wameanza na taasisi za elimu pamoja na taasisi nyingine kubwa kubwa (kama magereza) kutumia nishati safi ya kupikia na baadaye itaenea kwingine.
Swali.
Hivi Kuna Rais mwingine yeyote waTanzania Baada ya Nyerere ambae amewahi buni programu ikawa ajenda ya Afrika.?
Hongera Rais Samia Kwa Maono Yako mema.Mnaweza kusoma hapa pia Rais Samia afanikisha kupatikana Kwa TSHS.Trilioni 6 za Nishati ya Kupikia. Rais wa Benki ya AfDB Asema ni Kiongozi wa Mfano
Soma zaidi hapa Rais Samia kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano wa Kimataifa Kujadili Nishati Safi utakaofanyika Ufaransa
---
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko amesema Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kunakuwa na unafuu katika upatikanaji wa bidhaa za Nishati Safi ya kupikia ili kumwezesha kila mwananchi kutumia nishati iliyo safi na salama.
Dkt. Biteko amesema hayo tarehe 13 Septemba 2024 Jijini Dodoma wakati wa hafla ya Kusaini mikataba ya ushirikiano ya utekelezaji wa Nishati Safi ya Kupikia yenye thamani ya shilingi bilioni 50.98 kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Jeshi la Magereza, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Wasambazaji wa Gesi ya kupikia, hafla ambayo ilienda sambamba na uzinduzi wa jengo la REA.
“Namshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake yanayowezesha Sekta ya Nishati kuendeshwa kwa mafanikio ambayo yamepelekea leo hii tushuhudie hatua ikizidi kupigwa katika kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia unaolenga kuokoa maisha ya watanzania na pia kuiwezesha Wizara ya Nishati kutatua changamoto zinazojitokeza lengo likiwa ni kutoa huduma iliyo bora kwa wananchi," amesema Dkt. Biteko
Akizungumzia usambazaji wa nishati vijijini ikiwemo umeme, Dkt. Biteko ameipongeza Bodi na Menejimenti ya REA kwa kusimamia ipasavyo miradi na kwa kuwahimiza wakandarasi kukamilisha kazi kwa wakati.
"Nawapongeza sana Bodi ya REA; mnafanya kazi nzuri, nimekuwa nikiwaona mara kwa mara mkiwa vijijini mnahimiza Wakandarasi," alipongeza.
Akizungumzia jengo la REA alilolizindua, Dkt.Biteko amesema litawawezesha watumishi kutoa huduma kwa wananchi na kuwapongeza REA kwa kujenga jengo hilo la kisasa lenye ghorofa tano kwa gharama ya shilingi bilioni 9.8 kwa miezi 18 badala ya shilingi bilioni 13 zilizopangwa awali.
View: https://www.instagram.com/p/DAbgS54NtFi/?igsh=MTJxcTJic2lhOGRzbQ==