Kujibu kwa jazba hakuondoi sense au facts hicho ndio main concern!
1. Kwanza huhitaji kutoa awareness kwa jambo ambalo serikali ndio anapaswa kuanzisha hatua za upatikanaji wa hiyo nishati safi hasa kwa kuondoa kodi ili watu wengi zaidi watumie, hasa watu wa kipato cha kati na cha chini ambao ndio waathirika wakubwa wa matokeo ya matumizi ya nishati km mkaa na kuni na si hao unasema wenye uwezo, wao hawana cha kupoteza na huwezi walazimisha watumie hicho unachotaka!
2. Swali la nani anawalisha kwa mwaka mzima, hili ni la kukufanya ufikiri..hao unaowataja wanakula mlo mmoja kwa siku ni watu gani? watanzania wengi wako vijijini ambako ziko fursa nyingi kuwafanya waishi zaidi ya kiwango cha kujikimu..taarifa za TASAF zinasema nini? kundi hilo unalotaja si wengi, wajane, wazee wasio na watoto wa kuwatunza, walemavu nk ambao sababu za kuwa hivyo ni za kijamii.. kijijini hakuna mtu anakula mlo mmoja km anajishughulisha na kilimo, ufundi au kazi yoyote ya kumuingizia kipato, ndio maana ya mfano wa yule alihamasisha kilimo na kuondoa usumbufu wa kirasimu kusafirisha mazao ili watu wapate stahiki ya jasho lao..alifaulu kutokuwepo kelele za kukosa chakula, hata ziada ilipatikana kusaidia jirani waliopatwa na majanga wakakosa chakula..malawi na zimbabwe, maana hasa ya mfano huu ni kukuonyesha tatizo si UWEZO na wewe ubadilishe mtizamo ulio nao kushabikia matokeo ya tatizo, kukosa uwezo ni matokeo ya tatizo la msingi UVIVU na KUTOWAJIBIKA kwa watu wenyewe na wale wana jukumu la kusimamia watu wasile mlo mmoja unaoushabikia!
3. matumizi ya nishati safi hata tu ukianza na kundi la watu waajiriwa wote wakamudu kutumia nishati hiyo matokeo ya badiliko ni makubwa, kimapato na kimazingira..miti haitakatwa kwa kiwango kikubwa vile wanunuzi wa kuni na mkaa wamepungua, kwa hivyo si lazima kwa mara moja wote tutumie nishati safi la, pako pa kuanzia ili kunusuru misitu na uharibifu wa mazingira..walimu, matabibu, polisi, wanajeshi, wafanyabiashara ni kundi kubwa kwa kuanzia kabla ya hao unawaita wasio na uwezo..
4. sijui ni mazingira gani ya kijijini unayoeleza ambako nyumba za mabati hakuna wakati takwimu za sensa ya 2022 zinasema asilimia 77 ya watanzania wana nyumba bora za kuishi, ni za matofali hata km ni udongo na zimeezekwa kwa bati
https://www.nbs.go.tz/uploads/statistics/documents/sw-1719124055-04. Building_Census2022_English08April.pdf
km mtu ana nyumba ya bati atashindwa kununua mtungi japo ule mdogo au ule mkubwa ambao umeboreshwa kiteknolojia ili anunue kulingana na matumizi yake..? na hivyo ndio serikali inapaswa kufanya! mbona kuleta Luku za tanesco serikali waliweza?
Tusiwe mashabiki kushabikia matokeo ya matatizo yetu wenyewe, tutafute majibu..serikali ifanye wajibu wake, huwezi kila siku unaimba awareness..!tenda kwanza wewe kwa kiwango cha uwezo wako kabla ya kuita wengine kukusaidia!